Matokeo chanyA+ online




Thursday, January 18, 2018

PARACHICHI YA NCHI YETU NI URITHI WA ULIMWENGU LINA SOKO KUBWA NCHI ZA ULAYA.

Soko kubwa na bei Nzuri ya Parachichi imeimarika Nchi za Ulaya  za  Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania na Uingereza Likitoa fulsa mpya ya Ustawi wa  zao hili kwa Watanzania, imebainika  kwamba Parachichi ya Tanzania imechukua chati ya Ubora katika Soko hilo.

Uchunguzi kitakwimu una baini Mwaka 2012, kiasi cha mauzo ya nje ya Parachichi yalikuwa kilo 488,492 tu, Miaka mitatu baadae Mwaka 2015 Tanzania ilisafirisha Kilo 2,579,976 Ikiwa ni ongezeko la 428.48%.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Africado ambayo ni  kampuni ya kwanza ya Tanzania inayosafirisha Parachichi nchini Uingereza ambako maduka makubwa vyakula ya Ocado, Sainsbury, Tesco na Waitrose, Parachichi ya Tanzania inatajwa kuwa Bora zaidi katika soko hilo la Ulaya.

Walaji wa Ulaya wamenogewa na Parachichi linalo zalishwa Mufindi na Kilolo likitajwa kupatikana msimu ambao Nchi zaidi ya Kumi zinazozalisha Tunda hili kuwa Nje ya Msimu wa Uvunaji wa Zao hili
Parachichi linazaliswa na Nchi zaidi ya 10 Duniani  zikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Colombia, Dominican Republic, Israel, Kenya, Mexico, Morocco, Peru, South Africa, Spain, Swaziland, Tanzania

Zao la Parachichi limeonyesha mwenendo mzuri wa bei na Soko kubwa Ulaya likiuzwa kwa hadi Sh za Kitanzania 7000 ama Paun 1.95 hii leo,fulsa hii inaangukia Tanzania

Kipindi cha mavuno cha sasa ni Juni hadi Agosti, Huku Tanzania pekee inaweza kuvuna na kusambaza kuanzia mwezi Machi hadi Oktoba

Sisi Kama Taifa ni Muda sasa wa kuacha mambo yasiyo ya Msingi na kujikita na Fulsa kubwa kama hii,Tumeona MatokeoChanyA+ katika Korosho na Sasa Taifa Turudi kujikita na kilimo na hasa kunapojitokeza fulsa mazao kama Parachichi, kwa sasa wanaonufaika zaidi na Soko hili Ni wageni walioshtukia mapema Fulsa hii.



Tuesday, January 16, 2018

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI,MAGEREZA,JWTZ


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y'all kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Jumla ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati magari yote 11

Akizungumza leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo mwishoni mwa mwezi huu.

 Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya  Dar Coach. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la Magereza yanayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd


RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI 6 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.JANUARI 16,2018.

Balozi Mteule Dkt.Sahabu Isah Gada aliyeteuliwa kuwa balozi wa Nigeria nchini,akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Dkt.Sahabu Isah Gada aliyeteuliwa kuwa balozi wa Nigeria nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Dkt.Sahabu Isah Gada wa Nigeria mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Nigeria nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mteule Krzysztof Buzalski aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Poland nchini, akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Krzysztof Buzalski wa Poland mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Poland nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Balozi Mteule Ali Davutoglu aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uturuki nchini akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Ali Davutoglu aliyeteuliwa kuwa balozi wa Uturuki nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Ali Davutoglu aliyeteuliwa kuwa balozi wa Uturuki nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Ali Davutoglu wa Uturuki mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Uturuki nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Balozi Mteule Frederic Clavier aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Ufaransa nchini akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Frederic Clavier aliyeteuliwa kuwa balozi waUfaransa nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Frederic Clavier wa Ufaransa mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Ufaransa nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Frederic Clavier wa Ufaransa mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Ufaransa nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mteule Noah Gal Gendler  aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Israel nchini akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe.Noah Gal Gendler aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Israel  nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Noah Gal Gendler wa Ufaransa mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi wa Israel nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mteule Alison Chartres  aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Australia nchini akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe.Alison Chartres   aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Australia  nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw.Robert Sirotka Mume wa Balozi Alison Chartres aliyeteuliwa kuwa balozi wa Australia nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Noah Gal Gendler wa Ufaransa mara baada ya kupokea hati ya utambulisho ya kuwa Balozi Alison Chartres wa Australia nchini.Januari 16,2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Sunday, January 14, 2018

YALIYOJIRI  JANUARI 14, 2018 KATIKA MAZUNGUMZO YA RAIS WA JMT, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI  NA RAIS WA RWANDA MH. PAUL KAGAME KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NCHINI TANZANIA.

#Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame amewasili majira ya saa 4 asubuhi tarehe 14/1/2018 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa JMT, Dkt. John Pombe Magufuli.

#Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame yuko Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda.

#Nimemuhakikishia kuwa Watanzania tutampa ushirikiano wa kutosha katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika - Rais Magufuli.

#Tumekubaliana kukuza biashara kati ya Rwanda na Tanzania kwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara - Rais Magufuli.

#Juhudi za kukuza biashara kati ya Rwanda na Tanzania zilishaanza, mwaka 2017 mizigo iliyofika katika Bandari ya Tanzania kutoka Rwanda ilifikia tani 950,000 - Rais Magufuli.

#Tumekubaliana na Rais Kagame kujenga reli ya kisasa kutoka Isaka, Tanzania hadi Kigali, Rwanda ili kuchochea maendeleo ya nchi hizi mbili - Rais Magufuli.

#Naomba Mawaziri wa Rwanda na Tanzania wanaohusika katika sekta ya miundombinu wakutane wiki hii ili kupanga juu ya ujenzi wa reli hiyo - Rais Magufuli.

#Tunataka ndani ya mwaka huu tuweke mawe ya msingi katika ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ili ujenzi huo uanze rasmi - Rais Magufuli.

#Napenda kumpongeza Rais Kagame kwa hatua anazozichukua katika kuiletea maendeleo nchi ya Rwanda - Rais Magufuli.

#Nampongeza Mkuu wa Majeshi wa nchini Rwanda kwa kushirikiana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kuimarisha usalama wa nchi zote mbili - Rais Magufuli.

#Wananchi wa Rwanda wanataka kufanya biashara na watanzania hivyo hii itapelekea kudumisha amani na umoja wetu na kuinua uchumi wa nchi zetu - Rais Kagame.

#Naahidi kuendelea kutembelea nchi ya Tanzania ili kupata ushauri kuhusu mambo mbalimbali yatakayotuletea maendeleo katika nchi zetu - Rais Kagame.

#Tatizo la ajira ni changamoto kwa Afrika nzima hivyo kila nchi inahitaji kukuza biashara na uwekezaji ili kuongeza upatikanaji wa ajira - Rais Kagame.

#Pia jukumu kubwa linabaki kwa vijana namna ambavyo wanaweza kutumia elimu na ujuzi walionao katika kujitafutia ajira - Rais Kagame.







                                    IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO.

Saturday, January 13, 2018

DOLA ElFU 83 ZAKAMTWA UWANJA WA NDEGE WA MWL NYERERE


Tarehe 13/01/2018 majira ya saa 15:30hrs Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la juu la kuondokea abiria Terminal II, maafisa wa Forodha wakishirikiana na Polisi JNIA na maofisa wa usalama walimkamata abiria aitwae Boniface s/o Aldo Mbilinyi, Mtanzania mwenye hati ya kusafiria nambari AB 757247, Kabila Mbena, umri miaka 32, kazi Biashara na Mkazi wa Tabata Segerea aliyekuwa akisafiri na ndege ya shirika la ndege la Emirate kuelekea Dubai akisafirisha Dola za kimarekani 123,000.
Abiria alitoa taarifa TRA (self declaration) ya dollar 40,000 tu ambayo ni pungufu ya (USD) 83,000.00 ambazo hakuzitolea taarifa. Abiria huyo alikuwa alielekea Dubai kwa safari ya kibiashara.Kiasi cha pesa ambazo hazikututolewa taarifa (USD 83,000.00) tume seize na ku deposit kwenye akaunti ya Dollar ya FIU number 20110028135.
Abiria (mtuhumiwa) anashikiliwa na jeshi la polisi (Termina One) kwa mahojiano zaidi




KILA MMOJA AFANYE KAZI KWA BIDII, KAZI NI  KIPIMO CHA UTU NA UZALENDO WETU