Matokeo chanyA+ online




Monday, July 6, 2020

KATIBU MKUU BALOZI BRIGEDIA JENERALI IBUGE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ametembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Wizara Balozi Ibuge amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi zaidi ili kuyaona matunda ya nchi kuwa katika kundi la uchumi wa kati.

''Sasa nchi yetu imeingia katika uchumi wa kati ambao unamaanisha kila mtu aendelee kupiga juhudi zaidi ya pale alivyokuwa anafanya ili tuendelee kupaa kuliko hivi ambavyo tumefikia sasa'' amesema Balozi Ibuge.

Amesema Tanzania sasa ina Balozi 43 na Balozi ndogo tatu na ni mwenyeji wa Balozi 63 na Mashirika ya Kimataifa 30 ikiwa ni namna ya kuipeleka Tanzania katika anga za kimataifa tukionyesha mafanikio vivutio vyetu na vitu vingine vyote tunavyovifanya ili kujiletea maendeleo huku tukiimarisha mahusiano ya kimataifa.

Akiwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Balozi Ibuge ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na makampuni matatu ya Kigeni yanayoshiriki maonesho hayo.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiangalia jarida linaloelezea utekelezaji wa dipolomasia ya uchumi linalochapishwa na Wizara alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, katika picha ya pamoja na watumishi walioko kwenye banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akijadili jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu walipotembelea moja ya banda kwenye maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu wakimsikiliza mfanyabiashara kutoka Siria anayeshiriki maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

      



MTANDAO WA MAJI RUANGWA WAMTUA ‘WAMTUA NDOO MAMA KICHWANI’

 

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya mijini na vijijini kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002.

Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inaelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao, hatua inayolenga kuwaondelea changamoto mbalimbali ikiwemo maskini na magonjwa yanayosababishwa na maji.



Wizara ya Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini kwa kujenga, kupanua na kukarabati miradi ya maji, lengo ikiwa ni kufikia asilimia 85 ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020.

Miradi ya Maji Vijijini inatekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na sekta binafsi ambapo katika kuwapunguzia wananchi gharama, Serikali kwa kushirikiana na wadau inaandaa mifumo itakayofaa kusimamia na kuendesha miradi ya maji ikiwa ni pamoja na kuviimarisha Vyombo vya Watumiaji Maji.

Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi inatekeleza miradi mbalimbali ya maji katika vijiji mbalimbali vya Wilaya hiyo hatua inayolenga katika kutoa huduma endelevu kwa wakazi waishio mijini na pembezoni mwa miji.

Wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama kutoka katika vyanzo vya Visima vifupi, Visima vya kati, Visima virefu ambavyo vimefungwa pampu za mikono, miradi ya maji bomba ya maporomoko na miradi ya maji ya kusukumwa na mitambo.


Tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka 38.5% mwaka 2015 hadi kufikia 51.20% kufikia mwezi Novemba, 2018 ikiwa ni ongezeko la 12.7% ambapo jumla watu 64,498 waishio vijijini wanapata huduma ya maji.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Maji wa Naunambe-Mpekenyera unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kushirikiana na Kamati za Vijiji vya Naunambe na Mpekenyera katika kuhakikisha kuwa Serikali inamtua mama ndoo kichwani na kumuondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.

Kufuatia juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Wilaya ya Ruangwa mradi huo ulikamilika mwezi Juni, 2018 na jumla wananchi 7,000 wameanza kupata maji na salama na kiasi Tsh. Milioni 828 zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kusafisha maji na miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa maji kutoka katika vyanzo na kuwafikia wananchi.

Akizungumza na Timu ya Maafisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) waliofanya ziara Wilayani humo, hivi karibuni, Katibu wa Mradi huo, Selemani Nyamiri anasema mradi huo ulianza kuibuliwa na wananchi mwaka 2010 kwa kaya mbalimbali katika vijiji hivyo kuchangishana fedha kwa ajili ya kuhakikisha mradi huo unatoa huduma endelevu ya maji katika vijiji hivyo vyenye wakazi zaidi ya 10,000.

