Na.WAMJW- DSM
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo
amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo
wamekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya Tanzania na
Uswisi.
Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi huyo kuendelea
kusaidiana na Serikali ya Uswisi na katika mazungumzo yao wote wawili
wamekubaliana kufadhili uimarishaji mfuko wa afya ya pamoja (HBF),
mifumo ya afya pamoja na huduma zote za mtandao katika vituo vya kutolea
huduma za afya nchini.
Naye, Balozi Mhe. Didier Chassot amesema
Uswisi iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta mabadiliko
chanya katika sekta ya afya hususani katika swala zima la kuimarisha
mifumo ya vituo vya afya na huduma za mtandao.
Viongozi hao wamekutaka na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Wizara mkoani Dar es Salaam, ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe OR- TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment