Air Tanzania Company Limited (ATCL) imefanikiwa kupata idhini rasmi kutoka kwa mamlaka za usafiri wa anga za China kuanzisha huduma za usafirishaji wa mizigo kati ya Jiji la Dar es Salaam na Guangzhou, China. Hatua hii ni mafanikio makubwa kwa shirika la ndege la taifa, linaloendelea kupanua huduma zake kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, ndege ya mizigo inayotumika katika huduma hii ina uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo. Ndege hiyo pia ina uwezo wa kuruka kwa muda wa saa 10 bila kujaza mafuta, hivyo kuifanya iwe chaguo bora kwa safari za masafa marefu kama Dar es Salaam hadi Guangzhou.
Safari ya kwanza ya usafirishaji wa mizigo kuelekea China inatarajiwa kufanyika ndani ya wiki chache zijazo. Huduma hii inalenga kurahisisha biashara kati ya Tanzania na China kwa kuongeza kasi na ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa. Hatua hii pia inatarajiwa kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuwawezesha wafanyabiashara wa ndani kufikia masoko mapana nchini China.
Air Tanzania inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya anga na biashara ili kuhakikisha mafanikio ya huduma hii mpya, ambayo itaimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na usafiri wa anga katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Tumshukuru Rais wetu dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundombinu ya viwanja vya ndege pamoja na kusaidia kupata wadau mbalimbali kutoka Nchi za nje ambao watasaidia kukuza nyanja za kibiashara,kiuchumi kwenye mataufa mbalimbali #samiasuluhuhassan #kaziiendelee
ReplyDelete