‘Maji yaliyokuwa yakizalishwa katika chanzo cha Mpekenyeara yalikuwa yana chumvi sana, pia yalipatikana katika vyanzo visivyo safi na salama hivyo ilitulazimu kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya kutumia mafundi na utaalamu wa ziada ili kuhakikisha kuwa maji yanarejea katika ubora wake’’

Nyamiri anasema kwa sasa kiwango cha chumvi katika maji hayo kimepungua na kufanya maji hayo kuwa na ubora wa matumizi kwa binadamu, ambapo watumiaji wanalazimika kuchangia gharama ya Tsh. 200 kwa kila ndoo, ikiwa ni fedha zinazokusanywa na kamati hiyo kwa ajili ya kufanya matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya mradi.

Akifafanua zaidi anasema wananchi wa vijiji hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za maendeleo ya jamii ikiwemo huduma ya maji ambapo wananchi wamekuwa na mwamko wa kusimamia uhifadhi wa maeneo ya vyanzo vya maji ili kufanya vijiji vyote vinapata maji ya uhakika.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Naunambe Bi. Amina Abdalla aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa umeondoa kero kwa akina mama wa vijiji hivyo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

Bi. Rehema Mussa Mkazi wa Kijiji cha Mpekenyera alisema kwa kipindi cha nyuma hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika vijiji hivyo haikuwa ya kuridhisha, hususani wakati wa kipindi cha kiangazi na kuwalazimu wananchi wengi kutembea umbali wa kilometa 3 kufuata huduma ya maji katika vyanzo visivyo rasmi huku wakitembea na watoto migongoni.

‘Utekelezaji wa mradi huu ni mkombozi mkubwa sana kwetu wananchi wa Naunambe na Mpekenyera kwani kwa sasa shida ya maji imeisha, tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Mbunge wetu wa Ruangwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa’’ alisema Rehema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Andrea Chezue alisema hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo umefikia asilimia 55  huku kukisaliwa na maeneo machache ambayo yanakosa huduma ya maji ambapo Ofisi yake imekuwa ikiendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma ya maji inafikia walau asilimia 70 ifikapo mwishoni mwaka 2020.

‘Halmashauri ya Ruangwa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji katika vijiji mbalimbali ikiwemo mradi wa maji wa Naunambe-Mpekenyera wananchi wanapata maji na wanafurahia huduma inayotolewa kwa mwaka 2019 pekee tulipata miradi minne ikiwemo mradi wa maji Kitandi na tayari tumeanza kufanya mawasiliano na Halmashauri ya Mtama kuhakikisha kuwa maji yanafikishwa katika vijiji jirani ikiwemo vijiji vya Nangumbu A na B’’ alisema Chezue.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Kata ya Mandawa Rashid Mshamu anasema mradi wa maji mandawa unahuhudumia jumla ya vijiji 5 vya Nahanga, Chikundi, Mandawa Chini, Mchichili na Mtondo unaogharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 1.7 zilizotolewa na Serikali, ambapo mradi huo unawanufaisha jumla ya watu 13,756.

Anaongeza kuwa mradi huo ulioasisiwa mwaka 1975 ulikuwa na miundombinu  chakavu na kusababisha kero kubwa kwa wananchi hususani wazee, wanawake na watoto ambapo walikuwa wanahangaika, ambapo Serikali iliamua kuufua mradi huo katika bajeti ya mwaka 2014/15.

Anasema kuwa kwa sasa mradi huo unaendelea vyema na huduma ya maji ni ya uhakika na wananchi wa vijiji hivyo wanalazimika kuchangia kiasi cha Tsh. 50 inayopelekwa katika mfuko wa maji wa kijiji hicho na kutumika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya mradi.

Miradi mingine ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ni pamoja na mradi wa maji Nanganga, mradi wa maji Likunja, mradi wa maji Namahema, mradi wa maji Chenjele, ambapo katika maeneo yote hali ya upatikanaji wa maji ni ya kurithisha.

Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mibure, Namakuku na Namahema ambao tayari umekamilika na jumla ya watu 6,133 wananufaika, ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 631,593,444.50 zimetumika.

Serikali imewekeza katika miradi ya maji mikubwa na midogo ili kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ambapo uwekezaji huo umeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini na maisha ya wananchi kwa ujumla.

