Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akifafanua
jambo alipotembelea kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)
mkoani Rukwa hivi karibuni.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga (katikati)
akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Veta mkoani Rukwa. Kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi wa Veta wa wizara hiyo, Margaret Mussai na Msimamaizi
Mkuu wa Ujenzi wa chuo hicho, Jeremiah Longido.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga amesema
Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kukamilisha
ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha mkoa wa
Rukwa.
Amesema
utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza ulifadhiliwa kwa mkopo
kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na kujengwa na Mkandarasi
ambapo mradi ulifikia asilimia 52.
Mhe
Kipanga ameeleza kuwa kwa sasa ujenzi utakamilishwa kwa fedha za
Serikali kwa kutumia utaratibu wa force akaunti na unatarajia kukamilika
ili kuwezesha kuanza udahili Mwezi Julai 2021.
"Napenda
kuwatoa wasiwasi wana Rukwa kwani Serikali sasa imetenga Shilingi
bilioni 2.5 za kukamilisha ujenzi wa chuo hiki na kwamba tunatarajia
ndani ya muda mfupi fedha hizi zitalipwa ili ujenzi uweze kukamilika
ifikapo Julai, 2020," amesema Kipanga.
Awali,
akitoa taarifa ya mradi huo, Msimamizi Mkuu wa mradi, Jeremiah Longido
amesema awamu ya kwanza ya ujenzi ilianza mwaka 2018 na mpaka sasa
umefikia asilimia 52 ambapo umegharimu jumla ya Shilingi bilioni 3.6.
Naye
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Carolius Misungwi ameishukuru Serikali kwa
kutoa fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa chuo hicho na kuahidi ofisi
yake kutoa ushirikiano katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa
wakati.
No comments:
Post a Comment