Matokeo chanyA+ online




Wednesday, May 27, 2020

TUME YA UCHAGUZI IMEKUTANA NA VYAMA VYA SIASA NA KUJADILI NA KUPITISHA KANUNI NA MAADILI KWA UCHAGUZI MKUU

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, akizungumza katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu  Semistocles Kaijage, akifafanua hoja zilizotolewa na Washiriki wa Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu  Semistocles Kaijage, akifafanua hoja zilizotolewa na Washiriki wa Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, akiendesha Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, akiendesha Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera, akizungumza katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu. Humphrey Polepole akichangia hoja katika  Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa  Rais, Wabunge na Madiwani wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu.Francis Mutungi akifuatilia Mkutano wa NEC na  Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu  wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika  27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika  akichangia hoja katika  Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa  Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

CCM YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KATA YA UTENGULE, MAKAMBAKO

Na Amiri kilagalila,Njombe

Uongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe umesema umeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho katika kata ya Utengule halmashauri ya mji wa Makambako,kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Njombe ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako HANANA MFIKWA wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo,ambapo amesema,miradi yote ikiwemo ya afya,miundombinu ya Barabara na umeme imetekelezwa kwa asilimia kubwa.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano afisa mtendaji wa kata ya Utengule MOSSES MWALONGO kwa niaba ya diwani amesema kuwa kata hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu msingi na Sekondari.

Naye diwani wa kata ya Utengule STEPHANO MGOBA amesema amefanikiwa kutekeleza miradi hiyo kutokana na kuwashirikisha wananchi na kueleza kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitano ametumia fedha zake binafsi zaidi ya milioni 20 kuwawezesha wananchi katika shughuli zao. Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo wameridhishwa na utendaji kazi wa diwani huyo kwa kipindi hicho cha miaka mitano.

Tuesday, May 26, 2020

“CORONA ISIWE KISINGIZIO CHA KUTONUNUA KITAMBULISHO CHA UJASILIAMALI”- RC WANGABO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaasa wajasiliamali Mkoani Rukwa kutotaja ugonjwa wa Corona (Covid-19) kama kikwazo cha kushindwa kununua kitambulisho cha mjasilimali kwa mwaka huu 2020, kwani wananchi wa Tanzania walihimizwa kuendelea kuchapa kazi na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hali ambayo ni tofauti na nchi nyingine ambapo wananchi wake walikuwa wamefungiwa.
Mh. Wangabo amekataza vitambulisho hivyo kuuzwa rejareja kwani jambo hilo huzalisha wadaiwa (defaulters) na hivyo kuwataka wahusika kuviuza vitambulisho hivyo kwa fedha taslimu na kisha fedha hizo ziwasilishwe kwenye akaunti ya Katibu Tawala wa Mkoa ili zifikishwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kutumika katika maendeleo ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) Akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda vitambulisho vya ujasiliamali vya mwaka 2020.
“Kwahiyo fedha zitolewe kabla ya kupewa kitambulisho lakini kusiwe na kisingizio cha Covid – 19, kwamba mzunguko wa fedha, sijui nini, hiki ni kitambulisho kinachomtambulisha mjasiliamali ili asipate bugudha yoyote, vinginevyo ukisema kwamba huwezi, watawabugudhi , kwa namna wanayoona wao na kwa sheria zao, kwasababu hawakutambui wewe kama mjasiliamali mdogo, wewe unajitambua lakini hutambuliki, Mheshimiwa Rais amekupa heshimu ya kukutambua kuwa wewe ni mfanyabiashara mdogo, ukivaa kitambulisho chako unakwenda nchi nzima,” Alisema.
Aidha, Mh. Wangabo alitaja changamoto kadhaa zilizokwamisha zoezi la kwanza la uuzaji wa vitambulisho hivyo ikiwemo usimamizi na ukosefu wa Kanzi data ya wafanyabiashara wadogo pamoja na ucheleweshaji wa kuweka mapato kwenye akaunti ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) hali iliyopelekea kuchelewa kwa taarifa, hivyo kuwaonya wale wote watakaochelewa kuweka fedha hizo kwenye akaunti ya RAS.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) Akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule vitambulisho vya ujasiliamali vya mwaka 2020.

