Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amekataa ombi la Wakazi wa Rombo la kutaka kuwaua nyani na tumbili wanaodaiwa kuvamia makazi yao na kuharibu mazao kwani wanaleta fedha (dola)
Baadala
yake Waziri Ndumbaro amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori,
Dkt. Maurus Msuha kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori
(TAWIRI) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA)
kuwahamisha nyani hao kwa kuwapeleka katika Hifadhi zilizo mbali na
makazi ya Watu.
Waziri Ndumbaro ametoa agizo hilo jana wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro baada ya kupata malalamiko hayo kutoka kwa Wananchi,
Amefafanua
kuwa Wizara haiwezi kuwaua nyani hao kwa kuwa nyani na tumbili ni moja
ya vivutio vya Utalii vinavyotuletea pesa nyingi nchini kwa ajili ya
maendeleo ya Taifa.
Aidha,
Dkt. Ndumbaro ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
kuanza kufanya utafiti wa kuwapeleka nyani hao katika mazingira ambayo
yatakuwa sawa na ya Rombo ili wasiweze kupata shida yoyote kutokana na
kubadailisha mazingira.
Nyani
hao wanadaiwa kuvamia makazi na kuanza kung'anganiana chakula pamoja na
kudaiwa kuwachukua Watoto wadogo wa Binadamu na kuanza kukimbia nao
porini ambako wakati mwingine huwajeruhi.
Awali
Mbunge wa Rombo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.
Adolf Mkenda alisema licha ya nyani hao kuwasumbua Wapiga kura wake
lakini Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya
Kilimanjaro imekuwa ikifanya jitihada ya kuwaondoa nyani hao.
Hata
hivyo, Prof, Mkenda ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia
Taasisi zake jinsi inavyowasaidia Wananchi wa Rombo katika maendeleo kwa
kuwajengea shule pamoja na Zahanati.
Kwa
upande wake Diwani wa Katangara Mrere, Mallel Venance amesema nyani
hao wamekuwa tatizo sio katika kata yake tu bali ni Wilaya nzima
''Wanakuja
katika makazi yetu wakiwa katika makundi kati ya 40 na 100 na katika
baadhi ya vijiji wamekuwa wakiharibu mazao hali inayopelekea sisi kama
wazazi kushindwa kuchangia chakula katika shule ambako watoto wetu
wanasoma, Tukuomba Mhe. waziri tusaidie tunakuwa masikini kwa ajili ya
nyani hawa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa kwanza kushoto) akiwa
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakizungumza na
baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro mara baada ya
kufanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa kata ya Mashati iiliyopo
katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro
ameagiza nyani hao wanaovamia makazi ya watu wahamishiwe katika Hifadhi
zilizo mbali na makazi ya Watu. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na baadhi ya
Watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro mara baada ya kufanya
mkutano wa hadhara na Wananchi wa kata ya Mashati iliyopo katika wilaya
ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro ameagiza nyani
hao wanaovamia makazi ya watu wahamishiwe katika Hifadhi zilizo mbali
na makazi ya Watu. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Allan Kijazi
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Kata ya Mashati iliyopo katika wilaya ya
Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo amewahakikishia Wananchi hao
wanaolalamikia Nyani na Tumbili kuvamia makazi yao kuwa watahamishiwa
katika Hifadhi zilizo mbali na makazi ya Watu
No comments:
Post a Comment