Matokeo chanyA+ online




Wednesday, December 20, 2023


Miradi ya maji inayoendelea katika Wilaya ya Ludewa nchini Tanzania

Serikali inatekeleza jumla ya miradi saba ya maji. Gharama ya miradi yote ni Tsh. 13,866,290,252.86.

Maeneo Yanayofaidika na Miradi hii ni kata za Mavanga, Ludewa, Iwela, na Manda. Vyanzo vya maji ni Mavanga
Ukaguzi umefanyika kwenye ujenzi wa ofisi za vyombo vya usimamizi wa watumia maji ngazi ya jamii (CBWSO). Vituo vya ugawaji wa maji kwenye jamii vimekaguliwa.

Kwa mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilipokea Tsh. 2,108,673,191 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji. Miradi ni pamoja na ujenzi na uboreshaji wa mfumo wa Maji Ludewa Mjini, madope, Madindo, Ibumi, Lifua, na Ihela.

Hii inaonyesha jitihada za Serikali katika Wilaya ya Ludewa kutekeleza miradi ya maji ili kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo katika eneo hilo.

 Lengo la mradi  huu ni kuhakikisha kuwa Wana-Ludewa wanapata huduma ya Maji bora, safi, salama na yenye kutosheleza.

Na Haya Ndiyo Matokeo Chanya+

No comments:

Post a Comment