Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza
jambo kwa wajumbe wa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la
Posta Tanzania wakati akifungua rasmi kikao hicho, Dar es Salaam.
Wakisikiliza kwa makini viongozi wa Shirika hilo, wa kwanza kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali mstaafu Dkt. Haruni Kondo na wa kwanza kulia
ni Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania Kanali mstaafu Dkt. Haruni Kondo
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Isack Kamwelwe (wa kwanza kulia) wakati wa kikao cha Baraza Kuu la
Wafanyakazi wa Shirika hilo. Anayesikiliza kwa makini ni Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizarani, Kitolina Kippa.
Posta
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwelwe ( wa pili kushoto) baada ya ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la
Wafanyakazi wa Shirika hilo, Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali mstaafu Dkt. Haruni Kondo na wa tatu kulia ni
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizarani, Kitolina
Kippa (wa tatu kulia)
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta
Tanzania wakiimba wimbo maalumu wa wafanyakazi kabla ya ufunguzi wa
kikao hicho uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani)
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati
mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania baada
ya kufungua kikao hicho, Dar es Salaam. Viongozi wa Shirika hilo wakiwa
kwenye picha hiyo, wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Kanali mstaafu
Dkt. Haruni Kondo na wa nne kulia ni Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang’ombe
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ameuagiza
uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kurudisha mali zote za
Shirika hilo ikiwemo viwanja, majengo ndani ya miezi sita zilizopo
kwenye maeneo mbali mbali nchini nzima
Kamwelwe
ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha 26 cha Baraza Kuu la
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania kilichofanyika Dar es Salaam
ambacho kimejumuisha viongozi na wawakilishi wa Baraza hilo kutoka mikoa
yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo Shirika hilo lina mtandao wa
miundombinu yake na inatoa huduma za mawasiliano ya posta, vifurushi na
vipeto kwa wananchi
“Ifikapo
tarehe 30 Juni mwaka huu wa 2019 mali zote za Shirika ziwe zimerudi
kuwa mali ya Shirika la Posta Tanzania, hata kama mliuziana zirudi, hizi
ni mali za Serikali na ninyi hamtakuwa wa kwanza kurudisha majengo,
viwanja kwa kuwa wenzenu wa Shirika la Reli Tanzania wamerudisha,”
amesisitiza Kamwelwe
Pia,
ameuagiza uongozi wa Shirika hilo ndani ya kipindi hicho cha miezi
sita, kuhakikisha kuwa Wilaya zote 186 nchi nzima ziwe na huduma za
posta. Aidha, amewataka kupitia kikao cha Baraza hilo, wajadiliane
kuhusu utekelezaji wa jambo hilo na bajeti watakayoijadili iwe na
mwelekeo huo. Amesisitiza kuwa TPC ina watumishi wengi wapatao 821 nchi
nzima hivyo wafanyakazi kazi kwa bidii, wawe wabunifu na wachape kazi
kwa kuzingatia taaluma zao ili kuongeza ufanisi, tija, ukuaji na
maendeleo ya Shirika ili waweze kuwahudumia wananchi. Amewaagiza
kuhakikisha kuwa wanatumia mifumo ya kielektroniki kusafirisha fedha
badala ya kutumia mfumo wa zamani wa wafanyakazi kushika pesa za mauzo,
makusanyo na mapato mkononi
Amesema
kuwa anaushukuru uongozi wa Shirika hilo kwa kuendelea kulipa deni la
wastaafu ambalo limefikia kiasi cha shilingi bilioni 6.5 na amewaahidi
kushirikiana nao ili Serikali iweze kurudisha fedha zao na amekiri kuwa
Shirika limeiokoa Serikali na kuficha aibu hiyo. Pia, amewaahidi
kulifanyia kazi deni la shilingi bilioni 12 ambapo amesema kuwa
anahitaji kuelimishwa ili alielewe aweze kwenda kuwafahamisha wabunge
ili waridhie na watoe kibali cha kulipa deni hilo
Katika
hatua nyingine, ameuelekeza uongozi wa Shirika hilo kutumia miundombinu
ya postikodi iliyopo sehemu mbali mbali nchini ili kufanikisha na
kuharakisha utoaji wa huduma za mawasiliano ya posta kwa wateja wake kwa
kuwa watanzania wana imani na Shirika lao na lina mtandao mpana nchi
nzima
“Huduma
ziwafikie watu wa vijijini haraka ili kuwapunguzia gharama na kero za
kwenda mjini kufuata huduma ili kurahisisha uendeshaji wa kila siku wa
maisha ya wananchi na mafanikio ya Shirika hili yaguse watanzania wote,
ikitokea umepoteza nyaraka, mteja lazima ajibiwe haraka, kama umepoteza,
lipa,” amesisitiza Kamwelwe.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Kanali mstaafu Dkt. Haruni Kondo
amemweleza Kamwelwe kuwa Shirika halijapewa mtaji na Serikali ila
anawapongeza wafanyakazi kwa ushirikiano wao na kwa kulifikisha Shirika
hapo lilipo kwa kuwa wanadai deni la shilingi bilioni 6.5 Serikalini kwa
kulipa wastaafu
“Deni
tunaloidai Serikali la kulipa wastaafu linatutesa sana, tunajua nguvu
zako, tunakuomba utusaidie”, amesisitiza Kondo. Pia, ameongeza kuwa
anamuomba Kamwelwe alisaidie Shirika kuondolewa kwenye orodha ya
mashirika ya umma yaliyowekwa chini ya uangalizi ili Shirika liweze
kutekeleza majukumu yake kwa kuwa ni Shirika kubwa ambalo limelala
Akitoa
taarifa ya Shirika hilo kwa Kamwelwe, Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo,
Hassan Mwang’ombe amesema kuwa tayari Shirika limejiunga na mfumo wa
malipo wa Serikali kwa njia ya kielektroniki (eGPG) ili mteja anapolipia
alipie kwa urahisi na kuliwezesha Shirika kuona mapato yake yote kwa
njia ya mtandao kwa kuwa malipo yatakuwa yanafanyika kwa njia ya
kielektroniki na huduma zitaanza ndani ya wiki moja
No comments:
Post a Comment