Katika kipindi kuanzia mwezi Desemba 2020 hadi mwezi Februari 2021 Chuo cha Ardhi Morogoro kimefanya upimaji wa viwanja elfu arobaini mia nane kumi na tatu (40,813), kati ya hivyo viwanja 19,102 vipo Jijini Arusha katika Mitaa ya Mlimani (9,420), Msasani (1,349), Muriet (5,820), Mtaa wa Mashariki (1,041) pamoja na Mtaa wa FFU (1,552). Viwanja vingine ni Manispaa ya Iringa viwanja 2,385 Halmashauri ya Rombo viwanja 1,523 Halmashauri ya Wilaya Same viwanja 176, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi viwanja 1,076.
Kwa upande wa Dar es salaam, Chuo cha Ardhi Morogoro kimepima Halmashauri ya Jiji (Ilala) viwanja 5,981. Manispaa ya Temeke viwanja 1,112. Manispaa ya Kigamboni viwanja 2,675. Pamoja na Manispaa ya Kinondoni viwanja 1,000. Mkoa wa Mtwara, Chuo cha Ardhi Morogoro ndani ya muda huo kimepima viwanja 1,084 katika Halmashauri ya Nanyumbu, huku viwanja 4,699 vikiwa katika eneo la Manispaa ya Morogoro.
Ni mara ya kwanza katika shughuli za urasimishaji makazi, kampuni binafsi au taasisi kufanya upimaji mkubwa kiasi hicho kwa kutegemea michango ya wananchi. Mkuu wa Chuo hicho Bw Huruma Lugalla amesema kwamba huo ni mwanzo tu kwani mpango mkakati mpya wa Chuo wa miaka mitano kuanzia 2021 – 2024 umejaa maboresho makubwa na kasi ya ajabu kuhakikisha Taasisi hii pekee ya serikali inayozalisha wataalamu wa upimaji na ramani katika ngazi ya cheti na Diploma na kwamba Watanzania wategemee mambo makubwa katika sekta ya Ardhi. Bw Lugalla ameongeza kwamba yote haya yamewezekana chini ya uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya MakaziChuo cha Ardhi Morogoro kimepitia mabadiliko makubwa ya kiutawala baada ya miradi kudhoofu kwa kipindi cha nyuma, kwa sasa mabadiliko na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kwa baadhi ya watumishi zinaonekana kuleta tija na ufanisi zaidi katika utendaji.
No comments:
Post a Comment