Matokeo chanyA+ online




Monday, December 17, 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AUNGANA WAUMINI WA DINI NYA KIISLAMU KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BAKWATA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Novemba 17, 2018. Wengine katika meza kuu ni pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma,  Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry shilingi milioni 30 taslimu wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Desemba 17, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Heshima Mzee Mohamed Songambele, mmoja wa wazee mashuhuri  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika  maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa Kiisalamu kinamama akishiriki katika dua  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam .Desemba 17, 2018. Kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa na Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma,  Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali wakishiriki katika dua  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam .Desemba 17, 2018



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.Desemba 17, 2018.

Friday, December 14, 2018

UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI

Maafisa wa Serikali kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, miundombinu na Mawasiliano, wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Bariadi hadi Maswa, (km50) wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Simiyu, ili kujua mafanikio, changamoto na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Jordan Matonya, akitaka kupata ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Bariadi hadi Maswa, mkoani Simiyu, yenye urefu wa km 50, kutoka kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara mkoani humo, Mhandisi Mohamedi Athumani (Hayuko pichani).


Na Benny Mwaipaja, WFM, Simiyu

UJENZI wa barabara yenye urefu wa kilometa 50 kati ya mji wa Bariadi na Maswa mkoani Simiyu kwa kiwango cha lami, inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 88, unaendelea kwa kasi ambapo hivi sasa umefikia asilimia 34.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mohamedi Athumani, ameiambia timu ya maafisa wa Serikali inayoongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwamba mradi huo utakapo kamilika mwezi Oktoba mwakani, utafungua fursa za kibiashara na kiuchumi kwenye mkoa huo na mikoa jirani ya Mwanza, Shinyanga, Singida na nchi jirani ya Kenya.

Amesema kuwa kazi zilizofanywa na mkandarasi anayejenga barabara hiyo, Kampuni ya CHICO ya China, ni kuanza kwa ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Simiyu na Banhya na uinuaji wa tuta la barabara maeneo mbalimbli ya mradi.

“Kuna madaraja mengine madogo madogo (Pipe culverts 57) pamoja na makalvati madogo (Box culverts 12), kwenye kipande hiki cha Barabara chenye urefu wa kilometa 50 na mkandarasi, Kampuni ya CHICO inafanyakazi vizuri na tuna imani kwamba ujenzi wa barabara hii utakamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2019 kama mkataba unavyoonesha” alifafanua Mhandisi Athumani.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri Mkazi wa mradi huo, Mhandisi Swalihi Kazuvi amesema kuwa barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi na Lamadi, inayojengwa kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 172, itakapokamilika, italeta chachu ya maendeleo yanayopitiwa na barabara hiyo.

“Kipande cha barabara ya lami kutoka Mwigumbi mpaka Maswa na kile cha Bariadi hadi Lamadi vimekamilika kwa hiyo kipande kilichobaki ni hiki (Bariadi-Maswa), ndio maana unaona magari yanayopita barabara hii ni mengi licha ya kwamba kipande hiki cha kilometa 50 hakijakamilika, madereva wanaona afadhali wapite huku kwenda Musoma kuliko kupitia njia ya Mwanza” aliongeza Mhandisi Swalihi Kazuvi

Lengo la ziara hiyo ya maafisa wa Serikali ni kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezawa katika Mkoa huo ili kujua mafanikio, changamoto na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.

RAIS MAGUFULI AFUTA MAELEKEZO YA WIZARA YA ELIMU

Rais Magufuli afuta maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu Bendera, Nembo na Wimbo wa Taifa.

Thursday, December 13, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA MIKOA PAAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.DESEMBA 13,2018



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kikao kilichowahusisha Wakuu wote wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Ikulu jijini Dar es Salaam.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kikao kilichowahusisha Wakuu wote wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa yote mara baada ya kikao chao pamoja na Makatibu Tawala kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa yote mara baada ya kikao chao pamoja na Makatibu Tawala kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa yote Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala mara baada ya Kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wednesday, December 12, 2018

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI PAMOJA NA WAZIRI MKUU WA MISRI DKT. MOSTAFA MADBOULY WASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA UJENZI WA MRADI WA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 2100 KATIKA MTO RUFIJI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.DESEMBA 12,2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Dkt. Tito Mwinuka wapili kutoka kulia akifatiwa na Mwanasheria wa Shirika hilo Isdori Nkindi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mazungumzo na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakipiga makofi wakati waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco wakionesha vitabu vya mikataba hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kabla ya tukio la la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakielekea kwenye Ukumbi wa Kikwete Hall kwa ajili ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally. Wengine katika picha mstari wa nyuma ni Mawaziri kutoka Tanzania na Misri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry mara baada ya hafla ya utiaji saini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.
Askofu Josephat Gwajima akisali kabla ya hafla hio kuanza

Sunday, December 2, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA ARUSHA.DISEMBA 2,2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200 kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200 kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha
Wananchi wa Arumeru wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika eneo la mkutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. 
PICHA NA IKULU