Na. Catherine Sungura-Dodoma
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy
Gwajima amewahakikishia wakunga kwamba Serikali itaendelea kusimama nao
vema ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia akina
mama kujifungua salama.
Dk.
Gwajima ametoa pongezi hizo mapema leo alipozungumza kupitia kipindi
kimoja kinachorushwa na Kituo cha Radio hapa nchni kilichokuwa na mada
kuhusu Siku ya Wakunga Duniani ambayo hufanyika Mei 5, kila mwaka.
Amewapongeza
wakunga na wadau wote waliofanikisha maadhimisho ya siku hiyo nchini
hususan UNFPA (Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya
Idadi ya Watu).
“UNFPA
wametuunga mkono siku zote kuhakikisha tunakwenda vizuri na agenda hii
ambayo wao wanaisimamia vema kuhusu idadi ya watu duniani na maisha
bora ikiwemo masuala ya afya.
“Siku
ya leo tutakuwa tunaelekeza nguvu nyingi kuangalia vipaumbele vyote vya
Umoja wa Mataifa (UN) na malengo yake 17 (SDGs), lengo namba tatu
linahusu watu wa afya na ustawi wa jamii yetu tunavyoihudumia.
Ameongeza
“Wakunga wanafahamu siku ya leo kauli mbiu inaeleza tuongozwe na
takwimu maana ndiyo eneo muhimu litatufanya tuweze kujipima kama
tutafika hayo malengo ya 2030.
“Katika
malengo haya ambayo tumejiwekea kwamba vifo vya uzazi vitokomezwe
kabisa, isifikie kwamba mama anabeba ujauzito anakwenda kujifungua
anapoteza maisha au mtoto anapoteza maisha.
“Mchezo
huu unawahitaji wakunga, wao ndiyo Baraka ya kwanza kabisa ya kiumbe
hai ambacho mungu amekileta duniani, nini jukumu letu tunatakiwa
tuwasaidie, tuwajali, tuwaenzi, wawe na imani.
“Kwa
sababu kama wakirudi nyuma kwenye hotuba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa
Nchi, Samia Suluhu Hassan, alipokuja bungeni alisema kwamba mradi huu
wa masuala ya kuboresha huduma za uzazi wajawazito, wazazi na watoto
wasifariki ni mradi wake wa moyoni.
“Kama
Rais amesema ni mradi wa moyoni na ameniamini mimi na kunipa dhamana
kusimamia sekta hii mimi ndiyo nazama kabisa moyoni mwake kabisa mzima
mzima,” amesisitiza.
Dk.
Gwajima ameongeza “Kwa hiyo naunga na mheshimiwa Rais. kwamba na mimi
mradi huu ni wa moyoni mwangu na nitahakikisha nasimama na wakunga.
“Kuhakikisha
kwamba tunawekeza kuwahakikishia wana uwezo wa kitaaluma mahitaji,
miundombinu wanayohitaji, dawa zote na wanafanya kazi zao vizuri
kuhakikisha wanakuwa Baraka kwa mtoto huyu anayezaliwa mikononi mwao,
wao wakiwa wanafungua njia ya maisha bora yenye afya na furaha kwa mtoto
huyu ambaye ni Taifa la kesho,” amesema Dk. Gwajima.
No comments:
Post a Comment