Matokeo chanyA+ online




Monday, March 4, 2019

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Ndg Goerg Joseph Kazi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi, anayeshuhulikia Masuala ua Uvuvi na Mifugo Dr.Omar Ali Amir.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dkt. Ali Mohamed Shein,akisaini Hati ya Kiapo ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar anayeshughulikia Masuala ya Mifugo na Uvuvi Dr.Omar Ali Amir.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Ndg Seif Shaban Mwinyi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba, Maji na Nishati. Ndg. Salhina Ameir Mwita, hafla hiyi imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi.Mansura Misi Kassim, hafla hiyo imefanyika Ikulu leo Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Mawaziri aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Makatibu Wakuu na Manaibu aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar.   
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)

Sunday, March 3, 2019

KIKAO KAZI CHA WAZIRI KANGI LUGOLA NA WATENDAJI WAKE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akipitia maandalizi ya bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, kikao kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (wa pili kushoto), akimpitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kwenye maandalizi ya bajeti ya Jeshi hilo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Kulia kwa Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akifafanua jambo kwa watendaji wakuu wa Wizara yake wakati akipitishwa katika maandalizi ya bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa idara zilizo chini ya Wizara anayoiongoza. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akitoa ufafanuzi kwa watendaji wa idara zilizo chini ya Wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Magereza, Uhamiaji na NIDA (hawako pichani), ikiwa ni maandalizi ya bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akitoa ufafanua kwa watendaji wa idara zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Magereza, Uhamiaji na NIDA (hawako pichani), ikiwa ni maandalizi ya bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana.

Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Polisi wakisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu walipowasili kwenye kikao kazi cha maandalizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana. (Picha zote na Veronica Mwaffisi-MOHA)


Friday, March 1, 2019

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KAHAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1, Machi 2019 ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akiwa Wilayani Kahama Makamu wa Rais alitembelea mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya Ziwa Victoria kwennda katika miji ya Kagongwa na Isaka wenye gharama ya shilingi bilioni 24.72 zikiwa fedha za ndani.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isagehe ambapo pamejengwa matanki mawili ya maji ambayo yana uwezo wa kubeba lita laki 8 kila moja, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu ya tano inawajali na kuwathamini wananchi wake na kuwahakikishia wananchi hao maji yatafika kote yalipoahidiwa”

Makamu wa Rais pia alitembea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi na kutaka kufahamu mgodi huo umejiandaaje kuyaacha mazingira salama mara baada ya kufungwa.
 
Kwa upande wake Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amesema sheria mpya ya madini itasaidia sana katika kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwani pamoja na kodi itakayolipwa pia wachimbaji wanajukumu la kuchangia huduma za kijamii kwenye maendeo yanayozunguka mgodi.

Aidha, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa 8 ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 121 ikiwa ni miradi ya TEA na P4R katika shule ya Sekondari Nyashimbi wilayani Kahama.

Mwisho Makamu wa Rais alihutubia wananchi wa Kahama katika uwanja wa michezo wa Taifa ambapo alihimiza wananchi hao kushirikiana na Serikali katika masaula ya maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi.

Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka   

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kata ya Isagehe mara baada ya kukagua  matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72.  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen. 

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI IKULU ZANZIBAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas D.Ndumbaro, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha, Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe.Dkt. Damas D.Ndumbaro, wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar leo,1/3/2019.(Picha na Ikulu)   

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo eneo la maegesho ya ndege linaweza kuegesha ndege 19 za darala C, na 11 daraja E na jengo linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa muda ambao abiria ni wengi.

Mhandisi Mfugale amemhakikishia Mhe,. Majaliwa kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa, na kwamba jengo hilo litakabidhiwa kwa serikali tarehe 31 Mei, 2019.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale akisoma taarifa ya  Ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
  Kiongozi Mkuu wa Timu ya Wataalam wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Julius Ndyamukama (aliyenyoosha mkono) akimuonesha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ukumbi wa abiria wanaoondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia aina ya viti vya abiria vitakavyotumika kwenye Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) alipotembelea leo. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Bi. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wa pili kushoto ni Mhandisi Julius Ndyamukama, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.

Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 

 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere TerminalThree, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAAA

UTAFITI WA MUHAS WAONYESHA CHANJO DHIDI YA VVU NI SALAMA

Profesa wa Mikrobiolojia na Immunolojia MUHAS, Eligius Lyamuya akiwasilisha matokeo ya utafiti wa Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) iliyofanyiwa majaribio katika maeneo mbali mbali ya nchini Tanzania na Msumbiji wakati wa kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrea Barnabas Pembe akitoa neno la ufunguzi wakati wa kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Kisali Pallangyo akiendesha muhadhara wakati wa kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililokuwa na lengo la kuwasilisha matokeo ya utafiti wa Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Profesa wa Mikrobiolojia na Immunolojia wa Chuo cha Afya St. Joseph, Fred Mhalu akichangia mada wakati wa kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililofanyika jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Prof. Said Aboud na Dkt Edith Tarimo.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi akitoa ufafanuzi wa jambo.
Kamishna Msaidizi wa Polisi na Maganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ACP Dkt Charles Msenga akitoa mchango wake katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililokuwa na lengo la kuwasilisha matokeo ya utafiti wa Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akifunga kongamano la Kisanyansi la Kitafiti lililofanyika jijini Dar es Salaam lililokuwa na lengo la kuwasilisha matokeo ya utafiti wa Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Kamishna msaidizi wa Polisi na Maganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ACP Dkt Charles Msenga (kulia) akiteta jambo na Dkt Patricia Munseri wa MUHAS.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) inayofanyiwa majaribio nchini Tanzania ni salama na ina uwezo wa kuufanya mwili kutengeneza viashiria vya kinga.
Hata hivyo hiyo haimaanishi chanjo hiyo ni kinga dhidi ya Maambukizi ya Virusi (VVU) hivyo, matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), yamebainisha.
Akiwasilisha matokeo hayo, Profesa wa Mikrobiolojia na Immunolojia MUHAS, Eligius Lyamuya, amesema chanjo hiyo iliyofanyiwa majaribio imetengenezwa nchini Sweden na wataalam wenzao ambao wanashirikiana nao katika masuala ya tafiti.
"Tumeifanyia utafiti chanjo hii tuliangalia iwapo ni salama na iwapo ina uwezo wa kuchangamsha ile kinga ya mwili kutengeneza viashiria vya kinga na iwapo ina uwezo wa kutengeneza chembe chembe hai za mwili.
"Au uwezo wa kutengeneza molecular mbalimbali ambazo zinaashiria hii inaweza kuwa zinahusika katika kinga dhidi ya chanjo ambayo imetolewa.
" Hivyo, tumebaini chanjo hii ni salama na wote waliochanjwa hakuna ambaye amepata madhara yoyote hadi sasa wako vizuri," alisema.
Aliongeza "Jambo la pili ni kwamba tuna ushahidi kulingana na tafiti yetu chanjo hii inachangamsha ile kinga ya mwili kutengeneza viashiria vya kinga.
"Lakini hivi viashiria vya kinga vinavyotengenezwa haina maana kwamba ndiyo kinga yenyewe dhidi ya maambukizi ya VVU, hapana hivi ni viashiria tu vitahitaji kitu kingine zaidi kuona kama vina uwezo wa kupigana na vile virusi au la!," alisema.
Amesema katika kutengeneza chanjo hiyo wataalam wenzao wa Sweden waliangalia pia iwapo itafaa kutumika katika mazingira yetu au la!
"Tulikubaliana lazima ifae katika mazingira yetu kwa maana kwamba itakapotengenezwa huko siku zijazo kuwe na uwezekano wa kukinga dhidi ya virusi vya ukimwi ambavyo vipo katika mazingira yetu maana kuna aina nyingi ya virusi," amesema.
Amesema matokeo hayo yana maana kubwa kwamba bado wanaweza kuendeleza tafiti hizo kwa kushirikisha wahusika (sampuli) wengi zaidi.
"Katika hatua ya kwanza tulihusisha watu, wahusika walikuwa 60, lakini walioweza kupata chanjo zote tatu walikuwa 56 na walioweza kupata chanjo zote tatu na nyingine mbili za ziada walikuwa 42.
"Hii ina maana kuna ambao waliachia kwa sababu zao binafsi lakini kwa sababu ushiriki ni wa hiari hatuwezi kuuliza mtu kwa nini hakushiriki kupata chanjo mwanzo hadi mwisho," alisema.
Akizungumza, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi amesema matokeo ya utafiti huo yameonesha wazi namna MUHAS ilivyofanya kazi kubwa kuunga mkono jitihada za kidunia katika kutafuta chanjo dhidi ya ukimwi.
"Wizara tunaunga mkono juhudi hizi kwa sababu dunia inamaanisha tunaweza kufikia hatua ya kupata chanjo itakayofanya kazi vizuri, iliyo salama na kwa bei nafuu ambayo itasaidia mno katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi," alisema.
Ameongeza "Kimsingi, yamefanyika majaribio mengi, kizuri katika yote haya chanjo zimeonekana ni salama na zina uwezo wa kufanya mwili kutengeneza vichocheo vya kinga.
"Sasa chuo kitajikita kutafiti iwapo itakuwa na uwezo wa kukinga watu kutopata maambukizi ya ukimwi," amesisitiza Profesa Kambi.