Matokeo chanyA+ online




Friday, July 3, 2020

WAZIRI BASHUNGWA: TANZANIA KUINGIA UCHUMI WA KATI ITAVUTA WAWEKEZAJI WENGI

Bidhaa zinazotokana na zao la Mkonge ambazo zinauzwa katika banda la Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) lililoko katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi


Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO

Serikali imewataka Wananchi kuendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwani chanzo cha nchi kufikia uchumi wa kati ni pamoja na wananchi wake kupendelea bidhaa ambazo wanazizalisha wao kama wao, na mafanikio yametokana na juhudi za watanzania wote wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayofanyika  katika Uiwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa ili watanzania waweza kusheherekea mafanikio endelevu ya kuingia nchi zenye kipato cha kati wanatakiwa kuwa wa kwanza kutangaza bidhaa zao.


Waziri wa Viwanda na Biashara,  Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa  kutoka kwa wajasiriamali wanaofadhiliwa na Benki ya Biashara Tanzania (NBC), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi


"Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya ya nchi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye kipato cha kati yawe ni matunda kwa watanzania hasa kwa wakina mama na  vijana wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania". Alisema Mhe.Bashungwa.



Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa  kutoka kwa wajasiriamali wanaofadhiliwa na Benki ya Biashara Tanzania (NBC), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi

alisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuangalia bidhaa za ndani Kabla hawajanunua bidhaa kutoka nje ili kuweza kukuza viwanda na kuwa na uchumi wenye kipato cha kati endelevu kwani ili Watanzania waendelea kusheherekea mafanikio haya ya kufikia kipato cha kati tunatakiwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa  kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya Umeme cha AfriCAB alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.

Alibainisha kuwa kupitia maonesho 44 ya Biashara kimataifa (sabasaba)  ambapo takribani  kampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi zitashiriki, kutakuwa na fursa ya wananchi kuja kununua bidhaa na kuangalia teknolojia mbalimbali zikioneshwa na taasisi na makampuni ya kitanzania,  pia kupitia B2B wale ambao wapo nje wataendelea kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wanashiriki katika maonesho ya sabasaba hayo.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA),alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi

Pamoja na hayo Bashungwa amesema Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati inasaidia kuingia kwenye rada ya kimataifa hivyo wengi watapenda kuja kuwekeza hapa nchini.



Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa  kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya Umeme cha AfriCAB alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.


Thursday, July 2, 2020

WAZIRI NDALICHAKO ATIMIZA AHADI ATOA VYEREHANI 10 VETA MPANDA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametimiza ahadi ya kutoa vyerehani 10 kwa wanafunzi waliohitimu​ mafunzo ya ushonaji kutoka Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi​ Mpanda​ wanaotoka katika mazingira magumu.
​
Akizungumza katika halfa hiyo Mkoani Katavi, Profesa Ndalichako amesema ahadi hiyo aliitoa​ mwaka 2018 baada ya kuwakuta vijana wadogo wamemaliza masomo ya darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari​ na kujiunga na mafunzo ya ushonaji katika chuo hicho kupitia msaada wa kanisa





SIRI 10 ZA TANZANIA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Benki ya Dunia imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 50 duniani za uchumi wa kipato cha kati, ikiwa ni ya pili baada ya Kenya katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, baada ya ukuaji wa uchumi unaosukuma pato la mwananchi kukua (Per capita GNI) mwaka 2020.

Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati  miaka mitano kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, jambo ambalo ni la kujivunia.


Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 katika ukurasa wa pili, kipengele 1.2 “Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na kuwa na nchi ambayo umaskini unapungua, uchumi imara unaojengwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo”.

Dkt. Abbasi alisisitiza kuwa uchumi wa kipato cha kati umegawanyika katika madaraja mawili daraja la chini ambapo ni kuanzia dola za Kimarekani 1036 hadi 4045 na daraja la juu ni  dola 4046 hadi 12,535 na mwaka huu Tanzania imepanda daraja kuwa uchumi wa kipato cha kati daraja la chini, pamoja na nchi za Algeria na Benin.

Aidha, Dkt. Abbasi alifafanua siri 10 zilizoisaidia Tanzania kutajwa kufikia daraja la uchumi wa kipato cha kati na  Benki ya Dunia hapo Julai 1, 2020 kuwa ni nchi yenye amani na utulivu, na hivyo ni msingi muhimu nyuma ya mafanikio  ya nchi ya Tanzania  kuingia katika uchumi wa kipato cha kati kwani  bila amani hakuna kufanyakazi, hakuna kuzalisha na hakuna kuongeza kipato. Na hivyo viongozi, wanahabari  na wananchi kwa ujumla  wamesisitizwa  kuwekeza akili zao katika kuimarisha amani iliyopo na kukataa chokochoko zozote zile zinazoweza kuharibu misingi ya maendeleo.