Mh. Wangabo ametoa kauli hizo wakati akikabidhi vitambulisho 3,000 vya awamu ya kwanza kwa wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Rukwa ambapo kwa mwaka 2019, Mkoa wa Rukwa ulipokea vitambulisho 55,000 na kuuza vitambulisho 32,028 ambavyo ni sawa na asilimia 58.2 na hivyo kukusanya shilingi 640,560,000/= na mwaka huu mkoa unatarajia kupokea vitambulisho 25,000.
Akitoa neno la shukrani Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alimuhakikishia mkuu wa Mkoa kuwa maelekezo yanayotolewa na serikali hayahitaji kujadiliwa zaidi ya kuyatekeleza na kuongeza kuwa changamoto zozote watakazokumbana nazo watakuwa tayari kukabiliana nazo ili kuhakikisha uchumi wa nchi unaimarishwa na wanachi wenyewe.
“Mimi nimepokea na nitakwenda kutekeleza kwasababu maelekezo ya serikali sisi watendaji tulioko huku chini tunayapokea na kuyatekeleza, kwahiyo changamoto zozote ambazo zitajitokeza, tutakabiliana nazo kwasababu mimi pia naamini, uchumi wa nchi hii utajengwa na wananchi wenyewe, kwahivyo hii ni sehemu ya wananchi katika kuokoa na kuimarisha uchumi wa nchi yao kwa faida yao, kwahiyo ni suala ambalo tunaipongeza serikali na wajasiliamali wadogo wana nafasi ya kuchangia kwenye uchumi wa nchi yao,” Alisema.
Kwa awamu ya Kwanza, Manispaa ya Sumbawanga wamepewa vitambulisho 800, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wamepewa vitambulisho 800, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi wamepewa vitambulisho 800 na Halmashauri ya Wilaya ya kalambo Wamepewa vitambulisho 600 na hivyo kusubiri awamu ya pili ya ugawaji huo ambao utahusisha vitambulisho 22,000 kwa halmashauri zote nne za mkoa huo.

SHEIKH KISUKE: USHIRIKIANO BAINA YA WAISLAMU, WAKRISTO UTADUMU MILELE

 Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Manispaa ya Singida, Alhaji Sheikh Hamisi Kisuke.



Na Dotto Mwaibale, Singida

Umoja na ushirikiano uliopo baina ya Waislamu na Wakristo utaendelea kudumu milele hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Manispaa ya Singida, Alhaji Sheikh Hamisi Kisuke, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya Idd Pili.

Kisuke alisema kushirikiana, kupendana na kuheshimiana baina ya Waislamu na Wakristo ndio kunadumisha hali hiyo hapa nchini.

Alisema Waislamu na Wakristo wamekuwa wakijumuika pamoja katika sherehe zao mbalimbali kama za Idd na Krismas na kila upande ukiona shehere hizo kama ni zake.

" Wakati wa sherehe hizo Waislamu wamekuwa wakiwaalika wakristo na wakristo nao wamekuwa wakiwaalika waislamu" alisema Kisuke.

Kisuke alisema jambo hilo  liliasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alisema Serikali ya Tanzania haina dini ila wananchi wake ndio wanadini.

Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa Corona Kisuke alimpongeza Rais John Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na viongozi wengine kwa hatua walizozichukua za kukabiliana na ugonjwa huo.

Alisema wao katika ibada ya Idd walifuata maelekezo yote ya kuchukua tahadhari yaliyotolewa na  Mufti Mkuu wa Tanzania, Aboubakary Bin Zubeir, ambapo kila Muislamu aliswali katika msikiti wake badala ya kukusanyika katika viwanja maalumu kama ilivyozoeleka.

