Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, akitoa maelezo kwa Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Idara ya Majanga BoT, Bi. Dorosela Blasius na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akifurahia jambo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala na Afisa wa Benki Bi. Rukia Muhaji katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba.


Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande, akielezea namna ya kutambua Alama za Usalama za noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.



No comments:
Post a Comment