Na Marco Maduhu, Shinyanga
Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ana tarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye
maonesho ya biashara ya Teknolojia na Madini mkoani Shinyanga.
Maonesho hayo yatafanyika kuanzia Julai 23 mwaka huu hadi Agost Mosi, katika viwanja vya Butulwa, Kata ya Old Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, amebainisha hayo leo wakati
akizungumza na vyombo vya habari ,kuwa maonesho hayo ni ya awamu ya
pili, ambayo yamelenga kukuza Sekta ya Madini na biashara mkoani humo.
Alisema
Mkoa wa Shinyanga una migodi mingi ya madini , hivyo kupitia maonesho
hayo, yatatoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani humo, pamoja na
kuunganisha mtandao wa wafanyabiashara.
"Maonesho haya ya
Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, yatatusaidia kukuza
uchumi wa Mkoa wetu, na pato la mtu mmoja mmoja, na Taifa kwa ujumla,
na tuta yafungua Julai 23, na Mgeni Rasmi atakua Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa," amesema Dk. Sengati.
"Tunaomba wananchi wajitokeze kwa
wingi kwenye maonesho haya, kuja kuona madini live, pamoja na wafanya
biashara wajumuike ili wapate mtadao na kukuza biashara zao," ameongeza.
Naye Mwenyekiti wa Maonesho hayo Kulwa Meshack, ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA)mkoani Shinyanga, alisema maonesho hayo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara, ambapo watabadilisha uzoefu namna ya kufanya kazi zao.
No comments:
Post a Comment