"Wakati wa ibada ya Idd tulichukua tahadhari zote kama kunawa mikono kwa maji tiririka, kuvaa barakoa na kuswali kwa kuzingatia umbali wa mita moja huku wakiwepo maafisa afya ambao walikuwa wakisimamia zoezi hilo la kuchukua tahadhari" alisema Kisuke ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Misuna.

Monday, May 25, 2020

RC SINGIDA ATAKA UADILIFU UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI AWAMU YA PILI 2020

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020 vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli mkoani hapa jana. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewataka maofisa wa Serikali watakao kuwa wakigawa vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020 vilivyotolewa na Rais John Magufuli kuwa waaminifu na waadilifu.

Dkt.Nchimbi alitoa ombi hilo jana wakati akiwakabidhi vitambulisho hivyo wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Singida.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.

"Rais John Magufuli mwaka huu tena ametuletea vitambulisho hivi pamoja na malengo mengine vinadhihirisha kwamba Tanzania wananchi wake wote wanafanya kazi katika ngazi mbalimbali wakiwamo wajasiriamali na kuwa hakuna zuio la kutofanya kazi wakati huu wa kipindi cha Covid-19" alisema Nchimbi.


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.

Dkt.Nchimbi alimpongeza Rais Magufuli kwa malezi yake ya kipekee kwa Watanzania na hatua aliyoichukua kukabiliana na Corona.

Alisema Tanzania hivi sasa tupo katika safari ya kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ukiwepo Mkoa wa Singida hivyo vitambulisho hivyo vitatoa fursa zaidi kwa wajasiriamali kutambulika.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba,  vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020. 
 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri , akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Justice Kijazi, Afisa Biashara, Sigisberto  Mwacha na Katibu Tawala, Winfrida Funto.

Dkt. Nchimbi alisema vitambulisho hivyo vimewafanya wajasiriamali kuthaminiwa, kutambuliwa, kuwa na haki na fursa ya kushiriki kufanya biashara pamoja na kuiamini Serikali yao.

Alisema kabla ya Rais Magufuli ajaanzisha utoa wa vitambulisho hivyo wajasiriamali walikuwa hawathaminiwi bidhaa zao zilikuwa zikiharibiwa na hawakuwa na uwezo wa kuratibu mipango ya biashara zao lakini leo hii wanaheshimika na hakuna tena zile tozo walizokuwa wakizitoa ambapo kwa mwaka zilikuwa ni nyingi tofauti na sasa.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea itambulisho hivyo.

Aliongeza kuwa vitambulisho hivyo vitakuwa vikitambulika kila wilaya kwa namba maalumu na mjasiriamali atalipia sh.20,000 kwa njia ya mtandao na fedha hizo zitaingizwa kwenye mfumo wa upokeaji wa fedha za Serikali tofauti na ilivyokuwa mwaka jana ambapo kila mtu aliweza kupokea fedha hizo toka kwa mjasiriamali hivyo kuleta changamoto ya utunzaji wa fedha hizo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea itambulisho hivyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mjasiriamali, Prisca Nyelo kutoka Bhigizimana Product kitambulisho chake cha Ujasiriamali Awamu ya pili 2020.

Na Dotto Mwaibale, Singida

Dkt.Nchimbi alisema vitambulisho vilivyotolewa kwa awamu ya kwanza ni 9,000 kati ya vitambulisho 55,000 vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wote wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungu, Edward Mpogolo alisema vitambulisho hivyo vya awamu ya kwanza katika wilaya hiyo wajasiriamali walichangia zaidi ya sh.milioni 100 na kuwa kwa awamu hii ya pili wamepanga kuwafikishia katika magulio yote, na kila maeneo walipo wafanyabiashara, masokoni na kwa wauza nguo.

