Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi na wajumbe wa
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani)
wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao makao makuu
ya bodi jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa
Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa, akieleza majukumu ya Bodi kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo
na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya
bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald
S.B. Ndagula akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi
na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi
na Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na
Masilahi katika Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji
kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi
na Wajumbe wa Bodi hiyo ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa
Umma cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo
jijini Dar es Salaam.
Watumishi
na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
wametakiwa kutofanya kazi kimazoea katika kutekeleza jukumu lake la
msingi la kuishauri Serikali namna bora ya kuoanisha na kuwianisha
mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuwavutia
na kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma ili waweze kuwahudumia
vizuri wananchi katika Taasisi za Umma.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya
Mishara na Masilahi katika Utumishi wa Umma makao makuu ya bodi hiyo,
wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji,
kufahamu majukumu ya bodi na kujiridhisha namna bodi hiyo inavyotekeleza
majukumu yake.
Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, yeye ni muumini wa ufuatiliaji hivyo
atakuwa akifanya ziara za kushtukiza katika ofisi za Bodi ya Mishahara
na Masilahi katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kujiridhisha na
utendaji kazi wa bodi hiyo, hivyo amewataka watumishi hao kubadilika na
kuachana na utendaji kazi wa kimazoea ili bodi hiyo iwe na tija na
manufaa kwa watumishi wa umma nchini.
Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, pamoja na kuwataka watumishi na
wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa uzalendo, uaminifu na uadilifu
lakini pia amewataka kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili
kuisadia Serikali ya Awamu ya Tano kutimiza azma yake ya utoaji motisha
kwa watumishi wa umma ili waweze kuwa na ari ya utendaji kazi.
Aidha,
Dkt. Mwanjelwa amewataka wajumbe wa bodi ambao ni wastaafu na wazoefu
katika utumishi wa umma, kila mmoja kwa nafasi yake kutoa mchango
utakaowezesha bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa wakati, na
kuongeza kuwa, yeye binafsi anaamini kwa uzoefu wa wajumbe wanaounda
bodi hiyo, Serikali itapata ushauri bora wa kuoanisha na kuwianisha
mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini.
Kwa
upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi
katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa amesema kuwa, lengo la
kuanzishwa kwa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni
kuwa na chombo kimoja cha kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi
ya watumishi wa umma ili kuwa na mfumo endelevu unaoondoa malalamiko
kuhusu masilahi miongoni mwa watumishi wa umma kwa lengo la kuwavutia na
kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma.
Bibi
Mwanilwa ameeleza kuwa, hivi sasa bodi inafanya utafiti wa hali ya
masilahi na uhusiano wake na mifumo ya upimaji wa utendaji kazi katika
Utumishi wa Umma na kuongeza kuwa, utafiti huo unafanywa ili kubaini
uhusiano uliopo kati ya utoaji wa motisha mbalimbali na utendaji wa kazi
kwa lengo la kuwavutia na kuwabakisha watumishi wa Umma.
Bibi
Mwanilwa amefafanua kuwa, kwasasa hatua inayoendelea katika utafiti huo
ni uchambuzi wa taarifa za utafiti huo, hivyo bodi inatarajia
kuwasilisha taarifa hiyo serikalini ifikapo mwezi Februari, 2019.
Naye,
Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma,
Bw. Donald S.B. Ndagula amesema bodi yake inamtambua Dkt. Mwanjelwa kama
mlezi, hivyo amemhakikishia kuwa, imepokea nasaha, ushauri na melekezo
aliyoyatoa na ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote.
Bodi
ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu
wa Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 1977 na kuundwa kwa Hati ya Rais iliyotolewa kwenye Tangazo la
Serikali Na. 162 la tarehe 3 Juni, 2011.
No comments:
Post a Comment