Matokeo chanyA+ online




Monday, April 29, 2024

Mapitio ya Utekelezaji na Mwenendo wa Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024


A. MUUNDO NA MAJUKUMU YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA 1. Mheshimiwa Spika,muundo na majukumu ya Wizara yameainishwa katika ibara ya 17 na 18ya Kitabu cha Hotuba yangu. B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 2. Mheshimiwa Spika, masuala yaliyozingatiwa na maeneo ya kipaumbele katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 yameainishwa katika ibara ya 19 na 20 ya Hotuba yangu. C. MWENENDO WA BAJETI NA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 Makusanyo ya Maduhuli 3. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara pamoja na Taasisi za Wizara ilipanga kukusanya maduhuli yenye jumla ya Shilingi 12,676,201,000 (bilioni 12.68). Hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya Shilingi 7,515,601,174 (bilioni 7.5) zimekusanywa sawa na asilimia 59.29 ya lengo la makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2023/2024 ambayo ni sawa ya asilimia 71.15 ya lengo la kipindi cha miezi kumi.
Bajeti Iliyoidhinishwa 4. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara iliidhinishiwa na Bunge jumla ya Shilingi 383,619,511,000 (bilioni 383.62) kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 97,815,618,000 (bilioni 97.82) ni kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Shilingi 176,148,324,000 (bilioni 176.15) ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi 109,655,569,000 (bilioni 109.66) ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya fedha za maendeleo Shilingi 44,112,800,000 (bilioni 44.11) ni fedha za ndani na Shilingi 65,542,769,000 (bilioni 65.54) ni fedha za nje.

No comments:

Post a Comment