Siri ya  pili ni mipango thabiti ya maendeleo, ambapo Dkt. Abbasi alisema kuwa moja ya kanuni muhimu ya kuendelea ni kuwa na mipango inayokuwekea malengo makubwa  (Olympic targets). Serikali itaendelea kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo ya muda mrefu na mfupi, akitolea mfano mwaka 2020 Serikali ilianza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ambayo moja ya malengo ni kufikia uchumi wa kati.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi siri ya tatu ni utekelezaji usioyumba, katika miaka 59 ya Uhuru na mitano ya Awamu ya Tano Serikali imejitahidi kusimamia eneo hilo kwa  kuhakikisha mipango inayowekwa inatekelezwa kwa kina (3feet implementation).

Siri nyingine ni maamuzi magumu, “Moja ya mafanikio ya Serikali ya Tanzania kwa Awamu zote na sasa tumeimarisha katika Awamu ya Tano ni wakati fulani Serikali kufanya uamuzi mgumu ambao wakati fulani ulionekana kuwa ni ndoto lakini baadaye ukaleta mafanikio makubwa kwa jamii, tumepambana na wala rushwa na wahujumu uchumi, tumewekeza katika miundombinu mikubwa, tumekataa pia baadhi ya nadharia za kimagharibi kwenye utendaji wetu na utungaji wetu wa sera za maendeleo” alisema Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi alitaja siri nyingine kuwa ni azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi, kutekeleza miiko ya uongozi, kuwekeza kwenye miradi inayochechemsha uchumi, maendeleo ya vitu na sekta binafsi yenye tija.


 

 

 

 

 

 
 

MAKAMU WA RAIS SAMIA AENDELEA NA ZIARA YA KICHAMA MKOA WA MAGHARIBI UNGUJA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi Unguja  alipowasili katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo  Zanzibar  leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Zanzibar  leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi Unguja.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Magharibi Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Unguja leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi  Unguja.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Magharibi Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Unguja leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi  Unguja.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Zanzibar  leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi Unguja.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Magharibi Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Unguja leo Julai 02,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa Magharibi  Unguja.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI LUKUVI AWASHUKIA VIONGOZI WANAOPORA ARDHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi jana. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na wa tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekerwa na tabia ya baadhi ya viongozi kuhusika kupora ardhi ya wananchi na kueleza kuwa muarobaini wa viongozi hao umefika kufuatia watendaji wa sekta ya ardhi kuhamishiwa Wizarani sambamba na kuanzishwa ofisi za ardhi katika mikao.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema hayo wakati wa kuzindua ofisi ya ardhi mkoa Katavi wilayani Mpanda jana ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipeana mkono na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Michael Nzyungu ikiwa ni ishara ya kupongezana baada ya Waziri wa Ardhi kumkabidhi gari lenye thamani ya shilingi milioni 150 na vifaa vingine vya upimaji kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi katika sekta ya ardhi nchini.


Alisema, wapo baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa ambao ni sehemu ya migogoro ya ardhi na wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kupora na kuuza ardhi za wananchi tabia aliyoieleza kuwa inamkera rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa Lukuvi, uanzishwaji ofisi za ardhi za mikoa pamoja na uhamishaji watendaji wa sekta ya ardhi kutoka TAMISEMI kuja Wizarani unatoa nguvu kwa watumishi wa sekta ya ardhi kutumia na  kusimamia sheria na kuonya viongozi kutojihusisha na kupora ardhi za wananchi na kubainisha kuwa ardhi itapangwa na kusimajiwa kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Naibu wake Dkt Angeline Mabuka wakiongozwa kuelekea kutoa gari na vifaa vya upimaji kwa ajili ya urahisaji utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Katavi jana baada ya kuzindua ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi jana, Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera


‘’ Kuna viongozi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kupora ardhi za wananchi, safari hii hakuna fursa maana watendaji wote wa sekta ya ardhi wako chini ya Wizara ya ardhi, madiwani hawawezi tena kuwaazimia  kuwafukuza.’’ alisema Lukuvi

Akizungumzia suala la upimaji ardhi katika mkoa wa Katavi, Lukuvi aliagiza hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2020 vijiji vyote katika mkoa huo viwe vimepimwa na kupatiwa hati za kijiji sambamba na wamiliki 15,000 waliokwama kupewa hati kutokana na urasimu kupatiwa hati zao na kuweka wazi kuwa, hivi sasa hakuna visingizio kwa kuwa vifaa kwa ajili ya upimaji vipo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Naibu wake Dkt Angeline Mabuka wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mpima wa Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Katavi Eliya Mjina wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi.

