Na. Beatrice Sanga - MAELEZO
Sekta
ya Habari na Utangazaji ni moja ya sekta inayotoa huduma kwa jamii ya
watu wengi nchini ambayo ni haki ya msingi ya raia kama inavyoonekana
kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Aidha kutoa na kupokea habari kunatambuliwa duniani kote kuwa ni moja ya haki za binadamu ambapo Umoja wa Mataifa, na umoja wa afrika zina matamko rasmi ambayo Serikali imeridhia kuhusu haki ya kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote. haki hii kama zilivyo haki nyingine zote, hutolewa kwa kuzingatia wajibu wa kila raia kwa jamii na uhuru binafsi wa binadamu
Mei 3 kila mwaka Tanzania pamoja na
nchi nyingine Ulimwenguni huadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
tangu Umoja wa Mataifa ulipoidhinisha siku hiyo ikiwa na lengo la
kuwapatia watu taarifa na elimu za kujenga demokrasia na maendeleo
katika sekta ya habari
Mwaka huu 2021 kilele cha maadhimisho haya
nchini Tanzania yamefanyika Jijini Arusha na kujumuisha washiriki
kutoka sekta ya habari inayojumuisha Serikali kupitia Idara ya Habari
MAELEZO, vyombo vya habari binafsi na vya Serikali, Mashirika ya
Kimataifa, wadau wa maendeleo na asasi zisizo za kiserikali na wadau
wengine mbalimbali wameshiriki kwa kufanya midahalo mikubwa pamoja na
waandishi wa habari kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo
la kutangaza vivutio vyetu na kuutangaza urithi wa dunia na kwa
madhumuni ya kuvutia watalii.
Mwaka huu maadhimisho haya yamekuja na kauli mbiu ya "Habari kwa Manufaa ya Umma" ambayo inasaidia kujua namna ambavyo habari zinamanufaa kwa umma,ikiwemo haki ya kikatiba ya kupata habari na kwa mwaka huu Jamhuri ya muungano wa tanzania katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari imejikita katika maeneo makuu matano ya vipaumbele ambavyo ni Uhuru wa vyombo vya habari vinavyofaa, kuendeleza nguvu kazi, mazingira mazuri ya sheria na sera, ikiwa ni pamoja na hali bora ya kazi, ulinzi na usalama wa waandishi na kujua kufanya kazi za kiuandishi, ikiwa ni pamoja na uelewa wa matumizi ya kidijitali
Katika kuhakikisha habari zinanufaisha umma Serikali
imedhamiria kuweka mifumo ndani ya vyombo vya habari inayowalazimisha
kuleta matokeo chanya hasa ya matumizi ya sheria hususani kwa wahariri
na watekeleza sera kama Maafisa Utumishi, ikiwa ni sambamba na kupitia
upya sera ya vyombo vya habari ya mwaka 2003.
katika hotuba
iliyotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent
Bashungwa alisema kuwa, Serikali itaboresha mazingira katika sekta ya
habari ili Waandishi wa Habari watekeleze majukumu yao bila hofu, na kwa
kujiamini.
"Serikali itaendelea kuboresha mazingira katika sekta
ya habari ili muweze kutekeleza majukumu yenu bila hofu, na kwa
kujiamini huku mkizingatia sheria, kanuni, maadili na weledi ili
wananchi waweze kupata habari sahihi kwa ajili ya manufaa na maendeleo
yao,"amesema Bashungwa
Waziri Bashungwa alisema ili kuweza
kuendana na lengo namba 16 la Maendeleo Endelevu (SDG16), Tanzania
itahitaji kuwa na ukusanyaji wa fedha wenye tija na wa kudumu, takwimu
zenye ubora zinazozalishwa na kushirikishwa kwa umma, ambapo matokeo
yake yanaweza kufanyiwa majaribio na kupimwa maendeleo yake.
"Ni
muhimu kuwa na mpango wa maendeleo ili kuviwezeshe vyombo vya habari
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi. Waandishi wa Habari
wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu mbalimbali zikiwemo za
matunzo, na mishahara midogo kwa wafanyakazi, mapato yasiyotosheleza, na
kukosa kinga bima ya afya kwa waandishi pamoja na wasaidizi wao. Mambo
haya yamekuwa ni tatizo na kuleta wasiwasi kwa wanahabari," amesema
Bashungwa.
