Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili Igunga mkoani
Tabora
Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo
atatembelea Wilaya zote saba (7) za Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge,
Kaliua, Urambo na Tabora .
Lengo
la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi,
kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo
kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika
katika ziara.
|
No comments:
Post a Comment