Agizo la Lukuvi linafuatia kuelezwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Katavi Siyabumi Mwaipopo kuwa kati ya vijiji 172 vilivyopo kwenye mkoa wa Katavi ni vijiji vitatu tu ndivyo vilivyopimwa na kupatiwa hati za vijiji.

‘’Mwaka huu uwe wa mwisho kwa migogoro ya ardhi nchini kwani nyenzo zote zipo ikiwemo wataalamu pamoja na vifaa vifaa vya upimaji na nawataka viongozi wa wilaya na mkoa wasiwe sehemu ya migogoro’’ alisema Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Msajili Msaidizi wa Hati Liz Kibada wakati akikagua majalada ya ardhi katika ofisi ya Msajili wa hati jana katika uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi mbalimbali waliokwenda kushuhudia uzinduzi wa ofisi za ardhi mkoa wa Katavi jana.
Baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya pamoja na wananchi wengine wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisisitizia suala la ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi ambapo alisema ni muhimu wamiliki wa ardhi wakaepuka kuwa na malimbikizo ya kodi ya ardhi kwa kutii sheria ya kulipa kodi mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera mbali na kushukuru uamuzi wa kuanzisha ofisi ya ardhi katika mkoa wake, aliwataka wananchi wa Katavi kuitumia fursa ya kuwa na ofisi ya ardhi ya mkoa kupima ardhi na kumilikishwa na kusisitiza kuwa mkoa wake utaandaa opresheni maalum ya kupima ardhi katika mkoa mzima. 

Baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya pamoja na wananchi wengine wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi jana. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)


Na Munir Shemweta, WANMM KATAVI

Uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi uliambatana na makabidhiano ya vifaa mbalimbali ambapo Waziri Lukuvi alikabidhi gari lenye thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na vifaa vya upimaji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye halmashauri hiyo.

Wednesday, July 1, 2020

NAIBU WAZIRI KANYASU APONGEZA HOTELI YA SERENA KUFUNGULIWA BAADA YA JANGA LA CORONA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amepongeza uamuzi wa Hoteli ya Serena wa kufungua hoteli hiyo tangu ilipofungwa kwa ajili ya kuweza  kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona.

Amezitoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam wakati akishiriki hafla ya kufungua hoteli ya Serena ambayo imekuwa ni muhimu katika kuwahudumia Watalii wengi wanaotoka na kuingia kutoka  Nchi za nje kabla na baada ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.


Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hoteli ya Serena iliyopo Jijini Dar es Salaam  baada ya janga la Corona kufuatia kufungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa huo, Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa  Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Godwin Mollel na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Wadau wengine wa Utalii.

Amesema uamuzi huo wakufungua hoteli hiyo  unatoa ujumbe mzito Duniani     kuwa Tanzania ipo salama na ipo tayari kwa ajili ya kuwapokea Watalii.

Amesema kurudi kwa biashara hiyo kunarudisha uhakika wa maisha ya watu takribani 450,000 ambao wameajiriwa moja kwa moja katika sekta ya Utalii.


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto  Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt.Godwin Mollel pamoja na wadau wengine wa Utalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kufungua Hoteli ya Serena iliyokuwa imefungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya ugonjwa wa Corona

Amesema Ugonjwa wa Corona uliiathiri jamii katika nyanja za  kiuchumi na kijamii baada ya watu wengi kupoteza ajira zao na wengine kuachishwa kazi kutokana na janga hilo

Amesema uamuzi huo wa Hoteli ya Serena kuifungua hoteli hiyo kunaleta mwanga wa matumaini kwa Watanzania wanaoitegemea Sekta ya Utalii katika kuendesha maisha yao.



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona

" Ninawashukuru Hoteli ya Serena kwa kupeleka ujumbe kwa Wawekezaji wetu wote ambao wanaogopa na kufunga biashara zao kwa ajili ya Ugonjwa huo.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya  Corona na kuwa ugonjwa huo bado upo lakini hauwezi kukimbiwa ni  lazima tujifunze kuishi nao.



Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona

" Tunamshukuru sana Rais, Mhe.John Pombe Magufuli kwa kufanya maamuzi ya  kufungua anga ambapo tunaamini biashara ya Utalii na biashara ya anga zinategemeana kwa kiasi kikubwa.

Amesema uamuzi huo umeifanya biashara ya utalii kuweza kurejea kwa vile tayari mashirika ya ndege ya Ethiopia, Emirates, KLM na Quatar yameanza kuja nchini.



