Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wawekezaji wote nchini kuwa
Serikali itakidhi mahitaji yao ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuweka
sera bora na mazingira wezeshi kwa kuhakikisha uwepo wa huduma muhimu za
maji, umeme, ardhi na barabara na kuwataka kuwaalika marafiki katika
nchi zao na nje ya mipaka kuja na kuwekeza nchini kwa kuwa sera na
mazingira ya uwekezaji ni rafiki zaidi.
Akizungumza leo mara baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA Assemblers kilichopo Kibaha mkoani Pwani Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango wa wawekezaji nchini na itawaunga mkono kwa kuhakikisha changamoto zilizopo ndani ya uwezo wa Serikali zinapatiwa ufumbuzi.
"Mkoa wa Pwani una viwanda vya kutosha na bado maeneo yapo mengi, Mkuu wa Mkoa yupo na wawekezaji wenye uhitaji wa maeneo Serikali ipo kwa ajili yenu na tunawaunga mkono wakati wote." Amesema Majaliwa.
Waziri Majaliwa ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kuwa kinara na kutumia fursa ya kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wenye viwanda.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi. Evarist Ndikilo amesema, Mkoa wa Pwani una viwanda 1438 huku viwanda vikubwa vikiwa 82 kikiwemo kiwanda cha GFA Assemblers.
"Mwaka 2015 tulikuwa na viwanda 300, hadi sasa tumefikia idadi ya viwanda 1438 kwa ongezeko la viwanda 3100 ambavyo vimetengeneza ajira za moja kwa moja 50,0000 na ajira za muda 10,0000." Amesema Ndikilo.
Aidha amesema kuwepo kwa viwanda hivyo katika mkoa huo umepaisha mapato ya Mkoa huo hadi kufikia bilioni 147 na bado uwekezaji wa viwanda mkoani humo unashika kasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Aljawad Karimal ameiomba Serikali kutoa vipaumbele zaidi kwa sekta binafsi hasa katika masoko na sera za uwekezaji ili kuendelea kujenga taifa la viwanda.
Aljawad amesema wanajivunia uwekezaji walioufanya nchini hasa kwa kuwa kiwanda cha kwanza cha kuunganisha magari ya aina zote na kuiomba Serikali kuwapa masoko kupitia Halmashauri na taasisi zake ikiwemo jeshi na hospitali kwa kuwapa kazi za kuunganisha magari ya kutolea huduma.

mkuu Kasimu Majaliwa akisikiliza maelekezo kutoka kwa, Elizabert Mwaya
wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari
GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani Pwani jana.kulia ni
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Ally Jawad Karmali.Picha na Said Khamis
Waziri
mkuu Kassimu Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa kiwanda cha
kutengeneza magari cha GFA-Vehicle Assembling,Aljawad Karimal kilichopo
Kibaha wakati wa ziara ya kukagua kiwanda hicho. Kulia ni Mkuu wa
mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo.Picha na Said Khamis
Waziri
mkuu Kasimu Majaliwa akisikiliza maelekezo kutoka kwa Baraka Samson
,wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari
GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani Pwani jana. Wa pili kulia
ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Ally Jawad Karmali.
No comments:
Post a Comment