Matokeo chanyA+ online




Monday, December 7, 2020

BARAZA LA MAWAZIRI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 05 Desemba, 2020 amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi wa leo, Mhe. Rais Magufuli amewateua Mawaziri 21 ambao wataungana na Mawaziri 2 walioteuliwa tarehe 13 Novemba, 2020, na amewateua Naibu Mawaziri 23. Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wabunge 2 ambao pia amewateua kuwa Mawaziri.

Pia, Mhe. Rais Magufuli ameongeza wizara mpya 1 ambayo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Elias John Kwandikwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 

2.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

 

3.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 

4.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jumaa Hamidu Aweso kuwa Waziri wa Maji.

 

5.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

6.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jenister Joakim Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

 

7.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliyekuwa akishughulikia Afya, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

8.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji)

 

9.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 

10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

 

11.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

 

12.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

 

13.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Selemani Saidi Jafo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

 

14.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Medard Matogolo Kalemani kuwa Waziri wa Nishati.

 

15.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Leonard Chamuriho kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Mhandisi Chamuriho ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

16.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Adolf Faustine Mkenda kuwa Waziri wa Kilimo.

 

17.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Waziri wa Madini.

 

18.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

 

19.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. George Boniface Taguluvala Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

20.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Ally Mwalimu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

 

21.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

Tayari Mhe. Rais Magufuli alishawateua na kuwaapisha Waheshimiwa Mawaziri 2 ambao ni Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango na Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

Naibu Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

 

2.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 

3.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).

 

4.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

5.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

 

6.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

 

7.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI).

 

8.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.

 

9.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

 

10.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

11.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

 

12.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini.

 

13.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

 

14.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).

 

15.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.

 

16.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

17.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

 

18.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

19.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

 

20.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

 

21.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

 

22.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

 

23.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

 

Wateule wote wataapishwa wiki ijayo Jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.

Sunday, December 6, 2020

TANZANIA YAFUNGUA OFISI YA MWAKILISHI WA HESHIMA JIJINI MUMBAI

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda kwa pamoja na Mwakilishi wa Heshima Mteule wa Tanzania jijini Mumbai Bwana Nayan Patel wakisaini Mkataba wa Kazi wa kumwezesha Bwana Patel kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika mji huo. Mkataba huo ulisainiwa jijini Mumbai, India tarehe 04 Desemba 2020.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda na Bwana Nayan Patel wakibadilishana Mkataba wa Kazi wa kumwezesha Bwana Patel kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika mji wa Mumbai.

Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania Jijini Mumbai Bwana Nayan Patel akihutubia katika hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania Jijini humo iliyofanyika tarehe 04 Desemba 2020.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa hotuba kumpongeza Bwana Patel kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania jijini Mumbai na kumtaka kuiwakilisha vema nchi.


Balozi wa Tamzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania Jijini Mumbai Bwana Nayan Patel wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni walioshriki halfla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Kazi wa Mwakilishi wa Heshima.


Serikali ya Tanzania imefungua rasmi ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika Jiji la Mumbai katika hafla iliyofanyika jijini humo tarehe 04 Desemba 2020.

Mumbai ni jiji kuu la biashara na viwanda nchini India (commercial and industrial hub) ambapo linachangia zaidi ya asilimia 6 la pato la India na pia linachangia zaidi ya asilimia 25 ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani nchini India (25% of industrial output).

Aidha, Mumbai ni jiji mojawapo kati ya majiji kumi duniani, yanayoongoza kwa biashara, hususan katika mzunguko wa fedha duniani (global financial flow). Vilevile, Mumbai ni Jiji linaloongoza kuwa na mabilionea wengi nchini India, ambapo linashika nafasi ya 9 kuwa na mabilionea wengi duniani.

Kadhalika, shughuli za biashara na huduma za kifedha katika Jiji hilo lenye watu zaidi ya milioni 20 zinachangia mzunguko wa fedha katika uchumi wa India kwa zaidi ya asilimia 70.

Ni kutokana na umuhimu wa Jiji hilo, Serikali iliamua kusogeza karibu huduma za kikonseli, biashara, uwekezaji, utalii na mengineyo kwa kuwa na Mwakilishi wa Heshima atakayeratibu shughuli hizo kwa karibu. Ikumbukwe India ni nchi kubwa yenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu duniani wanaofikia bilioni 1.2. Hivyo, si rahisi kwa nchi zenye uwakilishi mjini New Delhi kuweza kuhudumia kwa ukamilifu nchini India bila kuwa na ofisi za aina hii.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda alielezea juu ya umuhimu wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima jijini Mumbai kuwa itasaidia kutoa huduma za Kikonseli kwa karibu zaidi na pia itasaidia zaidi kuvutia na kutangaza fursa mbalimbali za biashara, uwekezaji zilizopo nchini, kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo na viwanda vya Tanzania pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii wa Tanzania ili kukuza sekta ya utalii nchini.

Aidha, Balozi Luvanda alieleza kuwa ofisi hiyo itachangia katika kukuza biashara zaidi kati ya Jiji la Dar es Salaam na Mumbai kufuatia kuimarishwa kwa huduma za usafiri wa anga baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuanza safari zake za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai tangu mwezi Julai 2019. Vilevile, majiji haya yanaunganishwa na bandari kuu muhimu ambazo ni Bandari ya Dar es Salaam, kwa upande wa Tanzania, na Bandari ya Mumbai, kwa upande wa India.

Bwana Nayan Patel, ni raia wa India na mfanyabiashara mwenye mtaji mkubwa jijini Mumbai na amekwishaanza rasmi kazi ya Uwakilishi wa Heshima baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kidiplomasia. 

Bwana Patel aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa heshima kubwa ya kuiwakilisha Tanzania jijini Mumbai na maeneo mengine ya jirani na akaahidi kuitendea haki nafasi hiyo kadri atakavyoweza.

Friday, December 4, 2020

KATIBU MKUU MIFUGO ATAKA, SAYANSI YA MIFUGO ITUMIKE KULETA MABADILIKO


 

Katubu mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla hiyo fupi.

 Na.Mwandishi wetu Arusha.

Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa  Elisante Ole Gabriel amezindua  maabara mbili  ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA),Tengeru katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Akizungumza katika hafla fupi ya Uzunduzi wa maabara hizo Profesa Ole Gabriel alisema kuwa sekta ya Mifugo inathamani kubwa katika kuhakikisha kuwa inachangia Pato la Taifa kwa kiwango kikubwa,lakini bado haijafanya hivyo.

Ole Gabriel alisema kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa kuwa itawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo hali ambayo itaongeza uwezo  katika masomo yao.

Aidha alisema kuwa Sayansi inahitajika katika kuhakikisha kuwa wafugaji wanabadili ufugaji na kuwa na Mifugo Bora zaidi pamoja na mazao yenye thamani ambayo yanatokana na Mifugo.

"Tunahitaji Sana Sayansi ya Mifugo ambayo itatusaidia kupata nyama bora,maziwa bora na hata bidhaa nyingine zote ili basi idadi tuliyonayo ya Mifugo iendane na thamani ya Mifugo yetu na hivyo tutapata Mifugo Bora zaidi"alisema Profesa Ole Gabriel

Hata hivyo alisema kuwa uwepo wa maabara hizo mbili pamoja na vifaa vitawezesha wanafunzi hao ambao wanakwenda kusaidia wafugaji wa chini katika kuhamilisha na kuchanja Mifugo kubobea katika sekta hiyo na Mifugo kuwa Bora zaidi.

Pia alisema kuwa mpango wa wizara hiyo bado ni kuboresha  kosafu na mbari za mifugo,ili kupata Mifugo bora na bidhaa bora zaidi na hatimaye kuchangia Uchumi kwa asilimia 15 tofauti na Sasa Ambapo sekta hiyo inachangia 7.64.

Nae Mtendaji  Mkuu  wa Wakala wa  Vyuo vya Mifugo wa dkt.Pius Mwambene alisema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuboresha mafunzo  na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanawasaidia wafugaji katika kubadili  ufugaji wa mazoea.

Alisema  kuwa  ni  azma  ya Serikali kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu Mbali Mbali ili kuhakikisha kuwa sekta ya mifugo inachangia ipasavyo  pato la taifa.

Nchi ya Poland imekuwa ikiisaidia Serikali katika sekta ya Mifugo katika kuhakikisha kuwa inaongeza thamani ya mifugo ili kuongeza tija katika sekta hiyo.

Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel wa Tatu Kushoto akiwa pichani na Viongozi Mbali Mbali Mara baada ya Uzinduzi wa Maabara hizo.

Thursday, December 3, 2020

MBUNGE WA UKONGA, JERRY SILAA ATEMBELEA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA APOKEA CHANGAMOTO

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa amefanya ziara katika Hospital ya Mama na Mtoto iliyopo Nguvu Kazi Chanika ambapo pia amepokea kero mbalimbali.

Katika ziara yake hiyo Jerry Silaa ameweza kutembelea vitengo vyote vya Hospital na kupokea Changamoto mbali mbali ikiwemo eneo ambalo linatakiwa kujengwa chumba cha kuhifadhia maiti, kujengwa General Wodi pamoja na  mahitaji ya kuzungushiwa ukuta hospitali hapo.

Akiwa katika ziara hiyo, Jerry Silaa ameweza pia kumpa pole mmoja wa akina mama ambaye alieleza changamoto zake za uzazi kutokana na kufuata huduma mbali.

"Hospitali hii kwa sasa imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Jimbo la Ukonga na maeneo ya nje ya Ukonga.

Pole sana Mama Samia.... kwa changamoto ulizokutana nazo awali na kwa sasa Serikali yetu chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kero zote zimeendelea kutatuliwa."  Alisema Jerry Silaa.

Akimuelezea mama huyo aitwae Samia ambaye alijifungua mtoto wa kiume na bado hajapewa jina,


"Mama Samia anaishi Yongwe Chanika huyu ni mtoto wake wa tatu.

Wa kwanza alijifungulia umbali wa Kilometa 40 Hospitali ya Amana (Bahati Mbaya), Wa pili alijifungulia tena Amana yupo hai.

"Mama Samia alijiwekea nadhiri hatazaa tena...Hospitali hii ilipojengwa amebadilisha mawazo. Mama Samia ni mmoja kati ya kina mama 25-30 wanajifungua hapa toka Kata ya Chanika na Kata za jrani, Kisarawe na Mkuranga wanaojifungulia hapa" Alieleza Jerry Silaa.

Mbunge huyo ambaye anahistoria kubwa na Hospitali hiyo kwa kuiomba kwa serikali ya Korea, Kuandika upembuzi yakinifu wake , kupata msaada na hadi kusaini mkataba wa ujenzi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania  alisema wazo na ombi lake huko nyuma leo limekuwa msaada mkubwa kwa Mama Samia na akina mama wengine wanaofika kupata huduma Hospitalini hapo.

"Ningeweza kunywa soda na Naibu Spika wa Korea, kumshukuru kwa Hospitali ya Mnazi mmoja, tukacheka na angeondoka.

Niliamua kuukana unazi na kumweleza wazi waliojenga Hospitali Mnazi mmoja walikosea.

Leo Mama Samia na wengine wengi wanapata huduma hapa" Alieleza Jerry Silaa.

MTATURU ATIMIZA AHADI YAKE KWA VITENDO.




Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameendelea na ziara yake jimboni humo ambapo ametembelea miradi minne ya ujenzi wa miundombinu ya elimu yenye thamani ya Sh Milioni 196 inayotekelezwa na serikali katika shule ya sekondari ya Unyahati.

Miradi hiyo ni ujenzi wa bweni moja,madarasa matatu,maabara tatu na matundu sita ya vyoo.


Pamoja na kutembelea miradi hiyo,Mtaturu ametimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa kwa shule hiyo ya kupeleka mashine ya kuchapa (Printer) moja yenye thamani ya zaidi ya Sh laki tano inayofanya kazi ya kuchapa,kunakili na kuskani.

Akizungumza Disemba mosi 2020, akiwa katika ziara hiyo Mtaturu amemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuwapelekea fedha zilizofanikisha ujenzi huo.


“Katika Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM iliyopita na hii ya sasa imeeleza dhamira ya kuboresha miundombinu ili kuweka mazingira rafiki ya kujifunza na kufundishia,kwa niaba ya wana Singida Mashariki nimshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kuleta fedha maana kuahidi ni jambo moja lakini kutekeleza ni jambo la pili,Rais wetu ametekeleza,”alisema.

Amesema mbali na kutoa fedha hizo amewezesha upatikanaji wa elimu bila ya malipo na hivyo kupelekea uwepo wa mafanikio mbalimbali ikiwemo ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa na ongezeko la ufaulu.


Ili kuunga mkono juhudi hizo za serikali Mtaturu ametimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa ya kuwapa motisha wanafunzi watano waliofaulu kwa daraja la kwanza kwa kuwapa Sh laki moja kila mwanafunzi na walimu waliopelekea uwepo wa ufaulu huo.

“Niliahidi kuunga mkono juhudi za serikali,na katika vipaumbele vyangu saba nilivyoahidi kuvisimamia kipaumbele cha kwanza ni katika sekta ya elimu,na hapa nimesema nitakuwa kinara katika kusimamia  sekta hii kwa kushirikiana na serikali,na sasa natimiza ahadi yangu ya kutoa Sh laki moja kwa kila mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana  ambao sasa hivi wapo kidato cha tano,hivyo nakabidhi Sh laki tano,


“Najua mafanikio haya ya wanafunzi hayajaja yenyewe,bali yametokana na juhudi za walimu wetu,niliahidi na natimiza ahadi yangu ya kuwapa Sh laki moja kwa walimu wote kama njia ya kuwapongeza kwa kuwawezesha vijana wetu kufanya vizuri,na hii ni motisha ili mfanye vizuri zaidi ya mlivyofanya sasa,”alisema Mtaturu.

Amehimiza mshikamano katika suala zima la ufundishaji ili kuendelea kuboresha taaluma.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo mwalimu mkuu Method Njiku amemshukuru Rais Magufuli kwa fedha alizopeleka na kumshukuru pia Mbunge Mtaturu kwa uthubutu wake wa kuwashika mkono kwa kile walichoonyesha.


Kwa upande wake diwani wa Kata ya Unyahati Abeli Surri amemshukuru mbunge huyo kwa kuwatembelea na kusema miaka yote kumi ya udiwani wake hajawahi kutembelewa na mbunge.

"Mbunge wetu tangu umeingia bungeni umekuwa ukitusemea kero zetu na matunda yake tunayaona miradi mingi tunaipata,ahsante sana,"alishukuru diwani huyo.

DKT. ABBASI: SERIKALI INAKUJA NA TAMASHA, TUZO KUBWA ZA SANAA

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametangaza kuwa kutokana na urithi mkubwa wa sanaa uliopo nchini ikiwemo muziki, filamu, ngoma na uga mwingine, sekta hiyo inapaswa kuhakikisha inaiburudisha jamii yetu ya wachapakazi ipasavyo na kwa kuanzia Serikali kwa kushirikiana na wadau itaratibu Tamasha kubwa la aina yake la Muziki na Sanaa litakalotumia jina la moja ya vivutio vikubwa vya utalii hapa nchini. Adha, amesema kuanzia mwakani Serikali pia itashirikiana na wadau kurejesha tuzo za muziki na sekta nyingine za Wizara hiyo.

"Moja ya kazi kubwa ya sekta ya sanaa nchini ni kuhakikisha jamii yetu inayochapa kazi sana kwa sasa inaburudika ipasavyo, sasa naona sanaa inakuja tu pale panapokuwepo mdhamini au mwandaaji fulani asipokuwepo hakuna matukio na nchi iko kimya.


Serikali sasa inakwenda kuchechemsha sekta hii kwa kuratibu Tamasha kubwa sana litaanzia Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kuendelea kuungana na Tamasha la Kimataifa la Sanaa Bagamoyo. Tusisibiri wadhamini, wakija sawa, kama wako likizo, basi mimi nasema sisi wenyewe tunaweza kwa umoja wetu sasa tukutane Uwanja wa Uhuru Disemba 26 mwaka huu na kisha Desemba 27 twende Bagamoyo.

"Wasanii wakoungana watajaza Uwanja. Twende Tutateremsha wasanii wetu wote ambao ni urithi wa sasa na baadaye wa nchi hii halafu tuone kama watu hawatakuja," alisema Dkt. Abbasi akiwa katika siku ya tatu ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na wasanii wa Bongo Movie.