Wadau mbalimbali wakifuatilia Kongamano la kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir amesisitiza umuhimu wa Sera Bora ya Mambo ya Nje inayozingatia maoni ya wadau. Haya yamejiri katika Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, lililofanyika mjini Zanzibar. Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kushirikisha wananchi katika mchakato huo. Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. January Makamba, ameeleza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ni muhimu kwa ushawishi wa Tanzania duniani na marekebisho yanazingatia mabadiliko ya kimataifa. Kongamano limehudhuriwa na viongozi mbalimbali na linajumuisha maoni ya wadau wa ndani na nje ya serikali. |
No comments:
Post a Comment