Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema ,
Serikali inatarajia kufanya usanifu wa barabara ya Morogoro- Dodoma
yenye urefu wa kilometa zipatazo 259 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019
kwa ajili ya kupata michoro na gharama halisi ili kujengwa upya kwa
viwango cha ubora na mahitaji ya sasa .
Naibu
Waziri alisema hayo mjini Morogoro alipofanya ziara ya ukaguzi wa
matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali kutoka Dodoma hadi
Moropgoro yakiwemo ya Kibaigwa , Gairo na kuangalia shughuli za
ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara ya
Morogoro- Dodoma .
Alisema
, licha ya kuendelea kuihudumia barabara kuu hiyo , kwa sasa
Serikali imekuja na mpango mwingine wa kufanya usanifu kwa mwaka wa
fedha wa 2018/2019 ili kupata michoro ambayo itaelezea gharama halisi
ya kujenga barabara mpya katika kiwango cha ubora na mahitaji ya sasa.
Naibu
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda
suti) akipata maelezo ya Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya
Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia) alipokagua shughuli za ujenzi wa
mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara kuu ya
Morogoro- Dodoma hivi karibuni na ( anayemfuatia Naibu Waziri ) ni
Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi
Doroth Mtenga.
Naibu
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda
suti) akisisitiza jambo wakati akikagua shughuli za ujenzi wa mizani
mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara kuu ya Morogoro-
Dodoma hivi karibuni na ( wapili kushoto) ni Meneja wa Wakala wa
Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Doroth Mtenga.
Naibu
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda
suti) akikagua shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la
Dakawa Magereza barabara kuu ya Morogoro- Dodoma hivi karibuni
akiongozwa na Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya Ambicon ,
Mustafa Kasmir ( kulia) akiambatana na Meneja wa Wakala wa Barabara (
TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Doroth Mtenga ( wapili
kushoto) pamoja na Wakala wa Mradi kutoka Kampuni ya Group Six
International Ltd , Mhandisi Abdallah Rashid.( Picha na John Nditi).
Naibu
Waziri alisema, Serikali inatenga fedha nyingi kila mwaka fedha kwa
ajili ya ukarabati wa barabara kuu ikiwemo ya Morogoro- Dodoma ili
ziweze kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo ambapo kwa
baabara hiyo iliyojengwa miaka zaidi ya 30 iliyopita kwa hali yake ya
sasa imechakaa na kuzeeka.
Akizungumzia
ujenzi wa mizani , Naibu Waziri alisema , Serikali itaendelea kujenga
mizani ya kisasa katika barabara kuu nchini ambayo itapunguza
msongamano wa magari na kuharakisha usafirishaji wa mizigo , abiria
na pia kulinda barabara .
Naibu
Waziri alisema ,mizani ya kisasa inayojengwa na iliyopo
itakatoboreshwa ili ikidhi utoaji wa huduma zote muhimu kama vituo vya
Polisi, TRA, ukaguzi wa magari, upimaji wa ulevi kwa madereva ,
kuengesha magari na maeneo ya kupumzika madereva .
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi
Doroth Mtenga alisema, ujenzi mzani hiyo ya kisasa ulianza Oktoba
25, 2017 kwa gharama ya Sh bilioni 14. 784 fedha zilizotolewa na
Serikali kuu na hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 70 na kiasi
cha malipo kwa mkandarasi kilicholipwa ni Sh bilioni 5.7 sawa na
asilimia 40.
Mhandisi
Mtenga alisema , mradi huo wa ujenzi wa mizani mbili za kisasa za
kupima magari , eneo la Dakawa Magereza una majengo mawili ya ofisi,
vibanda viwili vya Polisi , vinne vya mlinzi na vyoo viwili na ni moja
wapo ya hatua za kudhibiti na kupunguza uharibifu wa barabara kutokana
na magari kuzindisha uzito.
“
Hapa kutakuwa na mzani miwili mmoja utapima magari yakiwa kwenye
mwendo mdogo na utarekodi na kuhifadhi taarifa zote za gari husika na
gari itaruhusiwa kuendelea na safari iwapo hajazidisha uzito na ikiwa
uzito umezidi litaelekezwa kwenda kupima kwenye mzani wa kawaida kwa
uthibitisho” alisema Mtenga.
Hta
hivyo alisema , ujenzi huo ulipangwa ukiamilishwe ifikapo Januari 24,
2019 , lakini kutoka na kuchelewa kupata eneo la upande mmoja wa
ujenzi kwa zaidi ya miezi sita ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa
mkandarasi kutokana na ardhi kumilikiwa na Taasisi mbili tofauti za
Serikali .
Mhandisi
Mtenga alisema , kwa sasa mkandarasi wamewasilisha ombi la kuongezewa
muda hadi Aprili 24, 2019, na kwamba Wakala utaendelea kumsimamia ili
ujenzi huo ukamilishwe kwa wakati katika muda wa nyongeza ulioombwa.
No comments:
Post a Comment