Wafanyakazi
wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi zao kwa
umoja, kuwasaidia wahitaji na kuwatendea haki wagonjwa wanaotibiwa
katika Taasisi hiyo.
Rai
hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula
alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Dar es
Salaam.
Dkt.
Chaula alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni ngumu na ni ibada hivyo
basi kutokana na matendo mema watakayowatendea wagonjwa ambao ni
wahitaji Mwenyezi Mungu atawalipa kwa kuwajalia afya njema ili waweze
kuwahudumia kwa miaka mingi zaidi.
“Nawapongeza
sana kwa kazi mnayoifanya ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya
moyo, kazi hii ni ngumu jambo la muhimu ni kuwa na upendo baina yenu
na wagonjwa mnaowahudumia. Hakika Mwenyezi Mungu atawalipa kwa huduma
yenu mnayoitoa”, alisisitiza Dkt. Chaula.
Alimalizia
kwa kuwataka wafanyakazi hao kufanya kazi zao kwa bidii, wakati na
kutimiza wajibu wao kwani hakuna kisichowezekana katika kutoa huduma
bora kwa wagonjwa vitu vyote vipo ndani ya uwezo wao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea Taasisi hiyo na kuona huduma
za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Prof.
Janabi alisema idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo
imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kutoa mfano wa wagonjwa wa nje
8557 waliotibiwa mwezi wa kwanza ukilinganisha na wagonjwa 7222
waliowaona mwezi wa Desemba mwaka jana.
Alisema
idadi ya wagonjwa wanaolazwa imeongezeka kutoka wagonjwa 282 kwa mwezi
wa kumi na mbili mwaka jana hadi kufikia 312 waliolazwa mwezi wa kwanza
mwaka huu.
“Tunaona
wagonjwa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ila wagonjwa
wetu wengi zaidi wanatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya,
Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Pemba,Katavi, Kigoma Kilimanjaro,
Lindi, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma,
Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Unguja ”, alisema Prof. Janabi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akimwelezea Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya, Dkt. Zainab Chaula jinsi duka la
dawa linavyohudumia wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo
wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na baadhi ya
wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara
yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za
matibabu ya moyo wanazozitoa.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wakati wa
ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za
matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Godfrey Mbawala akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt.
Zainab Chaula jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua
kwa watoto kutumia mtambo wa Cathlab wakati katibu mkuu huyo
alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara
kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiangalia moja ya chumba cha VIP
kilichopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara
yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za
matibabu ya moyo wanazozitoa. Kutoka kulia kwa Katibu mkuu ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
No comments:
Post a Comment