Ili kuleta matokeo tarajiwa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji hapa nchini unahusisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi na pia wadau wa maendeleo kutokana na ukweli kuwa Serikali imeweka lengo la kufakisha huduma ya maji kwa asilimia 85 kwa upande wa wananchi.

 

Sunday, July 5, 2020

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWACHUJA WAGOMBEA, MAGUFULI AMWAGIWA SIFA

 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uimarishaji wa Maadili na Usaidizi Katika Utumishi wa Umma na wa Binafsi (WoLaOTa) Samwel Olesaitabau akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo iliyofanyika mkoani hapa jana.
Waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo. 



Na Dotto Mwaibale, Singida

Viongozi wa vyama vya kisiasa wametakiwa kuhakikisha wote wanaoomba nafasi ya uongozi wanachujwa ipasavyo ili kusaidia kupunguza viongozi wala rushwa nchini.

Ombi hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uimarishaji wa Maadili na Usaidizi Katika Utumishi wa Umma na wa Binafsi (WoLaOTa) Samwel Olesaitabau wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo iliyofanyika mkoani hapa jana.

Katika hatua nyingine Olesaitabau amewaomba viongozi wa dini kote nchini kutenga muda katika ibada zao hata kwa dakika tano kuiombea Nchi na Uchaguzi Mkuu wa 2020 hata kwa wale wasio na dini rasmi wanaoabudu mawe au milima nao wafanye hivyo.

"Mwaka huu kuna uchaguzi na niwaombe sana viongozi wote wa vyama vya kisiasa kikiwemo chama Tawala cha CCM kuhakikisha wote wanaoomba uongozi wamechujwa ipasavyo na wasiwe na huruma na wakifanya hivyo basi kwa vyovyote vile tutapunguza viongozi wala rushwa Serikalini" alisema Olesaitabau.

Akizungumzia kusudi la kuanzisha taasisi hiyo alisema ni kusaidia uongozi wa nchi yetu kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kama aalivyoonesha Rais John Magufuli. 

Aidha Olesaitabau alisema dira ya taasisi hiyo ya kipekee hapa nchini ni utoaji wa elimu ya kuimarisha maadili kwa waajiri, na watumishi wa sekta za umma na binafsi Tanzania Bara ili watumie Ueledi na Taaluma zao kwa kuleta matokeo chanya.

Olesaitabau akizungumzia baadhi ya sifa kati ya 35 alizoziona za utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli alisema ni kiongozi ambaye ana uwezo wa kuamua jambo na kulisimamia kuanzia mwanzo hadi mwisho na kuwa hayumbishwi na kelele  ama za ndani ya nchi au hata nje kwa jambo ambalo amelianzisha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alitaja sifa nyingine kuwa anaichukia rushwa na anapenda kila mtu afanye kazi ya kujipatia kipato kwa jasho lake mwenyewe bila ya kumdhulumu mwingine na kuwa ana uwezo wa kuweka kumbukumbu/ takwimu kiusahihi katika kichwa chake kwa muda mrefu bila ya kusahau.

WAZIRI LUKUVI ATAKA WAMILIKI WA ARDHI WENYE HATI ZA MIAKA 33 KUZIHUISHA OFISI ZA ARDHI ZA MIKOA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizundua ofisi ya ardhi mkoa wa Mara jana. Kushoto kwa Waziri Lukuvi ni Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima na kushoto ni Bi Sophia Lugera mmoja wa wananchi wa kwanza kupatiwa hati kwenye ofisi hiyo.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wamiliki wa ardhi ambao hati zao za ardhi zinaishia miaka 33 kwenda ofisi za ardhi za mikoa zilizoanzishwa hivi karibuni kuzihuisha ili kupatiwa za miaka 99.

Lukuvi ametoa kauli hiyo jana mkoani Mara wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Mara ambayo ni ofisi ya kumi na mbili kuzinduliwa ikiwa ni mfululizo wa kuzindua ofisi za ardhi kwenye mikoa mbalimbali nchini.



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika Masijala ya ardhi ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Mara wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima.


Alisema, kuna baadhi ya wamiliki wa ardhi kwenye mikoa mbalimbali ambao viwanja vyao vimepimwa na michoro kuidhinishwa lakini hati zao ni za miaka 33 na wamiliki hao watakapoenda kuzichukua wanatakiwa kuziangalia ili zibadilishwe na kupatiwa hati za miaka 99.

‘’ Hati nyingi za wale wamiliki ambao hawajazichukua zimekwisha muda wake, muende kwenye ofisi za ardhi za mikoa, huko mtaelekezwa na Wasajili Wasaidzi wa ardhi katika ofisi hizo namna ya kuzibadilisha ili mpatiwe za miaka 99’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, zaidi ya wamiliki wa ardhi 50,000 kwenye mkoa Mara hawajachukua hati za ardhi wengi muda wa hati zao unaishia miaka 33 na kutaka kufika ofisi za ardhi mkoa wa Mara kurekebishiwa na kupatiwa za miaka 99 ili iwe rahisi kupata mikopo mikubwa .

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza huku akiwa amezungukwa na wananchi wa mkoa wa Mara walimfuata kutaka kutatuliwa kero zao za ardhi wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Mara jana.


Akizungumzia uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Mara, Lukuvi alisema mkoa huo umekuwa na migogoro mingi ya ardhi na kubainisha kuwa uzinduzi wa ofisi hiyo utawawezesha wananchi wa Mara kumaliza migogoro kupitia ofisi hiyo badala ya kuipeleka migogoro kwake.

Waziri Lukuvi aliongeza kuwa, pamoja na Wizara yake hapo awali kushughulikia kero na migogoro ya ardhi lakini tatizo la kimfumo lilikuwa kubwa na kuweka wazi kuwa uzinduzi wa ofisi za mikoa unakomesha kero ambapo sasa hakutakiwa na gharama yoyote kwa mmiliki wa ardhi zaidi ya ile atakayolipia wakati wa kuomba hati.

‘’Mgogoro wa kimfumo ulikuwa mkubwa zaidi na leo hii tumekomesha kero na hakuna gharama yoyote mmiliki wa ardhi ataingia kufuatilia hati zaidi ya ile aliyolipa wakati wa kuomba hati, serikali ya awamu ya tano imeondoa kero zote kwa wananchi kwenye utawala wa ardhi’’ alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara sehemu ya jengo la Huduma ya Mama na Mtoto alipokwenda kufuatilia maendeleo ya ujenzi huo jana wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Mara.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima alisema, ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko na kero nyingi na kati ya malalamiko kumi na mbili anayopokea kwa siku sita yanahusiana na ardhi na kusisitiza kuwa, mingi ya migogoro ya wananchi lazima nguvu hutumika jambo alilolieleza kuwa linaongeza gharama za kiafya katika masuala ya matibabu na kubainisha kuwa uwepo ofisi ya ardhi katika mkoa huo utarahisisha huduma katika sekta ya ardhi..

‘’ Kila malalamiko kumi na mbili ninayopata ofisini kwangu sita ni ya ardhi na mengi yana sura ya kijamii na hapa kuna neno la msamiati ukisikia vyesi ujue ni kesi’’ alisema Malima.

Mmoja wa wakazi wa Musoma aliyepatiwa hati katika uzinduzi ofisi ya ardhi Bi. Mara Sophia Lugera alifurahishwa na usogezwaji huduma za ardhi mkoani Mara na kubainisha kuwa aliifuatilia kwa muda mrefu hati yake iliyokuwa ofisi ya Kanda Mwanza na kusema, baada ya kuipata hati ataitumia kuchukulia mkopo benki ili aendeleze biashara yake ya ujasiriamali.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimpa mkono wa shukurani Padri Cleophas Sabure wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma kufuatia kutoa msaada ya Printer kwa ajili ya urahisishahi utendaji kazi wa ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Mara jana. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)



Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alitembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara inayojulikana kama Mawalimu Nyerere Memorial Hospital iliyopo eneo la Kwangwa Musoma mkoa wa Mara.

Akiwa katika mradi huo, Lukuvi aliagiza kukamilika kwa jengo ya Huduma ya Mama na Mtoto kufikia mwisho wa mwezi huu ili lianze kutumika kwa wananchi wa mkoa huo na Mikoa jirani.

Alisema, ujenzi wa jengo hilo umechukua muda mrefu na anataka kuona sehemu ya jengo hilo inakamilika kufikia julai 31 mwaka huu na Agosti mosi 2020 atamuagiza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kwenda kuona kama agizo lake limetekelezwa kama alivyoahidiwa.

Mhandisi na Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Hosiptarli ya Rufaa mkoa wa Mara Renald Kazyoba alisema, kimsingi sehemu ya ujenzi wa mradi huo sehemu ya Huduma ya Mama na Mtoto (Wing C) itakamilika kama alivyoagizwa kwa kuwa kazi kubwa imefanyika.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MZAZI WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Albetina Kasanga ambaye ni Mama Mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda wakati alipomtembelea Bibi huyo nyumbani kwake katika kijiji cha Kibaoni Mkoani Katavi, Julai 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA JENGO LA MPANDA PLAZA

Jengo la Mpanda Palaza ambalo ni kitegauchumi cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) limezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Mpanda, Julai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la Mpanda Plaza ambalo ni kitegauchumi cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC), mjini Mpanda, Julai 4, 2020. Wa pili kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homela na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulid Banyani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU MAJALIWA: BANDARI YA KAREMA IJENGWE USIKU NA MCHANA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili katika eneo la  Karema  wilayani Tanganyika kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Bandari, Julai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Karema wilayani Tanganyika, Julai 4, 2020. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group inayojenga Bandari ya Karema kwa gharama za zaidi ya sh. bilioni 47 ifanye kazi usiku na mchana na kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Congo.

Pia, Waziri Mkuu ametoa muda wa siku 21 kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Polisi, Wizara ya Madini na wawe wameanza kutoa huduma katika eneo la Ikola ili kuhudumia wageni wanaotoka Congo.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Julai 04, 2020) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Karema inayojengwa kwenye ziwa Tanganyika katika kata ya Karema wilayani Tanganyika, Katavi. Alisema mkandarasi anatakiwa ahakikishe mradi huo unakamilika haraka.

Waziri Mkuu alisema mradi huo unalenga kuongeza tija katika shughuli za kibandari kwenye ukanda wa Ziwa Tanganyika ndani na nje ya nchi na kwamba utaongeza fursa za kibiashara nchini na pia utakuwa chachu ya kukuza uchumi pamoja na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

“Tumeamua kujenga bandari hii ambayo itawezesha meli zaidi ya moja kupakia na kushusha abiria na mizigo kwa wakati mmoja. Hii ni Serikali ya kuahidi na kutekeleza na ni Serikali ya kusikia na kutenda na ndio maana halisi ya falsafa ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.”

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Dkt. Baraka Mdima alisema mradi huo unahusisha ujenzi wa gati kubwa la kufungia meli lenye urefu wa mita 150 pamoja na kingo ya kuzuia mawimbi makali, uchimbaji wa kuongeza kina cha lango la kuingilia bandarini na sehemu ya kugeuzia meli.

Alisema eneo jinguine ni ujenzi wa miundombinu ya bandari ikiwemo mgahawa, jengo la kupumzikia abiria, majengo ya ofisi, eneo la sakafu ngumu kwa ajili ya kuhifadhia makasha pamoja na miundombinu ya Zimamoto na Tehama. Mradi huo utazingatia ujumuishi wa Reli ya Kisasa (SGR).

“Mradi unajengwa kwa miezi 24 na kukamilika kwa bandari ya kisasa ya Karema, kutaboresha shughuli za kiuchumi katika mkoa wa Katavi na Tanzania kama kusafirisha watu na bidhaa katika maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na nchi jirani za Congo, Burundi na Zambia.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera aendelee na operesheni ya kuwasaka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.“Watu wote wanaomiliki silaha bila ya kuwa na vibali watafuwe popote walipo na wachukuliwe hatua za kisheria.”

Awali, Waziri Mkuu alizungumzia upatikanaji wa umeme katika wilaya ya Tanganyika, alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote nchini, hivyo waendelee kuwa na subira.

“Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme na amepunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka sh. 380,000 hadi sh. 27,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa licha ya gharama za kuunganishiwa umeme kupunguzwa, pia wananchi hatolazimika kulipia gharama za nguzo pamoja na gharama za fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari zimeshalipiwa na Serikali.

