Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene ameipongeza timu
ya watendaji na wataalamu kutoka Tanzania kwa kufanikisha ziara ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya
nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021.
Dkt.
Simbachawene ametoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini
Nairobi alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na
Biashara.
“Nawashukuru
na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa
ziara ya Mhe. Rais, ni wazi kuwa kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri
wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema Dkt.
Simbachawene.
Amewataka
watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yale yote
yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizi ili
kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hvyo
kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote
mbili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya
ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa mwenyeji wake
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Ziara hiyo ilifanyika
tarehe 4-5 Mei 2021 na kushuhudia makubaliano kati ya Tanzania na Kenya
kuhusu kushirikiana kwenye masuala ya utamaduni na ujenzi wa bomba la
gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa yakisainiwa kwa ajili ya
utekelezaji
Katika
ziara hiyo Viongozi wa nchi hizo walikubaliana kuondoa vikwazo vya
biashara vilivyopo baina ya nchi hizo vinavyozuia uwekezaji na biashara
katika nchi hizo na hivyo kushindwa kukuza uchumi wa nchi hizo .
|
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene akizungumza
na watendaji na wataalamu kutoka Tanzania waliokuwa nchini Kenya kwa
ajili ya kuhakikisha ziara ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
nchini Kenya inafanyika kwa mafanikio |
|
Watendaji
na wataalamu kutoka Tanzania ambao walikuwa nchini Kenya kwa ajili ya
kufanikisha ziara ya Rais alipoitembelea Kenya tarehe 4-5 Mei 2021
wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Ubalozi wa Tanzania jijini
Nairobi. |
|
Baadhi
ya watendaji na wataalamu kutoka Tanzania wakizungumza na Balozi wa
Tanzania nchini Kenya Mhe. Simbachawene katika Ubalozi wa Tanzania
jijini Nairobi. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Simbachawene akiwa na Mkurugenzi wa
TanTrade Bw. Edwin Rutagaruka na Mkurugenzi wa idara ya Afrika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikian wa Afrika MasharikiBw. Frank Mwega katika
Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi. |
|
|
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Simbachawene (katikati) akiwa na
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Maduhu Kazi (wa
kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje
(EPZA) (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto)
walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene (katikati)
akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Maduhu Kazi
(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya
Nje (EPZA) Bw. (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili
kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Bw.
Frank Mwega na maafisa Ubalozi walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa
Mhe. Balozi jijini Nairobi. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene (katikati)
akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Maduhu Kazi
(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya
Nje (EPZA) Bw. (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili
kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Bw.
Frank Mwega na maafisa Ubalozi walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa
Mhe. Balozi jijini Nairobi. |
|
|
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Tanzania waliofanikisha
ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan aliyoifanya nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021. |
No comments:
Post a Comment