Matokeo chanyA+ online




Friday, February 14, 2020

NAIBU WAZIRI WA UVUVI NA MIFUGO ULEGA AFUNGUA SHAMBA LA MAFUNZO NA UFUGAJI WA SAMAKI 'BIG FISH FARM' JIJINI DAR

 Naibu Waziri wa  Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdallah Ulega akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Shamba la mafunzo na ufugaji wa Samaki (Big Fish Farm) lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Shamba hilo linatumika kwa uzalishaji na kufundishia jinsi ya kilimo cha ufugaji wa samaki aina ya Kambale na Sato. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. balozi Jeroen Verheul akizungumza katika ufunguzi wa  shamba la mafunzo na ufugaji wa Samaki (Big Fish Farm) lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wadau waliojitokeza katika ufunfuzi wa shamba la mafunzo na ufugaji wa Samaki (Big Farm Fish) lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Big Fish Farm Bw. Abraham Mdeme ambaye ni mmiliki wa kampuni ya ufugaji wa samaki na mbegu za samaki (Kamale, Sato) akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Shamba hilo na eneo la uzalishaji na kufundishia jinsi ya kilimo cha ufugaji wa samaki.
Wadau waliojitokeza katika ufunfuzi wa shamba la mafunzo na ufugaji wa Samaki (Big Fish Farm) lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. balozi Jeroen Verheul (pili toka kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdallah Ulega (anayefuatia kulia) katika ufunguzi wa shamba la Mafunzo na uzalishaji wa samaki.
Naibu waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdallah Ulega (aliyenyoosha mkono) akiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. balozi Jeroen Verheul katika ufunguzi wa  shamba la mafunzo na ufugaji wa Samaki lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdallah Ulega akipata picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ufunguzi wa Shamba la mafunzo na Ufugaji wa Samaki lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wadau wakifurahia.
Kibao cha ufunguzi.
Mkurugenzi wa Big Fish Farm Bw. Abraham Mdeme (kwanza kulia) ambaye ni mmiliki wa kampuni ya ufugaji wa samaki na mbegu za samaki (Kamale, Sato) akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Uvuvi na Mifugo  Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. balozi Jeroen Verheul (kwanza kushoto) mara baada ya ufunguzi wa shamba la mafunzo na ufugaji samaki lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Uvuvi na Mifugo  Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. balozi Jeroen Verheul (kushoto) wakitembelea shamba la mafunzo na ufugaji wa Kilimo cha Samaki (Big Fish Farm) lililopo jijini Dar es Salsa.
Mabwawa ya kisasa yanayotumika kufugia.
Mitambo ya kisasa ya kukuzia samaki, Michuzi blog

Thursday, February 13, 2020

"TANZANIA NI SALAMA HAKUNA UGONJWA WA CORONA" - DKT NDUGULILE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile

Na Englibert Kayombo, WAMJW, Arusha

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi bado iko salama na hakuna mgonwjwa yeyote mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Dkt Ndugulile ametoa kauli hiyo akiwa Jijini arusha katika Ziara zake za kikazi ambapo waandishi wa habari walimuuliza juu ya tetesi za uwepo wa ugonjwa huo nchini, pamoja na kutaka kufahamu ukweli wa taarifa za mtu anayedai kuwa na dawa za ugonjwa huo.
“Niseme tuu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi bado tuko salama na hakuna mgonjwa yeyoteambaye ameripotiwa na amethibitika kuwa na ugonjwa” amesema Dkt Ndugulile.
Amesema kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa hawana ugonjwa.
“Sambamba na hilo tumeendelea kuchukua tahadhari mbalimbali na mimi niko katika Mkoa huu wa Arusha na nitaenda Kilimanjaro kwenda kuangalia utayari” amesmea Dkt. Ndugulile na kuendelea kusema “ Nimepita hapa leo nimeongea na uongozi na nimeridhika na maandalizi ambayo tunayo hapa katika Mkoa huu wa Arusha katika kudhibiti ugonjwa huo” Ameeleza Dkt. Ndugulile
Akijibu kuhusu mtu ambaye anasema kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo ambaye anajulikana kwa jina la Mosses Mollel maarufu kwa jina la “Nabii namba saba” aliyetoa taarifa za kuwa na dawa yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona, Dkt Ndugulile amesema kuwa anazo taarifa za mtu huyo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akijitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake.
“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu  anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu  atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile
Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo  hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka  Tiba ya ugonjwa huo.
Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa virusi vya corona na kuweka mawasiliano yake  kwenye mitandao .
Dkt. Ndugulile amesema kuwa mtu yeyote anayetoa tiba asili na mbadala kwanza ni lazima asajiliwe na mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Afya, pili lazima dawa zake ziwe zimesajiliwa na Wizara ya Afya na kusisitiza kuwa nabii huyo pia anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini.
“Tuepuke kutoa kauli ambazo zinakwenda kuchanganya jamii, na endapo tutabaini mtu huyu hana sifa ambazo anasema kuwa nazo tutamchukulia hatua za kisheria” Amesema Dkt. Ndugulile.

