Mhandisi
Cyrian Luhemeja akitoa maelezo ya mradi mkubwa maji kuelekea eneo la
Viwanda la Zegereni wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 3 utakaorahisha
upatikanaji wa maji katika maeneo hayo na kuboresha huduma hiyo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) kwa jitihada zake katika kuboresha
huduma kwa wananchi na maeneo ya Viwanda.
Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo Aprili 27 katika ziara maalum ya kutembelea viwanda vilivyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
"Nimesikia
mikakati mizuri ya Mkoa wa Pwani, DAWASA, TANESCO na TARURA inayoleta
matumaini makubwa katika kuboresha sekta ya Viwanda". Alisema Waziri
Mkuu na kuongeza kuwa viwanda vina mchango mkubwa katika kuinua uchumi
wa nchi na kuongeza mzunguko wa fedha katika jamii inayovizunguka.
Amesema
kwa sasa sekta ya Viwanda na Uwekezaji ipo chini ya Ofisi yake na
ametoa wito kwa taasisi wezeshi za Serikali kuweka mazingira bora ya
kuvutia ili wawekezaji wakubwa na wadogo wawekeze mitaji yao.
Amesema
viwanda vina faida nyingi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla huku
akitaja faida mbalimbali zikiwemo ajira kwa vijana, upatikani wa vifaa
kwa gharama nafuu, ukuaji wa pato la Taifa na ongezeko la mapato ya
halmashauri.
Awali akitoa taarifa ya uboreshaji huduma ya
Majisafi kwenye maeneo ya Viwanda, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA
mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa Mamlaka imejipanga kuboresha
huduma za majisafi katika maeneo yake yote ikiwemo viwandani.
"Waziri
Mkuu, DAWASA inawekeza asilimia 40 ya mapato yake ya kila mwezi zaidi
ya Tsh bilioni 13.5 kwa mwezi katika utekelezaji miradi. Jitihada ambazo
zimewezesha DAWASA kufikia asilimia 92 ya wananchi ndani ya eneo lake
la huduma," amesema.
Kuhusu eneo la viwanda la Zegereni, Wilayani
Kibaha Mhandisi Luhemeja amesema tayari manunuzi ya mabomba yapo katika
hatua za mwisho na kiasi cha Tsh bilion 1.6 kati ya bilioni.3.3
zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo zimepatikana.
Luhemeja
ameishukuru serikali kwa kuendelea kuisaidia DAWASA na kumuahidi Waziri
Mkuu uwajibikaji ili kutoa mchango stahiki katika kukuza uchumi wa nchi
kupitia Viwanda.
No comments:
Post a Comment