Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Shria Prof. Sifuni Mchome aliesimama
akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria
nchini uliozinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati
akizundua ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar
es Salaam leo, kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa
ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam
leo kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Wajumbe
wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini katika picha ya pamoja
na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu
Mhe. Prof. Ibrahim Juma baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar
es salaam leo
Na Sheiba Bulu
Wizara
ya katiba na Sheria imezindua ushirikiano wa Mamlaka Kuu za Sheria
nchini zitakazokaa pamoja kubainisha uwezo na changamoto zinazoikabili
sekta ya sheria nchini na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa sekta
hiyo na hivyo kutoa mchango stahiki kwa taifa.
Ushirikiano
huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) na kuhudhuriwa na Jaji Mkuu Mhe. Prof
Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni
Mchome.
Akizindua
ushirikiano huo Prof Kabudi amewataka wajumbe wa ushirikiano huo
kufahamu kuwa wajumbe wote kwa ujumla wao wanajenga nyumba moja na
wautumie ushirikiano huo kama chachu na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa
sekta ya sheria nchini ili iweze kutoa mchango wa kweli kwa Taifa.
“Sekta
hii ni moja, wote hapa mnajenga eneo moja, tumieni ushirikiano huu kama
chachu ya kuleta tija na ufanisi kwa sekta hii na muwe huru kushauri na
kuzungumza ili kuifanya sekta ya sheria ambayo ni sekta mtambuka kutoa
mchango wa kweli kwa taifa hili,” alisema Prof. Kabudi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma ameipongeza
Wizara kwa kuanzisha ushirikiano huo hasa ikizingatiwa kuwa sekta ya
sheria ndio mama wa sekta zote nchini kwani sekta zote zinatumia sheria
kujiendesha.
Amesema
Ushirikiano ulioanzishwa utawezesha kuwepo kwa mashauriano baina ya
mamlaka za sheria ili pamoja na mambo mengine utawezesha kuwa na msimamo
mmoja juu ya masuala mbalimbali na pia utawezesha kutumika kama njia ya
haraka ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta na kwa nchi kwa
ujumla.
“
nipongeze kwa kuzindua ushirikiano huu, ni kitu kizuri kitawezesha
kufanyika kwa mashauriano kwa pamoja na kutoka na msimamo mmoja kama
timu, ushirikiaano huu unaweza kutumika kama njia ya haraka ya kutatua
jambo na hivyo kutoa ushauri wa haraka kwa sekta husika kwa taifa na
hata kwa uongozi wa nchi,” alisema Prof. Juma.
Ushirikiano
huo unaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mwenyekiti na
wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma
Wizara ya Katiba na Sheria, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria-
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa
Mashtaka, Wakili Mkuu wa Serikali
na Kabidhi Wasii Mkuu.
No comments:
Post a Comment