Matokeo chanyA+ online




Saturday, June 15, 2024

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KUFANIKISHA UJENZI BARABARA YA BUGENE-KASULO-KUMUNAZI 

Wakazi wa Kijiji Cha Nyakahanga wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja.

 

Wameipongeza Wizara ya Ujenzi Kupitia Wakala ya Barabara Tanzania -TANROADS kwa kuwajengea barabara inayounganisha wilaya ya karagwe na Ngara kupitia hifadhi ya Burigi Chato ya Bugene-Kasulo- Kumunazi (Km 128.5), kipande cha Bugene-Burigi Chato (Km 60).

Mradi huo unatekelezwa kwa miezi 30 na Mkandarasi wa kampuni ya China Road and Bridge Cooperation ya China (CRBC) kwa gharama ya TSh. Bilioni 92.84 ambapo hadi hivi sasa mradi umefikia asilimia 41.9

 

Regina Berra, Ni Mkazi wa Kijiji Cha Nyakahanga Wilayani Karagwe, ameeleza kuwa awali barabara hiyo ilikuwa katika hali mbaya na kupelekea adha hasa kwa watumiaji wa vyombo vya moto, lakini Kutokana na matengenezo yaliyofanyika chini ya Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS barabara hiyo Sasa imeanza kupitika vizuri na wanategemea itakamilika kwa kiwango Cha lami.

 

"Barabara hii ilikuwa na Hali mbaya,Sasa hivi kwakweli tunaona mabadiliko mazuri na kwa sisi tunao tembea tunajisikia vizuri, kama Mungu akitusaidia barabara hii ikakamilika kama ilivyopangwa kuwekwa lami kwakweli tutatembea vizuri" Amesema Regina

 

Naye Thabit Hamis, Mkazi wa Kijiji hicho amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi huo wa Ujenzi wa Barabara kwani kipindi Cha mvua ilikuwa ni vigumu watu na magari Kupita hali iliyosababisha kupoteza muda mwingi wakiwa barabarani.

 

"Zamani tulikuwa tunatembea kwa masaa manne lakini baada ya mkandarasi kuanza tu mradi huu, sasa tunatembea kwa masaa mawili na hapo bado haijakamilika na kuwekwa lami" Amesema Thabit

Hii inatoa picha nzuri ya juhudi za Serikali katika kuendeleza miundombinu ya barabara na madaraja, na inaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, katika kesi hii kampuni ya CRBC, kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania.


#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

No comments:

Post a Comment