Matokeo chanyA+ online




Friday, April 22, 2022

WAZIRI BASHE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA KAMPUNI YA S.J. SUGAR TANZANIA

 Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya S.J. Sugar Tanzania Private Limited inayofanya uwekezaji   katika Kilimo cha  miwa na uzalishaji wa sukari  mkoani Mtwara. 

Waziri Bashe amekutana na viongozi wa kampuni hiyo ofisini kwake jijini Dodoma. 

Katika mazungumzo hayo,  Mkurugenzi wa kampuni ya S.J. Sugar Tanzania Private Limited, Bw. Hasnain Murji ameiomba Serikali kuipatia kampuni hiyo ekari 100,000 kwa ajili ya uzalishaji wa Alizeti na  mafuta katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Bw. Murji aliambatana na Mkurugenzi wa Fedha Bi. Meera Ghadigaonar, mtaalam wa umwagiliaji wa kampuni hiyo Prof. Fulaji Namdeo na Bw. Patil Jayant ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni. 

Mbali na mazungumzo na Mhe. Waziri, Viongozi hao wa kampuni walimuonesha Mhe. Bashe sampuli ya alizeti waliyoizalisha kwa majaribio katika kijiji cha Kitere Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Mhe. Bashe amewaelekeza viongozi wa kampuni hiyo kukutana na Taasisi ya Utafiti Wa Kilimo (TARI) Naliendele ili waweze kupata usaidizi wa karibu katika shughuli zao

Aidha Waziri Bashe ameipongeza kampuni hiyo kwa mikakati yao madhubuti na kuwaahidi ushirikiano katika shughuli zao za uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini.






No comments:

Post a Comment