Matokeo chanyA+ online




Saturday, September 28, 2019

DANGOTE APEWA WIKI MOJA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisisistiza jambo kwa uongozi wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Dangote kilichopo Mkoa Mtwara alipotembela kukagua na kusikiliza changamoto za wawekezaji mkoani humo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Jagat Rathee
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametoa muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya miaka miaka mitatu hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.

Waziri Kairuki ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Katika ziara yake ya kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuongea na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi septemba 27,2019 ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila baada ya miezi sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.

Waziri Kairuki aliwaeleza masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa kutowasilisha taarifa za utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya mradi, mipango ya upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo na ushauri wao.

"Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika suala hilo ni la kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia sasa nimewapa wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa haraka,"alisisitiza Waziri Kairuki.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa namna mfumo wa TEHEMA unavyorahisisha utendaji kiwandani hapo na Mhandisi Brezil Omary  wakati wa ziara yake kiwandani hapo.

Sehemu ya wajumbe waliposhiriki katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Balozi Celestine Mushi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.

Afisa Viwango wa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote Bw. Issawema akiwaonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kuendesha kiwanda hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)  
Aidha amewapongeza Dangote kwa uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya taifa.

Amewataka wawekeze na maeneo mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi.

Wakiwa Mkoani Lindi Waziri Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.

Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.

"Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza"alisema Dkt.Mabula

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.

Amesema wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa wananchi.
 
 

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA MHANDISI MANYANYA AFURAHISHWA TAMASHA LA JAMAFEST KUKUZA MILA NA DESTURI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akicheza ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara amefurahishwa jinsi Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam lilivyoweza kukuza mila na desturi za Mwafrika. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea katika uwanja wa Taifa leo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa amefurahishwa jinsi walivyoweza kusogeza ajenda ya Biashara nchini. "Nafurahi kwamba maonesho haya yameshirikisha watu wote, nimefurahi kuone watu wenye ulemavu wanatengeneza bidhaa nzuri ambazo zinawapatia kipato," amesema. 

 Amesema kuwa amefurahiswa kuona Mila na desturi zinafanana, ukiachana masuala madogomadogo tunaweza kushirikiana kwa karibu ili kujenga uchumi mkubwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

"Nimetembelea banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki na nimeangalia takwimu za nyuma kidogo za biashara za nchi wanachama zinaonesha biashara inaongezeka, kwa kiasi kikubwa Sana, kwa hiyo jukumu kubwa ni kujenga amani ili kujenga uchumi wa nchi zetu," amesema. 

 Ameongeza kuwa Tamasha la JAMAFEST ni fursa kubwa kwa wa EAC, kwa hiyo tunaweza kuangalia utaratibu wa kupunguza muda wa miaka miwili ili kuwawezesha watu wetu kufanya biashara na kupanua soko baina ya nchi Wanachama wa EAC. 

Mhandisi Stella Manyanya bidhaa zinazopatikana hapa JAMAFEST zinatufundisha kuwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla tuna vipaji vikubwa sana kutoka kwenye Sanaa na Utamaduni wetu.
Ngoma kutoka nchini Tanzania ikiburudisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akingalia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Watoto wa kitanzania akionyesha umahili wa kupiga ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Burudani ikiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akingalia bidhaa wa wajasiliamali wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (katika) akingalia burudani ya mchezo wa bao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Burudani ya sarakasi ikipamba.
Mchezo wa manyoka nyoka ukiendelea.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili toka kulia) akifuatilia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.

Friday, September 27, 2019

DC MURO ATOA SIKU 3 KWA WENYEVITI WA VIJIJI NA WATENDAJI KATA NA VIJIJI AMBAO HAWAJASOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KUTOA MAELEZO

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na maafisa watendaji wa kata na vijiji

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na maafisa watendaji wa kata na vijiji
 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ametoa siku 3 kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na maafisa watendaji wa kata na vijiji kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi pamoja na taarifa za maendeleo ya vijiji

Dc Muro amewalekeza wakurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dkt. Charles Mahera  pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Ndugu Emannuel Mkongo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watendaji ambao ndani ya siku tatu watabainika walizembea kwa makusudi kutosimamia uandaaji na usomaji wa taarifa hizo kutokana na kubaini kuwepo kwa vijiji ambavyo kwa zaidi ya miaka 3 sasa hawajawai kusoma taarifa hizo kwa wananchi.

Dc Muro amezungumza maneno hayo katika zaira ya kata ya Sing’isi na Nkwaranga ambapo anaendelea na ziara za kata 53 katika Ukaguzi wa miradi ya Maendeleo pamoja na kutatua kero Sugu za wananchi.

NGOMA ZA MATAIFA MBALI MBALI ZAZIDI KUPAMBA TAMASHA LA JAMAFEST 2019

Kikundi cha Ngoma na Sarakasi cha Safi kutoka nchini Tanzania kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Mmoja ya kijana wa kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi kutoka Tanzania akionyesha umahili wake wa kucheza kwa kutumia shingo na mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Vijana wa Kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi wakionyesha umahili wao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wakiwaaga wanajumuiya wa Afrika Mashariki waliohudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wasanii wa Kenya wakionyesha umahili wao wa kuigiza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma toka Zanzibar, Tanzania wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma ya Kisukuma kutoka Wilaya ya Buchosa, Sengerema - Mwanza wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Akina mama wa Kigogo wanaweza, wakionyesha umahili wao wa kupiga ngoma na kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Ngoma ya kigogo toka Dodoma wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Kenya kikionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili toka kushoto) akishuhudia ngoma za mataifa toka Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kuhudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Mambo ni moto!