Matokeo chanyA+ online




Wednesday, January 27, 2021

SKAUTI JIJINI MBEYA WAKARABATI MAENEO YALIYO ATHIRIWA NA MAFURIKO


Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakikarabati kivuko cha watembea kwa miguu  katika Mtaa wa Mayombo Kata ya Iwambi baada ya kuharibiwa na mafuriko.

Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakiwajibika.



Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakisafisha mitaro

Kazi ikiendelea.
Kazi ikiendelea.

Na Dotto Mwaibale

 Kutokana  na mvua zinazo endelea kunyesha Mkoa  wa Mbeya na kuharibu miundombinu ya barabara Chama cha Skauti mkoani humo kimeendelea kutoa huduma ya kukarabati miundombinu hiyo kwa wathirika wa mafuriko.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Kamishna wa Skauti  Mkoa wa Mbeya, Sadock Ntole alisema  mvua iliyonyesha Januari 23 mwaka huu ilileta athari kubwa kSatika Kata ya Iwambi na kuharibu miundombinu mbalimbali.


Alisema kufuata hali hiyo walikaa na kuratibu namna ya kufika katika maeneo hayo kutoa msaada ambapo kikosi cha uokoaji cha skauti wapatao 16 walikwenda kutoa huduma ya kusafisha  mitaro na makaravati. 

 " Mafuriko hayo yalisababisha athari za kubomoa kuta za nyumba za wakazi wa tatu wa eneo hilo na kuharibu vivuko vya watembea kwa miguu na kuleta changamoto ya matumizi ya barabara kwa wakazi  na wanafunzi waishio mtaa wa Mayombo na mitaa jirani ambao wanasoma katika Shule ya Sekondari Sinai, Nsenga, Maziwa, Stella Farm na Shule ya mmMsingi ya Iwambi."  alisema Ntole. 

Mratibu wa Majanga, Uokoaji  na Hali hatarishi wa chama hicho mkoani humo, Lusajo Sanga alisema kazi hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano kutoka kwa viongozi wao.

Alisema kazi kubwa walioifanya ilikuwa ni kurekebisha miundombinu ya kupitisha maji ambayo ilijaa taka na kusababisha maji kutoka nje ya mkondo wake na kuingia kwenye makazi ya watu na kujenga  vivuko vya waenda kwa miguu. 

Alisema kazi hiyo walifanya kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mayombo akiwepo Mwenyekiti  Philipo Mbembati, Mjumbe wa mtaa huo, James Ngungula pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Sanga aliwataja skauti walioshiriki kazi hiyo kuwa ni Kamishna wa Skauti Mkoa Mbeya, Sadock Ntole, Mratibu wa Habari na Mawasiliano Mkoa Mbeya Barnaba Moses, Waratibu wa Skauti Wilaya ya Mbeya, Baraka Martin, Emanuel Mwasikili na Stephano Mwangosi.

Aidha Sanga aliwataja kwa majina  skauti waliounda kikosi kilichoshiriki kufanya kazi hiyo kuwa ni Evaristo Sanga, Glory Augustino, Beckam Frank, Elika Mwakabana, Skauta Macklin Lamsi, Elisha, Ckelvi Ekela, Bambo Ekela na Ali.

Sanga alitumia fursa hiyo kusema kwamba Skauti mkoani humo wapo tayari kutoa huduma kwa jamii pamoja na elimu ya jinsi ya kuepukana na athari zitakazotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa  huo.

Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock  Ntole alitoa rai kwa wananchi na wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya kuchukua tahadhari na kuhakikisha miundombinu ya mitaro na makaravati inayopitisha maji inakuwa Safi na salama wakati wote ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi katika mkondo wake ambapo pia aliwasisitiza wanaozalisha taka wazipeleke kwenye maghuba  sahihi ya kuhifadhia ili kurahisisha ubebaji wa taka hizo na kuzipeleka kwenye dampo kuu.

Monday, January 25, 2021

BALOZI WA UINGEREZA APONGEZA UBORA WA MAJI YA MKWAWA YA MKOANI IRINGA


Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar akinywa maji yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akiwa na wadau mbalimbali  wanaokuwanywa maji hapoBalozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la maji ya kunywa la kiwanda cha Mkwawa wakati wa maonyesho ya kibiashara ya mkoani Iringa yaliyofanyika katika chuo cha Mkwawa balozi David Concar alisema kuwa amepongeza uzalishaji bora wa maji hayo ambayo yamekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa afya ya binadamu.

Balozi Concar alisema kuwa amekunywa maji hayo na kugundua kuwa yanaradha ya maji hayo ambayo anaamini kuwa kila mtu atayeonja maji hayo lazima avutiwe kwa namna yalivyokuwa bora.

Alisema kuwa amevutiwa na bidhaa hiyo ya maji ya kunywa ya kampuni ya Mkwawa na kuahidi kuitangaza kokote Kule atakapokuwa ametembea kutoka na kuvutiwa na jinsi ya uzalishwaji wake ulivyokuwa na bora wa kimataifa.

Balozi Concar aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho cha uzalishaji wa maji kuhakikisha wanatanua na kijitangaza zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ametembea kwenye super market nyingi hajaona maji ya kampuni hiyo ambayo yeye anaamni kuwa in maji bora hapa nchini.

Akiwa ameambatana na balozi wa uingereza nchini Tanzania, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa amekuwa balozi wa kujitegemea kuyatangaza maji hayo kila kona ya Tanzania kutokana na ubora wake.

Alisema kuwa anamuomba balozi huyo Nate awe balozi wa kutangaza maji yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kutokana na ubora wake ambao maji hayo yanayo.

Kasesela aliwataka viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatanua wigo wa masoko ya bidhaa hiyo ya maji ya kampuni ya uzalishaji wa maji ya Mkwawa inayopatikana mkoani Iringa wilaya ya Iringa.

Alisisitiza wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kuendelea kunywa maji safi na salama yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa kutokana na ubora wake.

Kwa upande wao baadhi ya wanachi mkoani Iringa waliohudhulia katika maonyesho hayo yaliyofanyikia katika chuo cha Mkwawa waliyapongeza maji hayo safi na salama kwa kunywa kutokana na ubora wake.

Walisisistiza kuwa wataendelea kunywa maji hayo yaliyokuwa na ubora wa hali ya juu lakini wanatakiwa kuhakikisha wanaulinda na kuuboresha ubora wake ambao upo hadi hivi sasa.

Thursday, January 21, 2021

WAGANGA WA TIBA ASILI WATUMIE SUA NA WATAFITI WAKE KUBORESHA BIDHAA ZILIZOPO NA KUANZISHA MPYA


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa akifungua kongamano kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.

Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri akitoa salamu za kurugenzi yake kwenye kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini.

Mtafiti Mkuu wa mradi wa GRILI Dkt. Faith MabikiAkileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini. 

Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey  akitoa salamu za Ndaki yake na kuwakaribisha wageni hao Chuoni hapo. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa (Katikati) akisikiliza maelezo toka kwa viongozi wa mradi, Prof. Samweli Kabote amabye ni Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha  (Wa kwanza Kushoto) Akifuatilia hotuba ya ufunguzi, W KWANZA Kushoto ni Dkt. Geofrey Kalugila Rasi wa ndaki ya Solomon Mahlangu ya sayansi na Elimu. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa akiangalia maonesho ya bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kwenye kongamano hilo kabla ya maonesho rasmi siku ya ijumaa.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.


Na Calvin Gwabara,  Morogoro.


WAGANGA wa Tiba Asili nchini wametakiwa kuangalia kwa undani namna ya kutumia matokeo ya tafiti zinazofanywa na watafiti wa Chou Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi zingine ili kuboresha bidhaa zilizopo na kuanzisha bidhaa mpya ili kuendana na mahitaji ya jamii kwa wakati sahihi.

Wito huo ulitolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.

Prof. Mhairwa alisema kuwa njia hiyo ni muhimu sana hasa katika wakati huu ambao dunia inahangaika kutafuta chanjo na tiba ya ugonjwa wa COVID 19 ambapo dawa za mimea zimeonekana kufanya vizuri Zaidi kuliko za hospitalini,

” Wanasayansi na waganga wa tiba ya asili sio kama vyama viwili vya upinzani, sisi tunafanya kazi kwa kutegemeana, sisi tunavitu tunavumbua kisayansi lakini pia kuna vitu vingine tunavifanyia utafiti vile ambavyo mmevianzisha nyinyi ili kuweza kupata udani Zaidi wa dawa mnazogundua kwahiyo hatupingi kazi zenu wala msituone kama vile maadui sisi tufanye kazi kwa pamoja kwa faida ya jamii na taifa letu” Alisisitiza Prof. Mhairwa.

Alisema bidaa za mimea dawa zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na uzalishaji,uvunaji,utengenezaji,uuzaji na upatikanaji endelevu wa malighafi hivyo ili kupunguza changamoto hizo na kuzindoa kabisa kunahitajika utafiti Zaidi wa kisayansi,ubunifu Zaidi katika masoko,uzingatiaji wa hali ya juu wa vigezo vya ubora vinavyotakiwa na kufuata taratibu za biashara zenye tija.

Lakini pia aliwataka Wataalamu hao wa Tiba asili kuangalia masuala ya kisera yanayoleta changamoto katika kuhaulisha teknolojia hizi ili ziweze kutumika kibiashara na kuanzisha viwanda vya uzalishaji wa mimea dawa na hasa katika kipindi hiki ambapo sera ya serikali ni kusukuma uanzishwaji wa viwanda kwenye sekta hii.

Naibu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha aliwahakikishia kuwa SUA na hasa kurugenzi ya uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu kwa kushirikiana na serikali wataendelea kuwa nao bega kwa bega kwa kusaidia jitihada za wadau wote kwenye sekta hii katika kuboresha tafiti za oaina hii kwa kadri mazingira yatakavyoruhusu.

Akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri alisema kuwa kurugenzi hiyo na vitengo vingne vya SUA vimekuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya aina hiyo ili kujaribu kuboresha biashara za mazao ya Kilimo,Ufugaji na Misitu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hizo.

“Katika makongamano haya SUA imekuwa ikishirikisha wasimamizi na wakaguziwa ubora wa biashara hizi pamoja na watunga sera kwa ujumla na utaratibu huu umeongeza mchango mkubwa wa chou chetu katika kutatua changamoto mbalimbali na kuboresha biashara za mazao nah ii ni muhimu hasa katika awamu hii ya serikali ya tano ambayo mwelekeo wake ni kuwa uchumi wa viwanda.

Prof. Kashaigili alisema Vyuo Vikuu kote duniani ni vitovu vya maendeleo ya kitaaluma na Tafiti mbalimbali na kwa muktadha huo kurugenzi ya uzamili kupitia kitengo chake cha uhaulishaji wa teknolojia pamoja na mradi wa GRILI zimeona ni vyema kutumia uzoefu wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau wengine kuandaa kongamano hili hapa SUA ili kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili namna ya kukuza uelewa na kutatua changamoto hizo.

Akileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo Mtafiti mkuu wa mradi huo Dkt. Faith Mabiki amesema Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwaka 2018 ukiwa na lengo la kuchangia katika kuongeza ubora wa bidhaa za miti dawa ili kuboresha Maisha ya watengenezaji,afya za watumiaji na kuchangia katika pato la taifa.

Dkt. Mabiki alisema ili kufikia malengo hayo ya muda mrefu mradi huo unajenga uwezo wa kitafiti wa kitafiti kwa wanafunzi wa shahada za uzamivu 5 na shahada za uzamili 2 katika maeno muhimu ya kemikali,usugu wa dawa na masoko na unategemea kutoa matokeo ya kitafiti yatakayo tumika na wadau muhimu wa kuboresha biadhaa hizi.

“Kongamano hili la kitaalamu la wadau likiwa ni moja ya shughuli za uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa litajikita Zaidi kwenye kujadili Uboredhaji wa uzalishaji,uchakataji,ufungsdhsji na uuzaji wa bidhaa zinazotokana na mimea dawa hapa Tanzania na namna ya kutatua changamoto hizo” Alisema Dkt. Mabiki.

Kwa upande wake Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey  alisema kwa upande wa utafiti ndaki hiyo ni ya pekee inayotoa shahada ya uzamili ambazo zinajikita moja kwa moja katika utafiti wa mazao ya mimea dawa ambayo mojawapo inahusika katika tukio hili na ina miradi Zaidi ya tisa ambayo kwa namna moja au nyingine zinagusa bidhaa hizi za mimea dawa.

“Kwa sababu hiyo tunategemea kuchangia juhudi za SUA na Taifa katika kuongeza ubora wa bidhaa hizi ili zipate Masoko” Alisisitiza Dkt. Kalugila.

 Pia Dkt. Geofrey Kalugila aliwashukuru wadau hao kutoka maeneo yote nchini kufiki akushiriki kwenye kongamano hilo,maonesho na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu na kuwataka watumia siku chache watakazokuwa SUA kujifunza na kujionea mambo mbalimbali ya kistoria kwenye kampasi hiyo ambayo ilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa Afrika kusini.

Kongamano hilo litafuatiwa na Maonesho makubwa ya Tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye viwanja vya soko kuu la mkoa wa Morogoro tarehe 22/01/2021 na baada siku ya jumamosi kutakuwa na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za tiba asili litakalofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mahlangu Mazumbu tarehe 23/01/2021 zilizoandaliwa na Mradi wa GRILi.

Wednesday, January 20, 2021

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUJIELEZA KWA KUKIUKA MAAGIZO YA MAKAMU WA RAIS


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha kwa wadau wa mazingira alioambatana nao wakiwemo viongozi wa dini katika siku ya Upandaji miti kimkoa inayofanyika kila tarehe 19 mwezi JanuariMiongoni mwa Wadau wa Mazingira akiwemo afisa Zana za kilimo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Sebastian Kioyo pamoja na Kaimu Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ntera wakipanda miparachichi katika Shamba la Gereza la Mollo Manispaa ya Sumbawanga.Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justin Malisawa (kulia) akiwa na wadau wengine katika siku ya upandaji miti na uzinduzi wa upandaji miti ya matunda katika mkoa wa Rukwa wakiwa katika shamba maalum la kupanda miparachichi katika  Gereza Mollo. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyeshika Jembe) akimalizia kufukia mparachichi alioupanda kati ya miparachichi 100 iliyopandwa katika shamba la Gereza Mollo Manispaa ya Sumbawanga akiwa pamoja na wadau wengine walioshiriki katika uzinduzi wa upandaji wa miparachichi. 


Mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku tatu kwa wakurugenzi wa Halmshauri za Mkoa wa huo kujieleza kwa maandishi sababu za kushindwa kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshmiwa Samia Suluhu Hassan yaliyotolewa mwaka 2015 ya kuzitaka halmashauri nchini kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akifafanua kutoridhishwa huko Mh. Wangabo amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa zilipanda miti milioni 2.5 ambayo ni sawa na 43% huku mwaka 2019/2020 halmashauri hizo zikipanda miti milioni 1.6 ambayo ni sawa na 26% wakionesha kushuka maradufu katika utekelezaji wa agizo hilo na kuongeza kuwa hali hiyo haikubaliki na hivyo kuwaagiza wakurugenzi hao kutoa taarifa ya maandishi kueleza sababu za kushindwa kutekeleza agizo hilo.

“Tangu Mwaka 2015 ‘trend’ ya upandaji miti inashuka chini sasa tupo kwenye asilimia 26 ya miti milioni 6, tumepanda milioni 1.6 kwa mkoa mzima, lakini uharibifu wa mazingira huko ni kubwa sana, uharibifu wa ukataji wa miti ni mkubwa, kwa shughuli za mifugo, shughuli za ujenzi, shughuli za mkaa, miti inaangamia lakini hatupandi inayolingana na tunayoikata,” Alisema

Aidha aliongeza kuwa taarifa hiyo iambatane na mpango kazi wao unaoonesha kujipanga kwa utekelezaji wa agizo hilo kuanzia mwezi januari mwaka huu, mpango ambao utaonesha upandaji na  usimamizi wa miti hiyo mpaka mwezi wa nne mwaka 2021 na kisha kuwataka wakuu wa wilaya kufanya ukaguzi katika halmashauri zao ili kuhakikisha kwamba kila halmashauri imepanda miti milioni 1.5 na inasimamiwa.

“Mimi mwenyewe nimeonesha njia hapa leo tu tumepanda miti Zaidi ya 100, sasa kinashindikana kitu gani huko, wenyeviti wa vitongoji wapo huko, wenye viti wa vijiji wapo, watendaji wa vijiji na kata wapo, Tarafa wapo, maafisa ugani wote wapo, taasisi za shule zipo chungumzima, hizi tu peke yake ukizisimamia zikapanda miti mbona miti ni imgi sana, lakini juu ya yote kuna wadau wa mbalimbali wa mazingira tunao hapa,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika siku ya upandaji miti kimkoa inayofanyika tarehe 19 ya Mwezi wa kwanza kila mwaka huku akizindua rasmi upandaji miti ya matunda hasa miparachichi katika Gereza la Mollo na Kijiji cha Malonje kwaajili ya kuimarisha vipato vya gereza na wananchi kuwa na zao mbadala la kilimo kwaajili ya biashara, tukio ambalo limekusanya wadau mbalimbali wa mazingira Pamoja na viongozi wa dini mkoani humo.

Akitoa taarifa fupi ya upandaji wa miti katika Gereza la Mollo Manispaa ya Sumbawanga Mkuu wa Gereza hilo SP Englibert Chingalo alisema kuwa gereza lilipokea miche 655 kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa hadi kufikia tarehe 14.1.2021 na kusema “Tangu gereza la Mollo lianzishwe mnamo mwaka 1967 haijawahi kupandwa bustani ya miche ya matunda kama inavyofanyika leo, aidha miti hii ya matunda itakuwa ni faida kubwa kwa wafungwa, watumishi wa gereza Mollo Pamoja na jamii nzima inayotuzunguka.”

Kwa upande wake Meneja wa Msitu wa Mbizi Mkoani Rukwa Mohamed Kiangi alimuomba Mkuu wa Mkoa huo kuboresha program hiyo aliyoianzisha kwa kuhakikisha inakuwa na usimamizi bora wa miti inayopandwa hasa katika taasisi za serikali Pamoja na kwa wananchi kwa kuwa na takwimu za wapandao miparachichi hiyo huku halmashauri zikichangia gharama za uzalishaji wa miche kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) mkoani humo ili wakala hao wawe kitalu cha kuzalishia miti hiyo.

Aidha kwa upande wao viongozi wa dini, wamesifu juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa huo katika kuhamasisha upandaji wa miti ya matunda na kulifananisha tendo hilo na ibada na hivyo kumuomba asichoke kuendelea kuwahimiza wananchi kupanda miti hiyo ya matunda.

Askofu wa Kanisa la KKKT Ambele Mwaipopo wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika kwa mkoa wa Rukwa na Katavi alisema, “Mwenyezi mungu alipomuweka mwanadamu katika bustani ya Edeni alimuweka katika mazingira yaliyorafiki kwaajili ya kuendeleza uhai wake kwahiyo tendo hili la upandaji wa miti nit endo la kiibada, tendo la sifa na tuzo kwa Mwenyez Mungu, Kwahiyo tuko Nyuma yako mkuu wa Mkoa tutatangaza kwenye makanisa yet una misikiti yet una maeneo yetu ya ibada.”

Naye Katibu wa Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoani Rukwa alisema, “Kama alivyosema Baba Askofu Mwaipopo kwamba sisi kama viongozi wa dini jambo hili tumelichukua na tutalitangaza katika nyuma zetu za ibada makanisani na misikitini kuwahamasisha waumini wetu kupanda zao hili la miparachihci Pamoja na mazao mengi ne tukushukuru Mkuu wa mkoa kwa kuhamasisha mazao haya ambayo tulikuwa hatuyapi kipaumbele.”

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa mazingira mkoani humo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira Mkoani Rukwa Kapteni Mstaafu Mzee Zeno Nkoswe alisema kuwa mazingira ya Mkoa yamerudi nyuma na kuongeza kuwa kuna uwazi Zaidi ya km 200 kuanzia Kijiji cha Tunko Wilayani Sumbawanga hadi mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi.

“Tunafikiria kazi hii uliyoianzisha itatupa tena nguvu ya kuelimisha wananchi wetu kuhifadhi na kupanda miti na sisi NGO’s zetu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tunakuunga mkono kwa asilimia zote katika suala hili na tuziombe taasisi hasa za dini tusaidieni makanisani kuwaelimisha wananchi juu ya upandaji wa miti na uhifadhi wake,” Alisema.

Mti mmoja wa parachchi unakadiriwa kuzalisha matunda 500 huku bei ya tunda moja inakadiriwa kuwa Shilingi 500 na hivyo miparachichi 100 iliyopandwa katika Shule ya Msingi Malonje inakadiriwa kuzalisha matunda 50,000 ambayo thamani yake ni shilingi milioni 25 ambazo zinategewa kupatikana baada ya miaka mitatu, fedha ambayo inategemea kutumika katika matumizi mbalimbali ya shule hiyo.

Tuesday, January 19, 2021

RAIS MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MADINI YA NICKEL NA UWEKAJI JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MAZIWA KARAGWE

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko na Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka (wa tatu toka kushoto walioketi) pamoja na wanasheria wakishuhudia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Adelardus Kilangi na Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED ya Uingereza Bw. Chris Von Chritierson wakitia saini makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni hiyo katika uchimbaji wa madini ya Nickel katika mgodi wa Kabanga wilayani Ngara mkoa wa Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akibadilishana nyaraka na Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED Bw. Chris Von Christierson baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika uchimbaji wa madini ya Nickel huko Kabanga katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mjini Bukoba  Jumanne Januari 19, 2021

Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akionesha nyaraka akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED Bw. Chris Von Christierson  (katikati) na afisa wa kampuni ya LZ NICKEL LIMITED baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika uchimbaji wa madini ya Nickel huko Kabanga katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mjini Bukoba Jumanne Januari 19, 2021

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Bw. Jossam Ntageki wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha
Kahama Fresh mjini Karagwe  Jumanne Januari 19, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akisikiliza maeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo utaondeshwa na mwekezaji mzawa Bw. Jossam Ntangeki leo Jumanne Januari 19, 2021
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe unaoendeshwa na mwekezaji mzawa Bw. Jossam Ntangeki  Jumanne Januari 19, 2021
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Bw. Jossam Ntageki baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo utaondeshwa na mwekezaji huyo mzawa Jumanne Januari 19, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya utiaji saini Mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Lz Nickel limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo Ngara mkoani Kagera  tarehe 19 Januari 2021

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli  akiwashukuru Wananchi na kuwaaga mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Lz Nickel limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo mkoani Kagera  tarehe 19 Januari 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kyaka Misenyi mkoani Kagera wakati akielekea Wilayani Karagwe.

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba iliyopo Bukoba mjini mkoani Kagera muda mfupi mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya LZ Nickel limited  tarehe 19 Januari 2021.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba mara baada ya kuzungumza nao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba mara baada ya kuzungumza nao.

Sehemu ya Wananchi wa Kyaka Wilayani Misenyi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama kuwasalimia  tarehe 19 Januari 2021

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 19 Januari, 2021 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya LZ Nickel Limited juu ya uchimbaji wa madini ya Nickel yaliyopo Kabanga katika Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Hafla ya utiaji saini mikataba hiyo imefanyika Mjini Bukoba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David William Concar, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brig. Jen. Marco Gaguti.

Kwa upande wa Tanzania mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko na Msajili wa Hazina Bw. Athuman Mbuttuka na kwa upande wa LZ Nickel waliotia saini ni Makamu Mwenyekiti Bw. Chris Von Christierson na Mtendaji Mkuu Bw. Chris Showalter.

Serikali ya Tanzania na LZ Nickel Ltd zimekubaliana kuunda kampuni ya ubia iitwayo Tembo Nickel Corporation Limited ambayo itamiliki kampuni 2 ambazo ni Tembo Nickel Mining Company Ltd ambayo itajihusisha na uchimbaji wa madini ya Nickel huko Kabanga na kampuni ya Tembo Nickel Refinery Company Limited itakayojihusisha na usafishaji wa madini huko Kahama, Shinyanga.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Prof. Palamagamba Kabudi (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na timu aliyoiongoza kufanya majadiliano na kampuni ya LZ Nickel Ltd ambapo makubaliano yaliyofikiwa yameiwezesha Tanzania kuwa mwanahisa kwenye uwekezaji huo pamoja na kupata manufaa mbalimbali yakiwemo kugawana faida kwa 50/50, kodi na manufaa mengine kama inavyoelekezwa na sheria mbalimbali ikiwemo sheria mpya ya madini ya mwaka 2017.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika uchimbaji wa madini ya Nickel kutoka Kabanga kwa kuwa mradi huo haukuwa umetekelezwa kwa kipindi kirefu cha tangu mwaka 1976/79 ulipofanyiwa utafiti na kubaini kuwepo mashapo makubwa ya Nickel tena yenye ubora wa daraja la kwanza.

Amepongeza mpango wa kujenga mtambo wa kusafisha madini (Smelter) huko Kahama ambao amesema utasaidia madini yote yanayochimbwa kujulikana, mfano uchimbaji wa Nickel huambatana na madini mengine kama vile Cobalt.

Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Madini kuhakikisha mradi huu unatekelezwa haraka ili wananchi wa Ngara na Kahama waweze kunufaika.

Akiwa njiani kwenda Karagwe, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Kyaka katika Wilaya ya Misenyi ambapo amewaahidi kupanua kituo cha afya cha Kyaka na kuwa Hospitali, na ameeleza kutofurahishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Kyaka unaotarajiwa kugharimu shilingi Bilioni 15.1 na ambao umefikia asilimia 30 ya utekelezaji.

Mhe. Rais Magufuli ameagiza ndani ya kipindi cha miezi 13 ya mradi huo, uwe umekamilika vinginevyo mkandarasi na viongozi wanaosimamia watachukuliwa hatua.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na kusindika chakula cha mifugo (Kahama Fresh) kilichopo Karagwe.

Kiwanda hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kusindika lita 10,000 kwa siku na kitazalisha ajira 400 kinamilikiwa na Mtanzania Jossam Ntangeki ambaye anawekeza shilingi Bilioni 9 ikiwemo shilingi Bilioni 2.7 alizopata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TaDB).

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Bw. Ntangeki kwa uwekezaji huo na ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kuwekeza katika ufugaji na uzalishaji wa maziwa kwa kuwa mahitaji ya maziwa kwa Tanzania ni makubwa kuliko uzalishaji uliopo licha ya kuwa nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika.

Ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) inaongeza mifugo katika ranchi zake zote, na kwa maeneo ambayo haiyatumii wapewe wafugaji wengine na kwa gharama nafuu.

Mhe. Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutangaza haraka zabuni za ujenzi wa kilometa 60 za barabara ya lami ya kuanzia Karagwe kwenda Ngara, kilometa 50 za kuanzia Kyerwa kwenda Karagwe na barabara ya Nyakahura – Rusumo ambazo zimeainishwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/25.

Amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Mhandishi Andrew Kasamwa kukamilisha ujenzi daraja la Kitengule katika mto Kagera ifikapo Juni 2021 vinginevyo atachukua hatua kwa kuwa ujenzi wa daraja hilo umecheleweshwa kwa miaka 3.


Monday, January 18, 2021

NAIBU WAZIRI WAITARA AIAGIZA MANISPAA YA MOROGORO KUJENGA DAMPO LA KISASA ILI KUSIMAMIA VIZURI TAKA


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara (wa tatu kushoto) akiwa katika ziara kukagua dampo la Manispaa ya Morogoro lililopo eneo la Viwandani ambapo alielekeza lilejengwe dampo la kisasa katika eneo lingine.  

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Witara ameiagiza Halmashauri ya Morogoro kujenga dampo la kisasa katika eneo lingine na kuweka usimamizi mzuri wa taka.

Waitara alitoa agizo hilo mara baada ya kutembelea dampo eneo la Viwandani katika Manispaa hiyo na kukuta hali ya usimamizi wa taka isiyoridhisha wakati alipofanya ziara ya mkoani Morogoro kwa lengo la kukagua usimamizi wa mazingira.

 


 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akiangalia hali ya mazingira katika dampo la Manispaa ya Morogoro lililopo eneo la Viwandani alipofanya ziara ya kikazi ambapo alielekeza lilejengwe dampo la kisasa katika eneo lingine.  

Alisema hali katika dampo hilo si nzuri kutokana na kutokidhi vigezo la dampo vikiwemo kutokuwa na utaratibu wa kutenganisha aina za taka ili kuwa na usimamizi mzuri.

 “Hapa hakuna usimamizi mzuri hatuwezi kuwa na dampo la aina hii na ni ngumu control taka hapa kama mlivyosema mmetenga eneo la ekari 174 nawahimiza muandike andiko mpate fedha mjenge dampo la kisasa hapa hapafai na si rafiki kwa mazingira haya maji yakisambaa ni hatari kwa binadamu, wanyama na mazingira,” alitadharisha.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akitoa maelekezo wakati alipofanya kikao kazi na Maafisa Mazingira kutoka Mkoa wa Morogoro, Manispaa na Kata zake wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo Januari 16, 2021.

Pia naibu waziri huyo alisisitiza elimu itolewe hususan kwa vijana kutumia fursa ya kutumia taka zinazooza ili waweze kujiajiri kwa kutengeneza mbolea ya mboji kwa ajili ya shughuli za kilimo pamoja na bidhaa zingine.

Awali akizungumza katika kikao na maafisa mazingira wa mkoa, manispaa na kata za, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Waitara alielekeza kila shule ya msingi na sekondari kusimamia kila mwanafunzi apande mti.

“Naelekeza wakurugenzi wote wa wilaya na watu wa mazingira kwenye mikoa na wilaya kuhakiksha kila mwanafunzi anapanda mti, kwa wa shule msingi autunze kwa miaka saba na kwa yule wa sekondari atautunza kwa miaka minne awapo shule hili litasaidia katika si tu katika kutunza mazingira bali pia kupata vivuli na matunda,” alisema.

 

  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Bakari Msulwa akimkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye amefanya ziara katika Manispaa hiyo.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Aidha, Waitara aliwataka maafisa mazingira kuzitembelea klabu za mazingira zilizopo katika shule mbalimbali ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wanaounda klabu hizo kuendelea kushiriki katika utunzaji mazingira.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa alisema mikakati iliyowekwa wilayani humo ni kuelekeza kila mwanafunzi anayeanza shule akishirikiana na mzazi wake kupanda mti mmoja na kuutunza.

Msulwa alisema kuwa kwa wastani kila shule inapokea wanafunzi takriban 200 na hivyo wanaamini watapata idadi hiyo ya miti na kuwa kwa kufanya hivyo watasaidia kampeni ya kupanda miti kushika kasi.