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 43 YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Keki  Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam akimvisha skafu Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam leo Febuari 13,2020 kwenye maadhimisho ya miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Keki  Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimlisha Keki  Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mama Kate kamba Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanachama wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam  Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanachama wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam  Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanachama wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam  Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza  aliyekuwa katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es salaam Catherin Semuhando baada ya kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picha ya pamoja

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi  wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wasanii mbalimbali waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika leo Febuari 13,2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Wednesday, February 12, 2020

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA USALAMA NA MAADILI PAMOJA NA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Usalama na Maadili kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam. Februari 12, 2020.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam. Februari 12, 2020.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Usalama na Maadili kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam. Februari 12, 2020.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI WILAYA YA KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM, PAMOJA NA MAJENGO YA MKUU WA WILAYA NA HALMASHAURI YAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na na viongozi wengine akikata utepe kuzindua jengo la Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya kulifungua rasmi  Jumanne Februari 11, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana  na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Sarah Msafiri na viongozi wengine baada ya kuzindua jengo la Mkuu wa Wil
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kufungua rasmi majengo ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuizindua rasmi Wilaya hiyo  Jumanne Februari 11, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Faustine Ndugulile wakiwea saini vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Sarah Msafiri na viongozi wengine baada ya kulifungua rasmi jengo la ofisi hizo  Jumanne Februari 11, 2020. Waliosimama ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Ng’ulwabuzu Ludigija.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kuzindua rasmi jengo la Mkuu wa Wilaya hiyo   Jumanne Februari 11, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Ng’ulwabuzu Ludigija akimpa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kulifungua rasmi Jumanne Februari 11, 2020.

PICHA NA IKULU

Tuesday, February 11, 2020

WAZIRI WA KILIMO MHE JAPHET HASUNGA AWASILI JIJINI ROMA, ITALIA KUMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA 43 WA IFAD

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino Jijini Roma, Nchini Italia kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa IFAD. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino Jijini Roma, Nchini Italia kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa IFAD

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 10 Februari 2020 amewasili Jijini Roma nchini Italia na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino.

Mhe Hasunga amezuru nchini Italia ambapo atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

Mkutano huo ambao hufanyika mwezi Februari ya kila mwaka na huongozwa na Rais wa IFAD na kuhudhuriwa na Magavana wan chi wanachama ambao ni Mawaziri wenye dhamana ya Kilimo.

Mkutano huo wa Magavana wa IFAD ndio chombo kikuu chenye maamuzi ya ngazi ya juu (High Level Decision Making Body) kuhusiana na shughuli zote za IFAD kwa kipindi cha mwaka mzima, Hivyo Waziri wa Kilimo wa Tanzania ni Gavana wa Tanzania ambaye pia ana dhamana ya kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo muhimu.

Kauli mbiu ya Mkutano wa 43 wa Magavana wa IFAD ni “Kuwekeza katika Mifumo Endelevuya Chakula kwa ajili ya kusitisha njaa ifikapo mwaka 2030 – Investing in sustainable food systems to end hunger by 2030”.

Majadiliano ya mkutano huo utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Februari 2020 yamelenga kuhakikisha ni kwa jinsi gani IFAD itaweza kutumia uzoefu wake katika masuala ya chakula na lishe ili kuweza kufikia lengo la pili la Maendeleo endelevu ya Dunia la kutokuwa na njaa kabisa (SDG 2 – Zero hunger).

IFAD ni Shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo, ambalo ni shirika la Umoja wa mataifa kwa ajili ya maendeleo vijijini lilioanzishwa tarehe 13 Desemba 1977 kwa  lengo kufanya ukue uzalishaji wa kilimo na  vyakula haki kufikia kwa ngazi ya maisha ya kujitosheleza.

Kwa namna hiyo unafadhili wa mipango ya kimaendeleo na ambayo ni muhimu kwa masikini zaidi kati ya masikini duniani na ambao wanaishi katika vijijini pembezoni kabisa mwa miji. Ni 70% ya watu duniani mara nyingi wamesahuliwa na wenye kuhitaji msaada mkubwa.


Thursday, February 6, 2020

UZINDUZI WA KITABU CHA KUVUTIA WATALII ‘A TASTE OF TANZANIA”


Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi umeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoitwa “A Taste of Tanzania” kilichosheheni picha zinazoonesha vivutio vya utalii pamoja na utamaduni wa Mtanzania. Uzinduzi wa Kitabu hicho chenye kurasa 343 ulifanyika wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii uliofanyika The Hague, Uholanzi tarehe 30 Januari 2020.