Aliendelea kueleza kuwa, Serikali inahimiza wadau wote
wa habari, kuhakikisha wanaweka utaratibu utakaowezesha kufanya
ufuatiliaji, na uwajibikaji katika kutekeleza sera na sheria za nchi,
pamoja na miongozo kwa umma na jamii kwa ujumla. Miongozo hiyo izingatie
kuwepo kwa mazingira na hali bora ya kazi, ulinzi na usalama wa
waandishi, kujua kufanya kazi za kiuandishi, ikiwa ni pamoja na uelewa
wa matumizi ya kijiditali.
"Serikali ya awamu ya sita inathamini
na kutambua uhuru wa vyombo vya habari na katika muktadha huo hivi
karibuni Serikali ilivifungulia vyombo vya habari vya kielektroniki vya
online TV vilivyokuwa vimefungiwa kwa makosa mbalimbali ili kuhakikisha
kuwa vinafanya kazi kwa uhuru na kukuza ajira za vijana nchini,"amesema
Bashungwa.
katika kuonesha uhuru wa vyombo vya habari nchini,
Waziri Bashungwa alieleza kua Tanzania ni miongozi mwa nchi chache zenye
vyombo vingi vya habari Barani Afrika ambapo mpaka sasa kuna jumla ya
Magazeti 246, Televisheni 53, Redio 194, Redio za Mtandaoni (Online
Radio) 23, Blogs 120 na Televishenio Mtandao (Online TV) 440. ambapo
ishara kuwa nchi yetu inathamini na kuenzi vyombo na taaluma ya habari,
na kusema Serikali iko tayari kushirikiana kuhakikisha na kunakuwepo na
uwazi katika upatikanaji wa habari kwa Watoa Huduma ya Mitandao, kama
sehemu muhimu ya habari kwa manufaa ya umma.
“Ni vyema mkatambua
kuwa jukumu lenu kubwa kama washiriki katika mjadala huu ni kuhakikisha
kuwa mapendekezo mtakayotoa yataleta mafanikio. Mafanikio hayo
yatapatikana iwapo wadau wote tutashirikiana kikamilifu katika
utekelezaji wa mapendekezo na maazimio. Kwa upande wa Serikali ya Awamu
ya Sita (06) inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, tunawahakikishia
ushirikiano mkubwa.” Amesema Bashungwa
Pia Waziri ametoa wito
kwa Viongozi mbalimbali ndani ya Serikali kuhakikisha anaondoa vikwazo
na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pale wanapohitaji taarifa
muhimu kwa Manufaa ya Umma na maslahi ya Taifa letu kwa ujumla.
Kuhusu
changamoto Waziri Bashungwa amesema anazitambua changamoto nyingi
zinazowakumba aandishi wa habari wakati wa kutekeleza majukumu ya kila
siku, zikiwemo kunyimwa taarifa bila sababu ya msingi hata kama
mwandishi anakuwa na kitambulisho kilichotolewa na Serikali
kumtambulisha kama ni mwandishi wa habari. na kuahidi kuwa Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
inazitambua changamoto hizo na itaendelea kuboresha mazingira katika
sekta ya habari ili kuwawezesha kutekeleza majukumu ya kiuandishi bila
hofu, na kwa kujiamini na kwa kuzingatia sheria, kanuni, maadili na
weledi ili wananchi waweze kupata habari sahihi kwa ajili ya manufaa na
maendeleo ya Taifa.
Sambamba na hilo, waziri bashunga ametoa pongezi nyingi kwa Shirika la Umoja amataifa , elimu sayansi na utamaduni (UNESCO) kwa kuendelea kuiunga mkono na kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuendeleza uchumi a nchi yetu na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo"kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano a Tanzania, ninapenda kuwapongeza na kuwashukuru UNESCO ka kushirikiana na Serikali katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu. niwapongeze kwa kusaidia kufanikisha maadhimisho haya, tangu mwanzo hadi mwisho. UNESCO mmekuwa mkiipatia Tanzania misaada ya kiufundi, kwa zaidi ya miaka arobaini na saba (47) sasa. Hivyo sisi kama serikali, hatuna budi kuapongeza, na kuaahidi ushirikiano mkubwa kutoka kwetu" amesema Bashungwa.
No comments:
Post a Comment