Matokeo chanyA+ online




Thursday, January 31, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

V25A9199
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Meneja Masoko na Utafiti Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndg. Itandula Kambalagi.
V25A9220
V25A9273
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9351
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulid Banyani (wa pili kulia) walipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BODI YA USHAURI NFRA YATEMBELEA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MKOANI MANYARA, YAMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI YA UJENZI

Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imetembelea eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara na kuipongeza kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kasi waliyoanza nayo ya ujenzi.

Kampuni hiyo ambayo imeanza ujenzi huo tarehe 15 Disemba 2018 katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara katika kipindi hicho imetekeleza mradi huo kwa kasi nzuri, Imesema Bodi hiyo.

Mradi huo katika Kanda ya Arusha (Babati), pamoja na Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda. utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na mkandari wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole alisema kuwa kampuni hiyo inapaswa kuongeza kasi zaidi ya ujenzi ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.


Alisema kuwa Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.



Pia, technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.


Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Eustance Kangole na katibu wake ambaye pia ni Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba imefanya ziara hiyo mara baada ya kikao kazi cha 33 cha Bodi hiyo Jijini Dodoma kilichofanyika kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya Wakala ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa mauzo ya mahindi Tani 36,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP) sambamba na kujadili maendeleo ya Mradi wa Vihenge na Maghala ya kisasa.

Vihenge 8 vinatarajiwa kujenzgwa Kanda ya Arusha katika eneo la (Babati) vyenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 25,000 ambapo pia yatajengwa maghala 2 yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 15,000 hivyo kuwa na jumla ya Tani 40,000.

Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa Tani 250,000 zaidi (vihenge vya kisasa 190,000 MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.

1R6A1184
Wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakikagua eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara unaojengwa na kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
1R6A1179

1R6A1190

1R6A1195


1R6A1198

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WATATU WAPYA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 31 Januari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka nchi 3 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi wa kwanza kukutana na Makamu wa Rais, alikuwa Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri hapa nchini ambaye alifika kwa lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchini  mbili ambao ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa Misri.

“Misri itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu, Afya na masuala ya teknolojia ya ujenzi wa miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema Balozi huyo.

Mwisho Balozi huyo mpya wa Misri aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali hizi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais alimpongeza na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri katika kazi zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano kati ya Misri na Tanzania umezidi kuimarika.

Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais alikuwa Mhe. Francisca Pedros, Balozi mpya wa Spain hapa nchini ambaye Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza mwanamke kuteuliwa kuja kuitumikia nchi yake hapa nchini.

Balozi wa Tatu kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya kuwa hapa na kuona namna mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo alisema kuwa

“nafarijika kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi hizi mbili”

Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alimpongeza Balozi huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake hapa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca (kushoto) aliyefika kujitambulisha ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wednesday, January 30, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI, BALOZI WA SWEDEN JIJINI DODOMA

V25A8961
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A8993
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9015
V25A9019
pika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA DSFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
Uteuzi wa Dkt. Sweke umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Livestock Research Institute - TAFIRI) – Kigoma.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
Uteuzi wa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania - GST).
Uteuzi wa Prof. Ikingura umeanza tarehe 18 Januari, 2019.

WAKENYA WAJA NCHINI TANZANIA KUJIFUNZA KUHUSU MIRADI MAJI TAKA

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). Ujumbe huo ulilenga kutembelea na kujionea miradi ya majitaka maeneo ya Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi maalum ya Maji Taka inayotekelezwa katika maeneo yasiyopimwa na yenye msongamano. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya majisafi na majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.  
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi (kulia) kiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutokea upande wa Maji na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundu vya jami wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Moja ya Choo cha kisasa vinavyojenga na Shirika la CCI kwa kusaidiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi.
Moja ya chemba za vyoo vya kisasa.
Muonekano wa Choo cha zamani ambacho wakazi wa Vingunguti walivyokuwa wakitumia.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam akionyesha namna mabomba ya vyoo yalivyopita.
Wageni wakiendelea na ziara.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Rahimu Seif Gassi (kulia) kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti.
Bi Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililopo nchini Kenya akizungumza machache juu ya jinsi walivyoweza kufika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Afisa Miradi wa Akiba Mahirani Trust ya nchini Kenya, Patriki Njoroge akieleza machache mbele ya wakazi wa Vinguti jijini Dar es Salaam wakati walipofika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Makazi wa Vingunguti akisoma risara mbele ya wageni.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA)  Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya mradi wa kuchakata maji Taka uliopo Toangoma wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) (mwenye shati jeupe) akiwaonyesha chemba ya mradi wa kuchataka Maji Taka iliopo Toangoma jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye (Kulia) akiendelea kutoa maelezo.
Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.