Sunday, May 24, 2020

PATO LA TAIFA LITOKANALO NA KILIMO LAONGEZEKA KWA ASILIMIA 17 - WAZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma, leo tarehe 23 Mei 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Job Ndugai akisisitiza jambo wakati wa kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma, leo tarehe 23 Mei 2020. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi wakati wa hafla ya kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma, leo tarehe 23 Mei 2020. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Bi Khadija Ngolo ambaye ni Mkulima kutoka Kondoa wakati wa hafla ya kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma, leo tarehe 23 Mei 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Job Ndugai (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya AGRICOM, Wafanyakazi wa Mfuko wa Pembejeo za Kilimo -AGITF pamoja na wakulima wakati wa kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma, leo tarehe 23 Mei 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imebainisha kuwa sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Katika kipindi cha miaka mitano, Pato la Taifa linalotokana na kilimo, kwa kutumia bei za Mwaka 2015 limeongezeka kwa asilimia 17 kutoka Shilingi trilioni 25.2 Mwaka 2015 hadi Shilingi trilioni 29.5 Mwaka 2019.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amebainisha hayo leo tarehe 23 Mei 2020 wakati wa kukabidhi matrekta kwa wakulima wanaokopeshwa na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) katika Mji mdogo wa Kibaigwa Mkoani Dodoma.

Mhe Hasunga amesema kuwa sekta ya Kilimo imeendelea kutoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 58 Mwaka 2018, imechangia asilimia 28.2 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao imechangia asilimia 16.2.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa upatikanaji wa pembejeo zote za kilimo unakuwa kwa wakati zikiwemo mbegu bora, mbolea sahihi, viuatilifu sahihi na zana bora za kilimo.

Baadhi ya Mikakati ambayo Serikali imeiweka kwa lengo la kuinua kilimo nchini na kipato cha mkulima ni pamoja na kujenga miundombinu ya umwagiliaji,  kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mbolea, kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya uongezaji wa thamani ya mazao, kuimarisha mifumo ya uuzaji wa mazao, kuimarisha ushirika, kuimarisha huduma za ugani na mafunzo, kuwekeza katika utafiti wa kilimo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya uhifadhi wa mazao n.k.

Amesema kuwa katika Mwaka huu wa fedha 2019/2020, Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za kilimo (AGITF) imetoa mikopo 93 yenye thamani ya Shilingi 836,359,000 ikiwemo tisa (9) ya mitambo ya mashambani, 80 ya Pembejeo, mmoja (1) wa Ukarabati, miwili (2) ya Miundombinu ya Kilimo na mmoja (1) wa fedha za kuendeshea shughuli za shamba.

Amebainisha kuwa huo ni ushahidi tosha wa nia njema ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwasaidia wakulima nchini ili waweze kuondokana na kilimo duni kisicho na tija.

“Sanjari na hilo, Wizara imeendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo ili kuongeza ufanisi katika shughuli za kilimo. Kutokana na jitihada hizo za Serikali, Wizara kupitia Mfuko wa Pembejeo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 imetoa mikopo mbalimbali  yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 15.1 ambayo kwa pamoja imesaidia kuzalisha ajira takribani 864” Amekaririwa Mhe Hasunga

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai ametoa Rai kwa wananchi waliokopeshwa matrekta kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri kuzalisha ili waweze kufanya marejesho kwa wakati na kwa kiwango kilichoainishwa kwenye Mikataba ya mikopo yao.

Amesema kuwa Uaminifu katika marejesho ya mikopo yao utawawezesha kumaliza deni kwa wakati na kuepusha ongezeko la gharama linalotokana na riba ya adhabu.

Kadhalika, Spika Ndugai ameishauri Wizara ya Kilimo kuongeza muda kwa wakulima hao kuanza kurejesha mkopo ambapo amependekeza walau mwaka mmoja kuliko muda mchache wa miezi sita ambao umewekwa kwa sasa.

Pia Spika Ndugai ameishauri Wizara ya Kilimo kutathimini namna inavyoweza kujenga Mabwawa kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji katika Wilaya ya Kongwa.


WAZIRI MKUU ASALI SALA YA EID EL FITRI, KATIKA MSIKITI WA GADDAFI, JIJINI DODOMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Dini ya Kiislam, Mkoa wa Dodoma, wakati akiwasili katika Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, kuhudhuria Sala ya Eid el Fitri, May 24, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiitikia dua, baada ya sala ya Eid el Fitri, katika Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, May 24, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waumini wa Dini ya Kiislamu, waliyohudhuria katika ibada ya sala ya Eid el Fitri, akiitikia dua, baada ya sala, katika Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, May 24, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam, baada ya sala ya Eid el Fitri, katika Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, May 24, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, May 22, 2020

WAFANYAKAZI NFRA WAJADILI UFANISI WA KAZI NA MASLAHI YAO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro, leo tarehe 22 Mei 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA)

Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umejadili kwa kina ufanisi wa kazi pamoja na msisitizo kuhusu maslahi ya wafanyakazi.

Katika Mkutano wa Baraza hilo unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro kwa siku mbili wafanyakazi wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa kushirikishwa katika shughuli mbalimbali mara kwa mara ili kutambua majukumu yanayofanywa na Taasisi hiyo.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakifatilia mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro, leo tarehe 22 Mei 2020.

Kadhalika wafanyakazi wa Wakala wameomba kuendelea kujengewa misingi ya uwajibikaji hasa katika kutambua wajibu wao kwa Umma na kusisitiza kuwa watattekeleza majukumu yao pasina uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizindua Baraza hilo jana tarehe 21 Mei 2020 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya alisema si vema watumishi kutumia muda mwingi katika kufanya shughuli ambazo hazina tija zinazoathiri utendaji kazi.

Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo dhamira ya dhati ya kuondoa uzembe na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma na hivyo mtumishi anaruhusiwa kudai haki zile za msingi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu za Utumishi wa umma wakati wa kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa Mwajiri na kwa kutumia lugha ya staha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro, leo tarehe 22 Mei 2020. Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga (Kushoto) na Katibu wa Baraza la wafanyakazi wa NFRA Ndg Jesse Mgana. 

Katika siku mbili za Kikao cha Baraza wajumbe wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu Wakala na miongoni mwa ajenda hizo ni Kupitia Mpango wa Biashara wa mwaka 2020/2021 (Business Plan), taarifa ya utekelezaji ya robo ya tatu ya mwaka 2019/2020 na kupitia Rasimu ya Miundo mipya ya Maendeleo ya Utumishi.

Wajumbe wamejadili kwa kina agenda hizo muhimu kwa kuwa agenda ya kwanza imewapitisha katika malengo/mipango ya Wakala, ya pili ni utekelezaji wa majukumu ya Wakala uliofanyika kwa mwaka tulionao na tatu ni mpango wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa lengo ya kuandaa majukumu mapya yanayoendana na Muundo mpya wa Taasisi.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakifatilia mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro, leo tarehe 22 Mei 2020.

Na Mathias Canal, NFRA-Morogoro
Pamoja na kwamba wafanyakazi wa NFRA wamesisitiza umuhimu wa maslahi yao lakini kwa nyakati tofauti katika michango yao wamesisitiza kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo wao wana wajibu muhimu wa kutekeleza majukumu yao na ari kubwa.

“Kwa kutambua uzito na umuhimu wa majukumu hayo kila mmoja wetu katika sehemu yake ya kazi anatakiwa kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa wananchi kwa kuwezesha nchi yetu kufikia uchumi wa kati” Amekaririwa Meneja NFRA Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa amesema kuwa bado Taasisi ina changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu ya kutoa huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu wa kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa malengo.

Lakini amewahakikishia kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto hizo ikiwemo kuiomba itupatie watumishi ili kukidhi matakwa yetu.

Lupa amesisitiza kuwa Watumishi wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma. Aidha, Serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka maadili ya Utumishi wa Umma.