Na Fredy Mgunda,Iringa.
Chama cha wafanyabiashara wa nguzo ambazo
hazijawekwa dawa (UWANGUTA) wamepanga kupeleka kilio kwa waziri wa nishati kwa
kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye viwanda na makapuni ambayo yamekuwa
yakinunua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabiasha hao.
Akizungumza kwenye mkutano wa
wafanyabishara hao,mwenyekiti wa UWANGUTA Negro Sanga alisema kuwa makampuni
ambayo yamekuwa yakinunua nguzo hizo yamekuwa yakiwacheleweshea malipo
wafanyabisha hao na kuwa pelekea kupata hasara mara kwa mara.
Alisema wafanyabishara hao
wanakutana na changamoto ya mitaji kutokana na kutegemea kukopa kwenye benki
mbalimbali ili kuendesha biashara ya nguzo hivyo kucheleshwa kwa malipo kutoka
kwenye kampuni hizo kunawasababishia kulimbikiza au kukua kwa riba katika benki
ambazo wanakuwa wamekopa fedha hizo.
Sanga aliongeza kwa kusema kuwa
lengo la kwenda kumuona waziri wa nishati Dr Medard Matogolo Kalemani ni kufikisha kilio cha
kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye kampuni ambazo wamekuwa wakiziuzia nguzo
hizo tofauti na alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli alipokuwa kwenye ziara mkoani Iringa.
“Mheshimiwa Rais alitoa wiki
mbili kuhakikisha kuwa sisi wafanyabisha wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa
tuliambiwa tulipwe baada ya wiki mbilia ila hadi sasa bvaadhi yetu wamelipwa na
wengine hadi hizi sasa tunavyoongea Zaidi ya wafabiashara mia moja (100)
hawajalipwa fedha zao” alisema Sanga
Sanga alimalizia kwa kusema
kuwa wameamua kwenda kwa waziri baada ya kufanya kila jitihada kushindikana
kutatua changamoto hiyo ya kulipwa kwa wakati kama iliyokuwa miaka ya nyuma
hivyo kwa pamoja wameamua kufunga safari kwa kwenda kutoa malalamiko kwa waziri
wa nishati.
Nao baadhi ya wafanyabisha wa
nguzo ambazo hazijawekwa dawa waliomba serikali kuzitambua kampuni zote na
viwanda ambavyo vinanua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabisha hao ili kuondoa
ubabaishaji kutoka kwenye kampuni hizo.
Walisema kuwa kampuni nyingi
mara kwa mara husema kuwa hawajalipwa kutoka katika shirika la umeme Tanzania (TANESCO)
hivyo kunasababisha kuwacheleweshea malipo hayo kwa wafanyabishara wa nguzo
ambazo hazina dawa.
Waliongeza kuwa kuna baadhi ya
wafanyabishara hao wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa hawajalipwa toka mwaka jana
2020 mwezi wa tisa kutoa kwenye kampuni ya New forest iliyopo mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment