![]() |
Tuesday, February 7, 2023
Monday, February 6, 2023
BILIONI 14 ZAJENGA SHULE MPYA 11 NA VITUO VYA AFYA 12 RUVUMA
Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 14 kujenga shule mpya za sekondari
11 na vituo vya afya 12 mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa
umefanikiwa kujenga shule hizo mpya katika Halmashauri zote nane za
Mkoa wa Ruvuma kwa gharama ya shilingi Bilioni 7.7.
“Ujenzi huu unajumuisha shule ya Mkoa ya Wasichana inayojengwa eneo
la Migelegele Kata ya Lwinga katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
kwa gharama ya shilingi bilioni nne’’,alisema Kanali Thomas.
Hata hivyo amesema Mkoa umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa
792 elimu msingi na sekondari yakijumuisha madawati, viti na meza kwa
gharama ya Shilingi Bilioni 14.93
Kwa mujibu wa Kanali Thomas,Mkoa umefanikiwa kujenga mabweni
matano ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa gharama ya
shilingi Milioni 640 na kwamba Mkoa ulipokea fedha kiasi shilingi milioni
400 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara 23 za Shule za Sekondari kupitia
fedha za Tozo na Serikali Kuu.
Akizungumzia kuhusu sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii,Kanali Thomas
amesema Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga Vituo vya Afya 12
kupitia fedha za Tozo na Serikali Kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi
bilioni 7.8.
Ameongeza kuwa Mkoa umefanikiwa kujenga nyumba tisa za watumishi
wa Afya kwa gharama ya shilingi Milioni 856 na kwamba Mkoa
umefanikiwa kujenga majengo matatu ya huduma za dharura (EMD) Kwa
gharama ya Shilingi Milioni 900.
Kulingana na Kanali Thomas Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga jengo
moja la wagonjwa mahututi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa
gharama ya shilingi milioni 250 na kujenga zahanati 21 kwa gharama ya
zaidi ya shilingi bilioni moja.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma unaendelea na ujenzi wa Hospitali
tano za Wilaya ya Nyasa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri
ya Madaba na Halmashauri ya Songea kwa gharama ya Shilingi bilioni 3.4
Amesema serikali pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa awamu ya kwanza katika eneo la Mwengemshindo Manispaa ya
Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo unahusisha jengo la wagonjwa wa nje
(OPD), jengo la mionzi na nyumba ya mtumishi na kuongeza kuwa hali ya
upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea
huduma za afya upatikanaji umeongezeka na kufikia asilimia 96.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. PHILIP MPANGO AKUTANA NA MWANAMFALME WA DUBAI FEB 6 2023
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon LLC ambaye ni Mwanamfalme wa Dubai Mheshimiwa Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum, alipofika kumsalimia Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Februari 2023.
|
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum ambaye ni Mwanafamilia wa Utawala wa Mji wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya Picha ya Jengo la Kihistoria la Zanzibar, Bait el Ajaib, Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.
|
RAIS SAMIA ATOA SULUHU MGOGORO WA ARDHI KINGALE - KONDOA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a ambao wamekuwa kwenye mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74. Mwishoni mwa wiki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu ya mgogoro huo kwa kuzingatia mahitaji ya Wananchi.
RAIS SAMIA ATOA SULUHU MGOGORO WA ARDHI KINGALE - KONDOA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu kwenye mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74 lililopo katika Vijiji vya Kata ya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a ambalo ni eneo lenye rutuba kwa shughuli za kijamii za uzalishaji.
Suluhu hiyo imewasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Mhe. Rais na ameitoa mbele ya wananchi wa Kata hiyo wakiwa na viongozi wao.
"Ardhi yote ni mali ya Serikali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipofika hapa alifikisha hili jambo kwa Mhe Rais aamue na Rais ametoa suluhu kwa Wanakingale. Amesema eneo lenye mgogoro la ukubwa wa ekari 7,495.74, ekari 3,272.4 zibaki kwa wananchi watumie kwa shughuli za kilimo, mifugo na za kiuchumi na Magereza watachukua ekari zilizobaki" amesema Mhe. Senyamule
Mbali na kuwasilisha utatuzi pia Mhe Rais ameagiza mambo kadhaa yafanyike katika eneo hilo; "Mhe. Rais ameagiza kuwa ndani ya mwezi mmoja, watu wa ardhi waje kuonyesha utaratibu wa maeneo yaliyogawanywa, yapimwe na alama ziwekwe zinazoonekana kwa kila mmoja. Vijiji tuendelee kutunza mipaka kuzuia mwingiliano wa matumizi, Magereza pia mtunze mipaka, wananchi wapo upande wa Bonde linalofaa kwa umwagiliaji. Wizara ya Kilimo mfanye utaratibu wa kujenda mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji, mifungo pia mjenge majosho kwa ajili ya kuosha mifungo ya wananchi" Ameongeza Mhe. Senyamule
Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi hao kufanya maendeleo kwa kushirikiana na Magereza kwani mgogoro umekwisha hivyo kutokana na miundombinu itakayojengwa kwenye eneo hilo, itawawezesha kupiga hatua kubwa kwa haraka na kumfanya Mhe. Rais kujivunia kuwapatia eneo hilo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mji Mhe. Ally Makoa amesema mapendekezo ya ya kupatiwa eneo waliloomba kutoka kwenye mpaka wa Magereza waliyowasilisha kwa Rais, ndicho kilichoamuliwa hivyo wananchi hao wataendelea kutumia eneo lao la mashamba huku Magereza nao wakibaki na eneo lao. Hakusita kutoa pongezi zake kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta wataalamu kutoka Wizarani kwa ajili ya kujenga miundombinu kwenye eneo hilo pamoja na kuridhia mapendekezo ya wananchi.


































.jpg)