Na Grace Semfuko,MAELEZO.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amelitaka Baraza la Kiswahili Tanzania-BAKITA kufanya jitihada za kiuza nje ya nchi lugha ya Kiswahili ili iweze kujulikana kwa haraka na kuleta tija ya kiuchumi kutokana na kuzalisha ajira pamoja na ada na tozo mablimbali za ufundishaji wa lugha hiyo.
Amesema ipo haja kwa BAKITA kuwasiliana na Balozi mbalimbali zinazoiwakilisha Tanzania zinazoiwakilisha Tanzania nje ya nchi ili ziweze kutenga vyumba vya madarasa ya kufundishia lugha hiyo adhimu Barani Afrika.
Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake katika ofisi za baraza hilo huku akisisitiza kuwa, zoezi hilo lianze mara moja kwani wanaonufaika sasa na lugha hiyo, ni watu wa kutoka nchi jirani ambazo hajimudu kuzungumza na kufundisha Kiswahili fasaha kama ilivyo kwa waasisi wa lugha hiyo ambao ni Watanzania.
“Kama kuna kitu mnatakiwa kukifanya sasa ni kukiuza kiswahili nje ya nchi badala ya kuachia majirani zetu wakiuze, wakati sisi ndio hasa tuna kiswahili fasaha kuliko wao ambao wanakiuza na kunufaika sana, hapo kwa kweli BAKITA tunakwama, tena mpendwa wetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliturahisishia sana, tuliona jinsi alivyokuwa na mchango mkubwa wa kuitangaza lugha hii Duniani, na Dunia wanatambua mchango wake” amesema.
Ameitaka BAKITA kutoa mafunzo ya lugha ya Kiswahili na istilahi zake kwa watu wa fani za ushereheshaji na ukalimani ambao wanaweza kutumika katika kuikuza lugha hiyo huku akisisitiza uharakishaji wa uagizaji wa vifaa vya kutafsiria lugha mbalimbali za kimataifa kwenda katika lugha ya Kiswahili.
“Mlisema mnaagiza vyombo ambavyo vitawasaidia katika tafsiri ya lugha mbalimbali, harakisheni hilo, pia ni vyema mkaanzisha mafunzo kwa washereheshaji wetu na wakalimani, hawa wanatumia Kiswahili zaidi na wanaweza wakatumika katika kukikuza zaidi Kiswahili, wanaweza kuwa kwenye matukio ya kiserikali au ya kijamii, wapewe mafunzo na istilahi mbalimbali za kuwawezesha kukitangaza Kiswahili” amesema Gekul.
No comments:
Post a Comment