Naibu Waziri wa  Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto,  Dkt. Goldwin Mollel  akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona

Naye, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto,  Dkt. Goldwin Mollel amewataka Wadau wa Sekta ya Utalii ikiwemo Wamiliki wa Hoteli kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Wizara yake ili kuhakikisha usalama wa Wageni na wenyeji wanaowahudumia Watalii

Akizungumzia uamuzi huo wa kuifungua hoteli hiyo amesema  inatuma ujumbe kwa Wawekezaji wengine kuwa Tanzania ipo salama kwa i na Watanzani wapo tayari kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta shughuli za kibiashra.



Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema tangu anga lilipofunguliwa kumeonesha dalili njema ya ujio wa idadi kubwa  ya watalii

" Kuna matumaini makubwa ya kupata watalii  wengi zaidi kwa mfano siku ya jana ndege ya Shirika la  KLM ilitua Uwanjaa  wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) ikiwa na kabiria 200 kati ya hao 45 ni watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kutalii" alisema Jaji Mstaafu Mihayo.

Amesema hiyo ni dalili njema  katika sekta ya Utalii nchini, " Miezi mitatu iliyopita tulikuwa hatupokei watalii kabisa kwa hofu ya janga la Corona.

DKT. MPANGO ARIDHISHWA NA UJENZI WA OFISI YA MKUU WA WILAYA BUHIGWE

Taswira ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma inavyoonekana kwa sasa.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kigoma na Wilaya ya Buhigwe  kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe inayojengwa katika eneo la Bwega, Tarafa ya Manyovu, wilayani Buhigwe mkoani Kigoma na kuagiza Jengo hilo likamilike kabla ya mwezi wa kumi ili wananchi wa wilaya hiyo waanze kupata huduma kwenye jengo hilo jipya.

Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo jipya la Ofisi ya MKuu wa Wilaya mpya ya Buhigwe ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 1.1

 

.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina, akimuongoza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kukagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, alipotembelea na kukagua ujenzi wa  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Mkoa wa Kigoma



“Nakupongeza Mkuu wa Wilaya na timu yako yote kwa usimamizi mzuri wa Fedha za Serikali, lazima tujenge Makao Makuu ya Wilaya ambayo yataishi kwa miaka mingi, kwa hiyo nimefurahi jengo ninavyoliona hata kama sio Mhandisi lakini ninaona lina ubora”. alisisitiza Dkt. Mpango.

Alimtaka Mkuu wa Wilaya kuendelea kusimamia rasilimali fedha  zinazotolewa na Serikali kama alivyofanya kwenye mradi wa ujenzi wa  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa ilingane na thamani ya fedha zilizotolewa.


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina, akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea na kukagua ujenzi wa  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mkoa wa Kigoma.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Bw. Masawika Kachenje, akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na wapili kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina, alipotembelea ujenzi wa mradi wa ofisi hiyo. Mkoani Kigoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipokea taarifa ya mradi ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Buhigwe mkoani Kigoma, kutoka kwa  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Rashid Mchata, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo Serikali inatoa fedha kuigharamia, alipokuwa ziarani mkoani humo.


Kwa upande wake, Meneja mradi huo Masawika Kachenje, akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amesema kuwa hadi sasa kiasi cha shilingi milioni mia tano (500,000,000) ambazo Serikali zilitoa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo  kimetumika kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi.

Aliongeza kuwa kiasi cha shilingi milioni (550,000,000), kimebaki ili kukamilisha kiasi cha sh. Bilioni 1.1 ikiwa ni gharama ya utekelezaji wa mradi wa  ujenzi  jengo zima, ambapo mipango ya Wilaya ilikuwa kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Julai tarehe 15 mwaka 2020.


Fundi Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhandisi Solomon Tile, akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Bw. Kanali Michael Ngayalina.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Buhigwe na mafundi wanaojenga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo baada ya kukagua jengo hilo mkoani Kigoma.


Na: Josephine Majura na Peter Haule KIGOMA


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali, Michaeli Ngayalina, amemshukuru Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa Fedha za Serikali na kuahidi kuzisimamia vizuri fedha zote zinazotolewa na Serikali kukamilisha miradi ya maendeleo.

Kanali Ngayalina, amemuomba Dkt. Mpango kusaidia upatikanaji wa Fedha zilizobaki ili waweze kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kama ilivyopangwa kwenye ratiba.


MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA YA KICHAMA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Kaskazini Unguja  alipowasili katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja  iliopo Mahonda  leo Julai 01,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kaskazini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini  iliopo Mahonda Unguja  leo Julai 01,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kaskazini Unguja. kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Idi Ali Ame

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini iliopo Mahonda leo Julai 01,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kaskazini Unguja.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)