Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga katika picha ya pamoja na Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, akieleza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Ikulu Jijini Dar es Salaam
*************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Katanga amekutana na ugeni huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sulluhu Hassan. Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) katika nyanja za biashara na uwekezaji pamoja na Ulinzi na Usalama.
Balozi Katanga amemhakikishia Waziri huyo kuwa Tanzania inayo mazingira mazuri ya biashara na salama kuwekeza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoka kwa Umoja huo wakati wote.
Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan amewasili nchini leo kuja kushiriki Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment