Waziri
wa Kilimo Prof. adolf Mkenda akizindua mfumo wa kilimo ujulikanao
“Kizimba Business Model ” unalenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo
biashara chini ya taasisi ya SUGECO leo mjini Morogoro.Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine Prof. Raphael Chibunda akizungumza
kwenye uzinduzi wa Kizimba Business Model leo Morogoro amesema mfumo huo
chini ya SUGECO unalenga kusukuma na kubadili kilimo kuwa cha
kibiashara na kuvutia vijana wengi zaidi kushiriki.Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akisalimiana na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kulia) leo wakati
alipozindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha
vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akitazama bidhaa inayotengezwa na mjasiliamali Fatma Mbaga (kushoto) chini ya usimamizi wa SUGECO ikiwa ni mkakati wa kukuza biashara ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji SUGECO Revocatus Kimario.
Na Farida Saidy, Morogoro.
Waziri
wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo
itaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo ili kuhakikisha kunakuwa na
mageuzi mapya katika sekta ya Kilimo kwa kufanya utafiti wa mbegu bora
za Kilimo ili kuleta tija katika Kilimo kwa ajili ya kuongeza ushindani
katika soko la dunia
Waziri
wa Wilimo Prof Mkenda alisema hayo katika ziara yake mkoani morogoro
wakati wa kuzindua mkakati mpya wa kilimo kwa utaratibu wa kizimba
ulioandaliwa na sokoine university graduate entrepreneurs cooperative
[SUGECO] tukio ambalo limewashirikisha wadau mbalimbali wenye nia ya
kuleta mageuzi kwenye kilimo
Alisema
kuwa kilimo kinachangia chini ya theluthi moja ya pato la Taifa licha
ya wakulima kukumbana na changamoto kwenye kilimo hivyo wakulima
wanahitaji fedha kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha katika kuleta
mageuzi ya kilimo
Alisema
kuwa suala la kuongeza tija katika kilimo litasaidia kuongeza pato la
wakulima na Taifa kwa ujumla, kuna haja ya kuongeza tija kwenye kilimo
ili kuwa na ushindani duniani pamoja na kusimamamia mauzo ya mazao ili
kuongeza faida kwa wakulima
“Bila
mbegu nzuri huwezi kuzalisha vizuri, tunahitaji matumizi bora ya
pembejeo na teknolojia ikiwa ni pamoja na umwagiliaji na namna ya
kuwafikia watu tunahitaji mfumo huu wa kizimba tuliozindua leo
kuharakisha namna ya kwenda haraka kuwafikia wakulima na kuleta matokeo
chanya ambayo itasambaa kwa watu na kuchukua kama mfano” alisema prof
mkenda
Alisema kuwa
mkakati wa kizimba ulipaswa kuanza mapema zaidi ili kusonga mbele katika
maendeleo ya kilimo, hivyo amesema kuwa vijana wanapaswa kupewa
kipaumbele katika uzalishaji wa mazao endapo kama watawezeshwa kupata
ardhi pamoja na mitaji
Katika
mpango mpya wa kizimba wanapaswa kupeana uzoefu na ushirikiano wa
kutosha ili kuzalisha zaidi ambapo wananchi wanahitaji fedha katika
kukuza uzalishaji huku akiwaomba wadau wa bank kutoa mikopo kuwezesha
wakulima kuzalisha mazao na kutengeneza kwa wakulima wanapozalisha mazao
yao na uhakika wa kupata masoko
Alisema
kuwa sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta zinazoajiri watu wengi zaidi
ni muhimu kupewa kipaumbele kutumika kama nguvu kazi ya taifa huku
akieleza changamoto kubwa inayokwamisha vijana ikiwa ni kukosa mitaji
pamoja na ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao
Aidha
prof mkenda alisema kuwa katika maeneo ya vijini hasa katika maeneo
yenye changamoto ya hali ya hela na uhaba wa mvua, inaonesha hali halisi
ya maisha ya wakulima hivyo utaratibu wa vizimba utasaidia kuongeza
tija katika kilimo
Wakati
huohuo ametoa wito kwa Halmashauri zote hapa nchini wasaidie namna ya
kusogeza kilimo kwa kuwa wakulima wengi wanalima bila kuwa na uhakika wa
masoko na kuuza mazao yao hivyo wajenge mazingira ya kutengeza hela ili
kupata faida
“Nawapongeza
halmashauri ya nzega kutoka hekta 40, kibiti hekta 1000, mvomero hekta
1500,na halmashauri ya liwale wametoa hekta 300 huu ni uthubutu wa pekee
sana kuongeza tija kupitia ardhi hii” alisema prof mkenda
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya SUGECO Dkt Anna Temu amewapongeza
SUGECO kubuni mbinu ya kukuza kilimo na kuwaomba waishi katika jamii ya
wakulima na wafugaji ili kujikita na mbinu za kuondoa umaskini ambayo
ndio kipaumbele cha sugeco katika mkakati wao kubuni mpango huo
Nao
wanufaika wa SUGECO Bwana Yohana Itayo na Fedrick Jonathan wameiomba
serikali kupanua wigo kusaidia vijana ili kupata ujuzi kwa vitendo
kushirikiana na wakulima wenye uzoefu hivyo wameshauri vijana
wanaomaliza vyuo wapelekwe kupata uzoefu wa kuanzisha mashamba yao wenye
joseph
Masimba ni Afisa Meneja uendeshaji wa SUGECO amesema kuwa kizimba ni
mfumo wa kuzalisha kwa pamoja ambao unaziweka rasilimali zote kwa pamoja
kujumuisha mabank, wadau wa maendeleo kilimo lengo ikiwa ni
kushughulikia changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo hasa tatizo la
tija, vijana kukosa ardhi na mitaji katika uzalishaji mazao ya kilimo
No comments:
Post a Comment