Mwanamitindo
na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss
Universe, Marisela De Montecristo amewasili nchini usiku wa kuamkia kwa
lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya
Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha.
Marisela
amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
kwa ndege ya shrike la ndege la KLM na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro ,Anna Mghwira.
Akizungumza
na Waandishi wa habari Marisela ambaye ni raia wa nchi ya El Salvador
aliyehamia Los Angels, Marekani amesema lengo la kuja nchini kutembelea
vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika
sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza.
Marisela
ambaye ameongozana na mchumba wake pamoja na mama yake mzazi akaeleza
nia yake ya kuja Tanzania ikiwemo kukuza uchumi kupitia utalii ,elimu
kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania . Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna
mghwira amesema hii ni fursa adhimu ambayo nchi nyingi zenye vivutio vya
utalii zimekua zikitamani hasa kwa kutembelewa na watu mashuhuri Kwani
kupitia kwao inasaidia kutangaza utalii Duniani. Mwenyeji wa ugeni huo
,Dennis Meela akaeleza namna alivyo fanya ushawishi kwa Mwanamitindo
huyo hadi kuamua kuja Tanzania.
Mwanamitindi
huyo kesho (Januari 18) ataanza safari ya kwenda katika Hifadhi ya
Taifa ya Tarangire ambako atakaa hapo kwa siku moja na baadae kuelekea
Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro
Creator).” Mwanamitindo huyo anakuja kujifunza baadhi ya vivutio
anavyotaka kuvitumia kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa akiwa
ameongozana na na kundi la watu wanne akiwemo mama yake mzazi na mpenzi
wake ambaye ni Mwanasheria nguli nchini Marekani.
Baada
ya safari ya siku mbili katika hifadhi hizo atarejea Moshi Januari 22 na
kutembelea moja ya kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu
na kuona namna ya kuweza kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu. Mwaka jana Merisela ameshiriki mashindano ya ulimbwende nchini
El Salvador na kufanikiwa kutwaa taji la hilo (Miss El Salvador 2018).
Pia
amewahi kushiriki mashindano ya Best National Costumes na kufanikiwa
kushika nafasi ya pili ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Brazili
na ya tatu Panama. Merisela anamiliki Taasisi binafsi ya kuwasaidia
watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Marekani.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa na Mwanamitindo
na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss
Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa
kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi
ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza jambo na na Mwanamitindo
na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss
Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa
kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi
ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akimpokea Mwanamitindo
na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss
Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa
kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi
ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
No comments:
Post a Comment