WANANCHI KATA YA PUMA MKOANI SINGIDA WATENGENEZA MADAWATI 71 YENYE THAMANI YA SH.3,408,000

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (kulia mwenye baraghashia)åakikabidhi jana moja ya dawati kati ya 71 kwa Wazazi wa Kata ya Puma yaliyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya kukaa chini kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma. 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa, akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (katikati) , akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa wamekaa kwenye  madawati hayo baada ya kukabidhiwa. 
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
 Viongozi wakiwa meza kuu kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule ya Msingi Puma, Joseph Helman akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mdimi akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Puma, Wenseslaus Masire  akizunguma kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu iliyosimamia kutengeneza madawati hayo, Clemence Mande,  akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Katibu wa Kamati ya hutengenezaji wa madawati hayo, Samsoni Masasi, akisoma taarifa.
 Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kutengeneza madawati hayo wakitambulishwa.
Mwalimu, Christina Lyimo,  akizungumzia msaada wa madawati hayo.

 Mkazi wa Puma, Magreth Agustino, akizungumzia msaada wa madawati hayo.
Mwanafunzi Mariam Abdallah akizungumzia msaada wa madawati hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

Wananchi wa Kata ya Puma wilayani Ikungi mkoani Singida kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamefanikiwa kutengeneza madawati 71 yenye thamani ya sh.3,408,000 kwa ajili ya kupunguza changamoto ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma ya kukaa chini.

Hatua ya kutengeneza madawati hayo  ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na kusoma katika mazingira bora.

Akizungumza jana wakati akipokea madawati hayo kutoka kwa kamati maalumu iliyosimamia hutengenezaji wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa aliipongeza kamati hiyo, wananchi na viongozi mbalimbali kwa kufanikisha kazi hiyo.

Alisema kazi walioifanya ni kubwa mno na italeta faraja kwa wanafunzi baada ya kupata madawati hayo.

"Mimi kama kiongozi mkuu niliye ndani ya Wilaya ya Ikungi ninaye isimamia Serikali kwa hawa walioshiriki kufanya kazi hii tutawatambua kwa kuwapa vyeti vya utambuzi wa kazi hiyo jambo litakalo wasaidia kuwatia moyo" alisema Likapakapa.

Alisema katika utekelezaji wa kazi hiyo anajua walikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za watu waliotoa ahadi kushindwa  kutoa fedha hizo ingawa watoto wao wapo shuleni hapo na watakaliaa madawati hayo.

Likapakapa alitumia mkutano huo kutoa sh.100,000 kama mchango wake wa kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika shughuli za maendeleo.

Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi aliwashukuru wananchi hao kwa kazi hiyo ya kujitolea kwa moyo wa dhati na kuwa wazalendo.

Kisuda alisema mwaka 2015 katika utekelezaji wa ilani ya CCM wilaya hiyo ilitarajia kutengeneza madawati 5000 katika kipindi chote cha miaka mitano lakini hadi sasa wana asilimia 75 ya madawati yote waliyokusudia kuyatengeneza na ili kukamilisha mchakato wa kuyatengeneza ilihitajika nguvu kutoka kwa wananchi pamoja na wadau. 

"Puma imekuwa ni kijiji cha nne kati ya vijiji vilivyoweka jitihada za kutatua changamoto hii ya kutengeneza madawati." alisema Kisuda.

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Unyahati, Nkhoire, Kisuluda na Puma na kuwa wazazi wote waliochangia kutengeneza madawati hayo wametimiza wajibu wao na wanakila sababu ya kupongezwa.

Kisuda alisema kwa muitikio huo waliouonesha halmashauri hiyo inawaahidi kuwapa kipaumbele katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye shule hiyo kama walivyofanya mradi wa choo ambapo kuna shule zaidi ya 108 lakini wameipa shule ya Puma.

Alisema madawati 66 yaliyosalia kutengenezwa kati ya hayo 71 ambayo yapo tayari halmashauri hiyo itatoa mbao 20 ili kuyatengeneza ambapo alitoa mwito kwa wananchi hao kuendeleza jitihada hizo za shughuli za maendeleo katika kata hiyo.