Matokeo chanyA+ online




Sunday, June 16, 2024

 Rais Samia Asherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika Pamoja na Wajukuu

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu wake katika Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Juni.

 

Katika maadhimisho haya, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia, na jamii kwa ujumla kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema. Ameeleza kuwa usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi peke yake.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa jamii kuwapatia watoto elimu bora na kuwafundisha historia ya nchi yao ili kuwahimiza kuwa wazalendo tangu wakiwa wadogo. Alisisitiza kuwa elimu na historia ni nyenzo muhimu katika kujenga kizazi chenye mapenzi ya dhati kwa nchi yao.

 

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni kumbukumbu ya mauaji ya watoto wa Soweto, Afrika Kusini, mwaka 1976, walipokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi na kudai haki ya kupata elimu bora. Hivyo, ni siku muhimu ya kutafakari na kuchukua hatua za kuboresha maisha ya watoto wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.


#SISI NI TANZANIA

 

No comments:

Post a Comment