Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Atashasta Nditiye amegawa kompyuta 25 kwa shule za sekondari za
Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa
lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunzia na waalimu kufundishia,
kuongeza uelewa na kupata maarifa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuunganisha kompyuta hizo na mtandao wa
intaneti ili kuwawezesha wanafunzi wa Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha
ufaulu
Nditiye amekabidhi kompyuta hizo kwa
Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa
ili ziweze kutumika kwenye shule mbali mbali zilizopo Wilayani humo
“Nimeleta
kompyuta 25 ili zigawiwe kwenye shule mbalimbali ili watoto wajifunze
kutumia TEHAMA pamoja na waalimu waliopewa mafunzo ya TEHAMA na taasisi
yetu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)”, amesema Nditiye.
Kompyuta hizo zimetolewa na UCSAF ambayo inahusika na ufikishaji wa
huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara
Nditiye ameongeza kuwa Wilaya ya Ludewa
inafahamika katika kipindi cha miaka ya nyuma kwa kuwa moja ya Wilaya
saba nchini ambapo wanafunzi wake wana kipaji cha akili ukilinganisha na
Wilaya nyingine zilizopo nchini ambapo ameona ni vema kuwapatia
wanafunzi wa shule za Wilaya hiyo kompyuta hizo ili waweze kuongeza
ufaulu, kujenga uelewa na kupata maarifa ili waweze kuwa wanafunzi
vinara kama iliivyokuwa imezoeleka katika kipindi cha miaka ya nyuma.
Pia, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika matumizi ya TEHAMA katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mara baada ya kupokea kompyuta hizo kwa
niaba ya wananchi, Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa alimuomba Mkuu wa
Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere kuwa, kuwe na kituo kimoja cha kutunga
mitihani Ludewa ili waalimu watunge mtihani wa aina moja na waweze
kumaliza kufundisha masomo ya kiada na ziada kama walivyopanga kwa
muhula husika wa masomo ili waweze kuwapima wanafunzi wote kwa pamoja
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Andrea Tsere
alimueleza Nditiye kuwa wataweka intaneti kwenye kompyuta hizo ili
waalimu na wanafunzi waweze kupata notisi. Pia, amesema kuwa kompyuta
hizo zitatumika kuinua kiwango cha elimu na zimefika muda muafaka
“Mmetusaidia sana, umeingia kwenye akili
yangu ya kuinua kiwango cha elimu Ludewa,” amesisitiza Tsere wakati
akimshukuru Nditiye kwa kuzipatia shule za Wilaya yake kompyuta 25.
Tsere amewataka waalimu wakuu wa shule kuzitunza kompyuta hizo na
kuzifanyia matengenezo pindi inapohitajika badala ya kuacha ziharibike
na pasipo kuzipanga vizuri kwa sababu ni vifaa vya Serikali badala yake
wanapanga lini wavichukue badala ya kuzitunza vizuri ili zisaidie
wanafunzi wengi na kwa muda mrefu. Aidha, amesisitiza kwa waalimu hao
kuwa kompyuta zikipotea na wao wapotee
Katika hatua nyingine, Nditiye amewaeleza
wananchi hao kuwa, Wizara yake ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kupitia UCSAF imetoa ruzuku kwa kampuni ya simu ya Halotel na Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili wajenge minara 11 kwenye maeneo ya
mwambao kwa wananchi waishio Wilayani Ludewa kwa kuwa hawana
mawasiliano.
“Tunahitaji Ludewa iwasiliane na dunia,”
amesisitiza Nditye. Amefafanua kuwa minara tisa imejengwa na kampuni ya
Halotel na miwili ni ya TTCL
Vile vile, ameongeza kuwa, ujenzi wa meli
ya abiria waishio Ludewa kwa ajili ya usafiri wa Ziwa Nyasa umekamilika
ambapo kwa sasa meli hiyo inafanyiwa majaribio kabla ya kuanza safari
zake na Serikali inakamilisha ujenzi wa gati za kushusha na kupakia
abiria kwenye mwambao wa ziwa hilo kwenye maeneo ya Manda, Lupingu,
Nsele, Yiga na Nkanda ambapo meli hiyo inatarajiwa kuanza safari zake za
kutoka Ludewa, Njombe hadi Kyela, Mbeya mwezi Aprili mwaka huu
“Tunataka Lupingu hadi Matema watu wapite
kwa lami,” amefafanua Nditiye. Ameyasema hayo wakati akiongea na
wananchi wa Ludewa mjini na kuwaeleza kuwa azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano ni kuhakikisha kuwa barabara ya Lusitu – Mawengi yenye urefu wa
kilomita 50 inajengwa kwa kiwango cha zege kwa gharama ya shilingi
bilioni 159 ambapo tayari mkandarasi wa kutoka nchi ya Korea yupo na
anaendelea na ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kupitisha madini ya
Mchuchuma na Liganga
Ngalawa amewaeleza wananchi kuwa
anamshukuru Nditiye kwa kuwa alifanya ziara kutoka Lupingu hadi Manda
mwaka jana mwezi wa tatu akiwa na miezi minne tu tangu alipoteuliwa kuwa
Naibu Waziri na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa wananchi waishio
mwambao na sasa minara 11 imejengwa ambapo tayari minara mitatu ya
Nkanda, Mawengi na Mahong’olo imewashawa na meli ya abiria pia itaanza
safari zake
Tsere alimshukuru Ngalawa kwa kumleta
Nditiye ambapo alisafiri na boti siku nzima Ziwani mwaka jana mwezi wa
Machi na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa kuwa tangu dunia iumbwe
wananchi wa mwambao hawajawahi kupata mawasiliano na sasa wanawasiliana
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment