Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DAWASA imepiga hatua kubwa
katika usimamizi wa miradi ya maji nchini ikiwemo matumizi mazuri ya
fedha zinazopatikana katika Mamlaka hiyo kwa kuwekeza kiasi cha Shilingi
Bilioni 17.8 katika Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua
kero ya Maji kwa Wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika ziara hiyo, Naibu Waziri, Mhandisi
Maryprisca Mahundi amewapongeza DAWASA kwa kujituma kutekeleza Miradi
hiyo ya kimkakati ili kutatua kero ya Maji katika sehemu mbalimbali za
mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Pia
amepongeza Watumishi, Wasimamizi wa Miradi yote ya DAWASA wakiongozwa
na Afisa Mtendaji Mkuu, Cyprian Luhemeja katika kufanikisha utekelezaji
wa Miradi hiyo takribani 27 sehemu mbalimbali ya Dar es Salaam na Pwani.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA, Mhandisi
Ramadhani Mketo amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi
utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na
Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu wanalaza mabomba kwa umbali wa
Kilometa 59 katika Mitambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.
Amesema
pia mradi huo utatatua kero ya Maji katika Bandari Kavu ya Kwara na
kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR Kwara, amesema Lita 9,300,000 za
Maji zitatumika kwa siku baada ya kukamilika Mradi huo.
Naye,
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhwan Kikwete amesema ujio wa Naibu
Waziri wa Maji katika Maeneo hayo itasidia katika utekelezaji wa Miradi
hiyo ya Maji na kuondoa kero kwa Wananchi wake.
Mkurugenzi
wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa
ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi
kuhusu ulazaji wa Bomba za inchi 10 zinazolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka
Mboga yenye kilometa 58.9 kwenye Mradi wa Chalinze- Mboga unaotekelezwa
na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi
Ishmael Kakwezi
Muonekano wa Bomba la inchi 16 linalolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga litakalokuwa na kilometa 58.9
Kazi ikiendelea
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata maelezo kutoka
kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu
ulazaji wa Bomba unavyopita kwenye ramani kuanzia Ruvu Juu mpaka Mboga
kilichopo Wilaya ya Bagamoyo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi
mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akikagua mradi wa
ulazaji wa mabomba ya inchi 16 katika eneo la Kitongoji cha Mbala
kilichopo Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi
ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Kazi ikiendelea
Msimamizi
wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa
Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu mradi wa kujenga pampu ya kusukuma maji
katika Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara ya naibu Waziri wa maji
alipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Msimamizi
wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa
Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga wakati
wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akiendelea na Ziara
yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Mkurugenzi
wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na
DAWASA wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca
Mahundi.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
namna wanavyosimamia miradi hasa ya maji ili kuondoa hadha kwa wakazi
wa Chalinze ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama
wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca
Mahundi alipokuwa anatembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
No comments:
Post a Comment