Matokeo chanyA+ online




Tuesday, January 29, 2019

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI ZANZIBAR

IMG_1418
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, kuhusiana na maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Mshauri wa Rais Masuala ya Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Abdulrahman Mwinyijumbe, mkutano huo umefanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
IMG_1420
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, kuhusiana na Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Kilimo Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.
IMG_1437
 Waziri wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma, akiwasilisha ripoti ya Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara yake ,wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
IMG_1442
IMG_1444
 Viongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia taarifa ya maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi.Mhe. Rashid Ali Juma, wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
IMG_1451
 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Sadalla, akichangia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,kuzungumzia maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
IMG_1462
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII

PMO_09899
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Jakaya Kikwete jijiniDodoma kufungua mkutano huo, Januari 29, 2019.
PMO_9906
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza mtoto, Hussein Jailal (kushoto) wakati alipotoa ushuhuda kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, uliofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019.
PMO_9916

PMO_9925

PMO_9934
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Mwaka  wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9940

PMO_09950

PMO_9953
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019.
PMO_9795
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mtoto, Faisal Rashidi Haroun kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019. Kushoto ni Mama Mzazi wa mtoto huyo, Habiba Mohammed.
PMO_9876

PMO_9880
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Fundi Mkuu wa Karakana ya Vifaa Visaidizi vya Wenye Ulemavu iliyopo eneo la Sabasaba jijini Dodoma, Bw. Mwita Marwa Maki baada ya kuvutiwa na baiskeli za magurudumu matatu zilifungwa mota ambazo zimebuniwa na zinatengenezwa na karakana hiyo. Tukio hilo lilifanyika kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, kabla ya Waziri Mkuu kufungua Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


*Awataka wajiepushe na rushwa wafanye kazi kwa bidii, weledi na uadilifu
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa watekeleze majukumu yao kwa bidii, weledi, uadilifu na wasijihusishe na vitendo vya rushwa.

Amesema maafisa hao wanatakiwa watumie mbinu shirikishi ambazo zinahusisha jamii yenyewe na wataalamu ambao ni watoa huduma ngazi ya jamii (Community Case Worker) ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Januari 29, 2019) kwenye Mkutano wa Mwaka wa Kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, jijini Dodoma.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka maafisa hao wahakikishe kwamba haki za msingi za makundi hayo zinapatikana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo katika kutoa huduma ya taaluma yao.

Amesema taaluma ya Ustawi wa Jamii imepewa dhamana ya kuwa mlinzi wa mtoto, kumhudumia na kusimamia haki zake, hivyo amewatakawazuie na watokomeze aina zote za ukatili kwa watoto, wazee na wenye ulemavu.

Waziri Mkuu amesema jukumu hilo pia linahusisha watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi na wanaoishi na kufanya kazi mitaani, wazee, wanawake wasio na uwezo na watu wenye ulemavu.

Amesema pamoja na mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeyapata ni muhimu wakaendelea kuongeza nguvu na weledi ili kutorudi nyuma katika kujenga msingi wa kuimarisha ustawi wa makundi maalumu.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza maafisa hao wakasimamie utekelezaji wa mkakati wa  Mkono kwa Mkono, Familia kwa Familia, Kaya kwa Kaya kupitia huduma ya kuzuia ukatili ngazi ya familia wenye lengo la kuzuia ukatili ndani ya familia ili ulete matokeo tarajiwa.

“Tambueni umuhimu wenu na kwamba jamii inawategemea kutekeleza majukumu yenu kikamilifu ili kupunguza matatizo ya kijamii kwa wale wenye uhitaji wakiwemo watoto, watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye migogoro na akina mama wanaonyanyaswa na makundi mengine.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewashukuru wadau wa maendeleo kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo likiwemo suala la uimarishaji wa huduma za ustawi wa jamii nchini.

Amesema anatambua mchango mkubwa kutoka kwa shirika la UNICEF, USAID, UN WOMEN, UNFPA, John Snow Inc, Pact, HelpAge International, World Vision, Save the Children, Plan International na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wameendelea kushirikiana na Serikali kuinua kiwango cha utoaji huduma za ustawi wa jamii nchini.

“Ninapenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, ipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi ili tuweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.”

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Nguzo katika kuelekea Uchumi wa Kati wa Viwanda.”

Waziri Mkuu amepongeza kwa kuanzisha utamaduni huo wa kukutana Watendaji wa Sekta ya Ustawi wa Jamii kwa kuwa hiko ni kiashiria kwamba kuna mabadiliko katika utendaji kwa kuzingatia kuwa mkutano huu haujawahi kufanyika toka mwaka 2006.

Mkutano huo wa siku tatu unajumuisha Maafisa Ustawi wa Jamii 164 kutoka mikoa yote Tanzania Bara, wadau wa maendeleo, wawakilishi wa wazee, watoto waishio katika mazingira hatarishi waliohitimu mafunzo ya VETA pamoja na watoto waliokuwa wakiishi mitaani ambao kwa sasa wameunda kikundi cha burudani.

RAIS DKT.MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI 6 WA MAHAKAMA YA RUFANI NA MAJAJI 15 WA MAHAKAMA KUU TANZANIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Winnie Korosso Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sahel Barke Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Lugano Samson Mwandambo Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Dkt. Mary Levira Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Ignus Paul Kitusi Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kerefu Sameji Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. John Rugalema Kahyoza Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Susan Bernard Mkapa Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Fahamu Hamidu Mtulya Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Cyprian Phocas Mkeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Willbard Richard Mashauri Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dunstan Beda Ndunguru Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Seif Mwinshehe Kulita bKuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Upendo Elly Madeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Yohane Bokobora Masara Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Mustapha Kambona Ismail Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Athumani Matuma Kirati Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Zepherine Nyalugenda Galeba Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dkt. Ntemi Nimilwa Kilikamajenga Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Dkt. Juliana Laurent MasaboKuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Dkt. Lilian Mihayo Mongella Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.

Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Wakuu wa Wilaya wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 Mahakama Kuu. Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakitia saini hati za kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani mara baada ya kuwaapisha Majaji hao na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu,Watumishi mbalimbali wa Mahakama mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu na Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu, Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 10 wa Halmashauri, Mara baada ya kuwaapisha Majaji. Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.
Wakuu wa Wilaya wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 wakiwa katika hafla ya uwaapisho wa Majaji 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama Kuu .Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.