Maeneo ya utalii yanayooneshwa kwa kina ndani ya Kitabu hicho ni pamoja na; Mji wa kimataifa wa Arusha; Mlima Kilimanjaro; Hifadhi za Taifa za Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Tarangire na Ruaha; Mlima Ol Donyo Lengai na Ziwa Natron. Maeneo mengine ni Olduvai Gorge; umaarufu wa Ziwa Eyasi na Bonde la Ufa; Utalii wa mkoa wa Iringa; aina mbalimbali za mapishi pamoja na viungo vyenye ladha nzuri vinavyoleta upekee katika mapishi hayo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe ya Uzinduzi wa Kitabu na Maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju aliwashukuru waandaji wa Kitabu hicho kwa uwasilishaji sahihi kuhusu Tanzania, hali itakayowezesha watalii kuongezeka zaidi nchini, Balozi Kasyanju alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa Waholanzi na Jumuiya ya Kimataifa kuja kuwekeza Tanzania kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika katika miundombinu na taratibu za uwekezaji.

“A Taste of Tanzania” ni kitabu kilichoandaliwa na mwandishi Bw. Stephen Walckiers kwa kushirikiana na mpiga picha maarufu, Bw. Wim Demessemaekers, wote wakazi wa Uholanzi waliowahi pia kuishi Tanzania. Uzinduzi rasmi wa kitabu hicho kinachopatikana kwenye mitandao na maduka ya vitabu nchini unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania tarehe 05 Februari 2020.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.




Baadhi ya picha zilizotumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika kitabu cha "A Taste of Tanzania." 


Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiteta jambo na mpiga picha aliyeshiriki katika maandalizi ya uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho, Bw. Wim Demessemaekers.

Mhe. Balozi kasanju akipokea ufafanuzi wa tafsiri za picha mbalimbali kutoka kwa Bw. Wim

Balozi wa Yemen nchini Uholanzi, Mhe. Sahar Ghanem akimsalimia na kumpongeza Bw. Wim kwa umahiri wake wa kupiga picha. Mhe. Ghanem alielezea nia yake ya dhati ya kutembelea Tanzania.

Sehemu ya Wanadiplomasia, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wadau wengine walioshiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa Kitabu na ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii wa Tanzania.

Baadhi ya vyakula vya kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa kitabu na ufunguzi wa maonesho.

Wednesday, February 5, 2020

NMB KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Benki ya NMB imesema itahakikisha inaendelea na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano ili kuifikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi .

Kauli hiyo ilitolewa Mkuu wa idara ya huduma za Serikali wa benki ya NMB, Vicky Bishubo wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa ya benki hiyo kwenye mkutano wa utoaji taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) uliofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)- Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya wizara hiyo  Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa NMB - Vicky Bishubo mara baada ya kuwasilishwa mwisho wa wiki,  Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe. Mwita Waitara.


“Benki ya NMB ni mali ya wananchi na Serikali hivyo tunafurahi tunapoona kila upande unaendelea kuiunga mkono katika mafanikio yaliyopatikana hivyo tunawaomba mwendelee kutuunga mkono kwa kufungua akaunti na kuweka fedha kwetu”alisema.

Bishubo alisema Benki ya NMB itahakikisha inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ili kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema benki hiyo inaendelea kufungua matawi na kuweka mashine za ATM katika maneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za kibenki karibu na maaneo yao.

Alibainisha kuwa uwepo wa benki hiyo katika kila Wilaya hapa nchini imesaidia pia kurahisisha maendeleo ya wananchi kwa kupata huduma za kifedha karibu kwenye maeneo yao. Aliongeza pia benki hiyo imeweka mawakala wengi hapa nchini kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma za kifedha katika maeneo yao.

Aidha alisema benki hiyo imekuwa ni sehemu ya mafanikio ya Ofisi ya Tamisemi kutokana na kufanyakazi kwa karibu na Halmashauri zote hapa Nchini.

Kwa upande Waziri Selemani Jafo alitaja baadhi ya mafanikio ya Ofisi hiyo kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya 97 zimejengwa na vingine kukarabatiwa na Serikali katika kipindi hicho cha miaka minne ya mafanikio

Jafo alitaja mafanikio mengine kwenye sekta ya elimu kuwa ni ongezeko la ufaulu wa wanafunzi, ujenzi wa vyumba vya madarasa na ukarabati wa majengo ya shule kongwe hapa nchini.

Hata hivyo aliwashukuru benki ya nmb kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa misaada mbalimbali kwenye sekta ya afya na elimu hapa nchini. #NMBKaribuYako

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) - Mhe. Selemani Jafo akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki ya NMB - Vicky Bishubo walipokutana katika mkutano wa utoaji taarifa ya mafanikio ya  TAMISEMI .