Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
Kilimo
cha parachichi kinaendelea kukua hasa katika nchi za Afrika Mashariki, Pia
kilimo hichi hakihitaji fedha nyingi na subira ya ukuaji wa matunda haya mara
nyingi huambatanishwa na faida kubwa wakati wa mavuno.
Kwa
Tanzania, kilimo hichi kimeanza kushika kasi zaidi mwaka 2015 ambapo baadhi ya
watu walijitokeza na kuelezea mafanikio waliyopata kutokana na kilimo cha
parachichi.
Nchi
za Ulaya kama Denmark, Ufaransa, Uingereza, Norway na Uholanzi zimeonyesha
kufurahishwa na maparachichi yanayotoka nchi za Afrika Mashariki hususani
Tanzania. Mikoa iliyojikita zaidi na uzalishaji wa zao hili ni Kilimanjaro, Mbeya,
Njombe na Iringa, hii ni kutokana na hali ya hewa ya baridi iliyopo katika
mikoa hiyo.
Kufuatia
umuhimu huo wa zao la parachichi Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda leo
tarehe 3 Juni 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mhe Queen Sendika Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Katika
mazungumzo yao Waziri Mkenda amemuhakikishia Rc Sendika kuwa Wizara ya Kilimo
imejipanga kuimarisha sekta hiyo katika zao la Parachichi ambapo miongoni mwa
mikoa ya kimkakati katika zao hilo ni pamoja na mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Mhe Queen Sendiga ambaye katika mazungumzo hayo aliambatana na Katibu
Tawala wa Mkoa huo Bi Happiness Seneda amesema
kuwa Mkoa wa Iringa hutegemea miche ya Parachichi kutoka mikoa ya Njombe na
Iringa hivyo jambo hilo huchelewesha kasi ya uzalishaji wa Parachichi.
Kufuatia changamoto hiyo Rc Sendika amemueleza Waziri Mkenda kuhusu uhitaji wa miche mingi ya Parachichi ikwiemo uwezekano wa kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche hiyo kwa wingi mkoani Iringa.
Wapewe jicho la pekee kupatiwa miche na ikiwezekana kuwe na uzalishaji wa miche ya Parachichi Mkoani Iringa
Amesema
kuwa wakulima wengi wanaojihusisha na kilimo hicho huuza katika soko la nje
hivyo kuna umuhimu kwa serikali kuwezesha vijana nchini hasa wasio na kazi za
kuajiriwa kujihusisha na kilimo hiki kwa kuwa hakina gharama.
No comments:
Post a Comment