TPA NA EACOP WAFIKIA MAKUBALIANO KUIMARISHA BANDARI YA TANGA KWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia mikataba mitatu na East African Crude Oil Pipeline ( EACOP) Limited kwa ajili ya kuridhia kutumika kwa Bandari ya Tanga katika kutekeleza mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania.
Mikataba hiyo mitatu inahusisha kukodisha eneo la kujenga miundombinu ya kuhifadhi mafuta, kutumia eneo la maji katika Bandari ya Tanga na mkataba wa kufanya shughuli za Bandari ambapo TPA imetoa sehemu ya gati mita 200 kwa Mkandarasi wa mradi Kampuni ya BBN Ltd kwa ajili ya kuegesha vyombo vinavyotumika kupokea na kupeleka vifaa na mahitaji mbalimbali ya ujenzi wa Gati Maalum (Jetty) la kupokelea mafuta ghafi.
Mikataba hii ni ya muhimu katika utekelezaji wa mradi wa EACOP hususani katika sekta ya usafirishaji majini kwa kuzingatia kuwa TPA kwa mujibu wa Sheria imepewa jukumu la kusimamia maeneo yote ya fukwe na mwambao kwa ajili ya shughuli za kibandari.
Sherehe hizo zimefanyika katika Kata ya Sojo iliyopo Jimbo la Bukene, Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora na kuhudhuriwa na Wananchi na Viongozi wa Nchi za Tanzania na Uganda.
#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+
No comments:
Post a Comment