Katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir Tweve akipokea miche ya miti kwa niaba ya wananchi wengine mbele ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita
Na Fredy Mgunda,Iringa.Wadau wa misitu mkoani Iringa
wameipongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti
la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kugawa miti milioni moja kila mwaka
kwa wananchi na taasisi mbalimbali zinazolizunguka shamba hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche ya miti ,katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir Tweve alisema kuwa uongozi wa shamba la Sao Hill umekuwa ukitoa miti na elimu ya utunzaji wa miti kwa wananchi wanalizunguka shamba hilo.
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa
elimu ya uhifadhi misitu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanajihusisha
nawasiojihusisha na zao la miti kwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira
yasihalibike kwa njia mbalimbali kama vile kuchoma moto au kukata miti hovyo.
Dr Tweve aliongeza kuwa kitendo
cha TFS Mufindi kutoa miche milioni moja kunasaidia kuwakumbusha wananchi
kupanda miti na kuitunza vizuri hadi pale itakapofika muda wa kuvunwa kutoakana
na aina ya mitia ambayo wameipanda.
Alisema kuwa uchumi wa wilaya
ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla unategemea misiti hivyo zao la miti
linachangia kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na kueleta maendeleo kwa
ujumla kwa wananchi wa mkoa wa iringa nan je ya Iringa.
Dr tweve aliwaomba uongozi wa wakala
wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo
wilaya ya Mufindikutoa elimu ya uvunaji wa miti ili kuepukana na wananchi
kuvuna miti ikiwa bado haijakomaa kuvunwa na kupeleka bidhaa ambayo haihitajiki
sokoni.
“Sasa hizi imezuka tabia ya
wananchi wanaomiliki mashamba binafsi kuvuna miti ambayo haijakomaa kuvunwa
kutoka na hali ya uchumi hivyo niwaombe mfike kwa wananchi na kutoa elimu hiyo
kipindi mnatoa miche na baada ya miche hiyo kupandwa” alisema Dr tweve
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Peter Tweve aliwashukuru wakala wa huduma
za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya
Mufindi kwa kazi kubwa wanayifanya ya kutunza maziringa na kutoa elimu ya
mazingira kwa wananchi wanaolizunguka shamba hilo.
Alisema kuwa wananchi wa wilaya
ya Mufindi kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea Misiti hiyo kitendo cha Sao
Hill kutoa miche kwa wananchi kunahamasisha wananchi kuendelea kupanda miti na
kutunza mazingara.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la
miti la Sao hill Juma Mwita alisema kuwa wameyapokea mawazo ya wadau na kuahidi
kuyafanyia kazi ikiwapo swala la kutoa elimu kwa wananchi wanaovuna miti mapema
kabla ya muda wake.
Alisema kuwa wakala wa huduma za misitu Tanzania
(TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi wamekuwa
wakitoa elimu hiyo na wataendelea kutoa elimu mara kwa mara lengo la wananchi
wawe na uelewa wa utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment