Matokeo chanyA+ online




Wednesday, December 4, 2024

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, Hatua Kubwa za Ujenzi Kuelekea Mapinduzi ya Usafiri wa Anga Tanzania

 

Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, unaojengwa katika Kata ya Msalato, Wilaya ya Dodoma Mjini, Jiji la Dodoma, unatekelezwa kwa awamu mbili na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 600 hadi kukamilika kwake. Ujenzi ulianza mwaka 2022, na awamu ya kwanza imegharimu shilingi bilioni 196. Mradi huu unajumuisha ujenzi wa majengo mbalimbali kama mnara wa kuongozea ndege (Control Tower), jengo la abiria (Terminal One), njia za kuruka na kutua ndege (Runways), na majengo mengine muhimu.

 

Kufikia Julai 12, 2024, ujenzi wa miundombinu ya njia ya kuruka na kutua ndege ulikuwa umefikia asilimia 67.6, huku ujenzi wa jengo la abiria ukiwa umefikia asilimia 32.21.  Hata hivyo, kufikia Agosti 30, 2024, maendeleo yaliongezeka ambapo ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege ulifikia asilimia 72, na jengo la abiria lilifikia asilimia 39. 

 

Mradi huu unafadhiliwa kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ambapo AfDB inachangia dola za Marekani milioni 329.47, na Serikali ya Tanzania inachangia shilingi bilioni 127, ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa mradi. 

 

Uwanja huu unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza. Aidha, utakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa aina ya Airbus na Dreamliner, hivyo kuboresha usafiri wa anga na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla. 

 

Serikali imepanga kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi ifikapo Desemba 2024, na inasisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. 

 


 

2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Moja kati ya viwanja bora zaidi nchini ni uwanja huu wa Ndege Msalato...Katika sekta ya uchukuzi hakika mama amefanya na anafanya makubwa sana sio tu viwanja vya ndege hata katika upande wa Reli na Bandari tunaona mapinduzi makubwa..#SisiNiTanzania #SSH #SisiNdioWajenziWaTaifaLetu #MSLAC #KatibaNaSheria #MatokeoChanya

    ReplyDelete