Waziri wa nchi
ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Watu wenye Ulemavu), Jenista
Joackim Mhagama amefanya ziara na kutembelea miradi ya maendeleo
inayotekelezwa Halmashauri ya Chalinze kwa fedha zilizotolewa na Benki
ya dunia na kusimaniwa na TACAIDS na TANROAD ili kusaidia mapambano
dhidi ya UKIMWI kwa watu wanaoishi eneo la mradi na wale wanaopita
katika eneo hilo kama wasafiri na madereva wanaopumzika katika maeneo ya
Chalinze kabla yakuendelea na safari zao ndani na nje ya Nchi ikiwemo
nchi za Maziwa Makuu.
Jenista Mhagama alibaini
ucheleweshwaji wa ukamilishaji wa Miradi hiyo inaotekelezwa Katika Kituo
cha Afya Chalinze na Mdaula licha ya fedha za utekelezaji kuwa
zimekwisha lipwa tangu mwezi Januari mwaka huu.
Akitoa kauli juu ya kusuasua kwa ujenzi huo kwa Mkandarasi, Waziri alisema:
"Sijaridhishwa
na kasi ya utekelezaji wa mradi huu ukizingatia fedha kwa ajili ya
ukamilisha wa kazi mliopewa imekwisha lipwa tangu Januari mwaka huu".
Alisema Mh. Mhagama
Aidha, alimtaka Mkandarasi aliechukua mkataba
wa kutekeleza ujenzi wa zahanati ya Mdahula, Maabara na Jengo la
ushauri nasaha kwa watu wenye maambukizi Kituo cha afya Chalinze na
Mdaula kuhakikisha anakamilisha ndani ya miezi miwili na yeye mwenyewe
atakuja kulifungua mwisho wa mwezi wa nne.
'Ninawaagiza miradi
yote mliopewa kutekeleza hakikisheni inakamilika kabla ya tarehe
25.04.2021 na nitatuma maafisa toka ofisi yangu kuja kukagua na tarehe
30.04.2021 nitakuja kuzidua huduma katika majengo haya pale nitakapo
jiridhisha kuwa yamekamilika kwa viwango vinavyohitajika' Alisema Mh.
Mhagama
Aliongeza kwa kusema, kuwa: "Lengo la Serikali yetu ya
awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wetu Msikivu Mh. Dr John Pombe
Magufuli ni kuhakikisha huduma zinazohusu mapambano dhidi ya ukimwi
zinapatikana kila eneo kwa lengo la Kutoa elimu ya mapambano dhidi ya
UKIMWI,Upimaji na Utoaji dawa za kufubaza virusi vya ukimwi zinapatikana
kila sehemu, Aliongeza Waziri Muhagama.
Aidha, alisema uwepo wa
janga la ugonjwa huo wa Virusi vya Ukiwmi ikiwemo nchi za Afrika
Magharibi na Pembezoni mwa Janga la Sahara ikiwemo Tanzania, Jambo hilo
lilipelekea Serikali kutenga bajeti na kwa kutumia wahisani kujenga
vituo hivi 20 nchi nzima ili kuzidisha mapambano haya dhidi ya UKIMWI.
Ambapo
zaidi ya Fedha za kitanzania Milioni 600 zimeletwa Chalinze ili
kukamilisha ujenzi wa Jengo la ushauri na nasaha na Maabara kituo cha
Afya Chalinze na Zahanati ya Mdaula.
Kwa upande wake, Mbunge wa
Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika ziara hiyo alimshukuru
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli kwa kuendelea kuijali Chalinze kwani nje na Milioni 600 ambazo
ametoa kwa ajili ya miradi aliokuja kuikagua Mhe. Jenista Mhagama
takribani Fedha za kitanzania Bilioni Moja zimeletwa kwa ajili ya Ujenzi
wa jengo la huduma ya mama na mtoto Hospitari ya Wilaya Chalinze iliopo
Kata ya Msoga.
Ambapo alisema jengo hilo litasaidia kunusuru maisha ya wajawazito akina mama waliojifungua na watoto.
Mbunge
alimpongeza Mhe. Jenista Mhagama kwa kuteuliwa kuwa waziri na kutaka
aendeleze kasi aliokuanayo katika kusimamia Wizara hiyo ili mambo yote
ambayo yamekua yakikwama yaweze kufanikiwa kwa mustakabari wa
Wanachalinze na Taifa kwa ujumla.
"Nina laani vikari juu ya
ucheleweshwaji wa miradi hii ulioitembelea leo kwa kua hapakuwa na
sababu kwani Kampuni lililopewa mkataba wa ujenzi (Kihure Company Ltd)
mlishalipwa fedha za mradi.
Nakushukuru kwa maagizo yako kuwa
ndani ya miezi miwili miradi yote miwili iwe imekamilika nami kama
kiongozi wa eneo hili nakuahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya
ujenzi huo kwa kushirikiana na viongozi wenzangu akiwemo Mhe. Mwenyekiti
wa Halmashauri Jeofrey Kamugisha Diwani wa Bwilingu Mhe. Nasarr Karama
na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndugu. Ramadhani Possi". Aliongeza
Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Miradi hiyo tayari baadhi ya maeneo imeshakamilika na kufanya kazi ambapo kwa Halmashauri ya Chalinze, inatarajiwa kuokoa maisha ya watu wengi kwa siku inakadiliwa kulaza malori zaidi ya 1000.
No comments:
Post a Comment