Mwenyekiti
wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Hassan Wakasuvi akijitambulisha wakati wa
mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini ambao umefanyika leo
mkoani Tabora
Baadhi wa Wakuu wa Wilaya na wadau wa tumbaku nchini wakiwa katika mkutano wa Kitaifa wa wadau wa tumbaku leo Mkoani Tabora.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwashukuru wajumbe wa mkutano wa
kitaifa wa wadau wa tumbaku kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho
cha siku moja kilichofanyika mkoani humo leo.
Mkoa
wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za mkoa huo wakati wa mkutano wa
kitaifa wa siku moja wa wadau wa Tumbaku nchini leo .
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa
Tumbaku nchini leo mkoani Tabora uliokuwa ukijadilia masuala mbalimbali
ikiwemo kuongeza uzalishaji. Picha na Tiganya Vincent
SERIKALI
imeziagiza Bodi zote zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo kuanza mara
usajili wa wakulima wa mazao yote na zihakikishe zinawapa vitambulisho
kwa ajili ya kuwatambua na wanapofanyika kazi zao ili iwe rahisi
kuwahuduma.Hatua hii inalenga kuwatambua na kuwasaidia kuboresha kilimo
chao ili waweze kupata huduma za uhakika kwa ajili ya manufaa yao na
Taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akifungua
mkutanowa kitaifa wa mwaka wa wadau wa sekta ya Tumbaku Tanzania.
Alisema hatua inalenga kuwatambua wakulima wote na maeneo ambayo
wanalima ili kuwaondoa na kilimo cha kujikimu na kuelekea katika kilimo
cha kibiashara na kisasa.
Hasunga
alisema hadi hivi sasa ni Bodi ya Tumbaku pekee ndio imesajili wakulima
na kuwapa vitambulisho. “Lazima tuanze kuwatambua wakulima wetu walipo,
mashamba wanayolima na ukubwa wake na mazao wanayolima na kiwango mazao
ambacho wanatarajia kuzalisha ” alisisitiza.
Hasunga alisema lazima shughuli ya kilimo ianzie kutambulika kama zilivotaaluma nyingine
Alisema
kukosekana kwa takwimu halisi za wakulima , ukubwa wa mashamba yao na
walipo kumesababisha kuwa vigumu huduma muhimu kwa ajili ya kuboresha
kilimo kuwafikia na kusababisha wapatiwe huduma za kitaaalamiu ambao
halizingani na mahitaji yao na wakati mwingine sio halisi.
Waziri
hiyo wa Kilimo aliongeza kuwa nguvu kubwa lazima ielekezwe katika
kuwasaidia wakulima kulima cha kisasa kwa sababu ndicho kinatoa ajira
kubwa kwa Watanzania ambapo asilimia 65 ya wananchi wamejiari katika
kilimo na asilimia 8 wanashughulika na biashara inayotokana na mazao ya
kilimo.
Katika
hatua nyingine Hasunga amegiza Bodi ya Tumbaku Nchini na wadau wa zao
hilo kuhakikisha wanasaidia kuinua zao la Tumbaku ambalo limeshuka na
kupoteza uongozi wa kuwa zao linaloingiza fedha nyingi za kigeni.
Alisema
uzalishaji umeshuka kutoka tani 126,0000 kwa msimu wa mwaka 2010/11
hadi kufikia tani 54,800 kwa msimu 2018/19 na kuongeza kuwa hata wastani
wa bei umeshuka kutoka wastani wa Dola 2.11 kwa msimu wa mwaka 201/11
na kufikia Dola 1.72 mwaka 2018/19. Hasunga alisema ni lazima Bodi ya
tumbaku na wadau wengine kuja na mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao
hilo ambalo siku za nyuma lilikuwa likiongoza kuingiza fedha za kigeni
nchini.
Alitaja
mikakati ni pamoja na kutafuta wanunuzi wengine sehemu mbalimbali ili
kuongeza ushindani wa bei na kumnufaisha mkulima na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Hassan Wakasuvi
alisema kuwa moja ya mambo ambayo yatawezesha kuleta mabadiliko katika
sekta ya tumbaku ni marekebisho ya Sheria ya tumbaku. Aliwataka wadau
kuwa tayari kutoa maoni yao wakati ukiwaidia ili kuwepo na Sheria nzuri
No comments:
Post a Comment